Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,796
- 5,509
Tumesoma kwenye vyombo vya habari kuwa IPTL/PAP wameomba leseni ya kuendelea kuzalisha umeme ambao inauuza Tanesco. IPTL/PAP imekuwa mjadala mkubwa kitaifa tangu kuingia nchini miaka ya 1990 hadi sasa kwani imehusishwa na ufisadi uluohusisha viongozi, wanasiasa, wanasheria, na wafanyabiashsra. Ni IPTL/PAP ambayo ilihusika kutoa rushwa kwa majaji, waziri, viongozi wa dini n.k.
Ni kashfa za ufisadi wa IPTL/PAP ndio uliosababisha kuvuliwa madaraka kwa Waziri Tibaijuka na Prof. Muhongo awamu iliyopita, ni kampuni hiiihii iliyosababisha kashfa ya Escrow na kusababisha Bunge kuja na azimio maalumu kwa serikali.
Kuna wakati lilitolewa azimio kuwa serikali iinunue IPTL na kugeuza mitambo yake ili itumie gesi na wapewe Tanesco lkn katika hali ya kushangaza serikali ilitugeuka na IPTL kumilikishwa kwa PAP ili kuendeleza wizi dhidi yetu.
Lakini kama wasemavyo wahenga, hakuna marefu yasiyo na ncha, sasa muda wa leseni umeisha na IPTL/PAP wanalazimika kuomba upya leseni ya kuzalisha umeme nchini.
Humu JF wapo Watanzania wa aina zote: Wanasiasa-mawaziri, wabunge na hata rais wa nchi, tupo wafanyabiashara, wakulima, wasomi, na wananchi wa kawaida. DG wa Ewura , Felix Ngalamgosi anapitia humu, Msemaji wa Ewura-Titus Kaguo umo humu, bodi na wajumbe wa bodi ya Ewura mmo humu, wanasheria mmo humu.
Hivyo basi, hapa kuna uwakilishi wa kutosha wa moja kwa moja wa watanzania.
Sasa tupige kura, Je, IPTL/PAP wapewe leseni tena?
Vv