Je eti diclopar ina madhara kwa watumiaji?

Diclopar ni mchanganyiko wa paracetamol na diclofenac. Side effects ni pamoja na abdominal pain, diarrhoea, nausea and vomiting, skin rash na tinnitus
Hapo ulichokuwa unakionyesha ni show off kwamba unailewa hyo dawa lakn hujajbu swali
 
MADHARA MAKUBWA NA YA MOJA KWA MOJA NI KUPOTEZA KUMBUKUMBU KUSAHAU KWA MFANO UNAWEZA KUWA UNAITAZAMA SAHANI UNAIJUA LAKINI JINA LAKE KUWA NI SAHANI UNALISAHAU NA UNAWEZA FIKIRI UMETAMKA SAHANI KUMBE UMETAMKA KIJIKO
 
Diclopar ni mchanganyiko wa paracetamol na diclofenac. Side effects ni pamoja na abdominal pain, diarrhoea, nausea and vomiting, skin rash na tinnitus
Mleta uzi nilivyomuelewa mimi anataka atajiwe madhara ya muda mrefu(longrun effects) ya kutumia Diclopar na siyo side effects!........ Side effects ni suala la kawaida kwa dawa,karibia kila dawa ina side effects ambalo huwa ni suala la muda mfupi tu!

Sent from my Armor using JamiiForums mobile app
 
Mleta uzi nilivyomuelewa mimi anataka atajiwe madhara ya muda mrefu(longrun effects) ya kutumia Diclopar na siyo side effects!........ Side effects ni suala la kawaida kwa dawa,karibia kila dawa ina side effects!

Sent from my Armor using JamiiForums mobile app
Ameshajibiwa mkuu wapo walienda shule hapa
 
Ameshajibiwa mkuu wapo walienda shule hapa
Sawa mkuu, nilishtuka kwa sababu suala la side effects huwa ni la muda mfupi tu(wakati wa kutumia dawa) kwa hiyo hatuwezi kuliita kuwa ni madhara ambayo ni significants!!

Sent from my Armor using JamiiForums mobile app
 
MADHARA MAKUBWA NA YA MOJA KWA MOJA NI KUPOTEZA KUMBUKUMBU KUSAHAU KWA MFANO UNAWEZA KUWA UNAITAZAMA SAHANI UNAIJUA LAKINI JINA LAKE KUWA NI SAHANI UNALISAHAU NA UNAWEZA FIKIRI UMETAMKA SAHANI KUMBE UMETAMKA KIJIKO
Mmmh

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Sawa mkuu, nilishtuka kwa sababu suala la side effects huwa ni la muda mfupi tu(wakati wa kutumia dawa) kwa hiyo hatuwezi kuliita kuwa ni madhara ambayo ni significants!!

Sent from my Armor using JamiiForums mobile app
Kwakua zinafanya efferent neurotransmitter s numb can cause memory loss in the long run.
 
Sky eclat pm tafadhali

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kama uzi tajwa hapo naomba kujuzwa madhara ya diclopar Kama kidonge cha kutuliza maumivu mfano mtu anapoumwa na Jino akiweka kwenye jino linalouma Mara moja maumivu yanakata afu pia hua nasikia mama aliyejfungua kwa oporeshen haruhsiw kutumia ikiwa nyuzi bado hazijatolewa.


Nawasilisha
Kesho nikiwa na time nitapita kujaza waliyoyasema wenzangu,kifupi Kama alivyosema Sky eclat ,Dawa hii ni mchanganyiko wa dawa mbili,Diclofenac na Paracetemol,nitaoongea juu ya paracetamol ambayo ikitumiwa kwa dozi kubwa zaidi ya 3gm kwa siku itaweza kusababisha madhara gani na pia Diclofenac zaidi ya 200mg kwa siku itasababisha nini.Kesho wadau tukiwa wazima.
 
Kama uzi tajwa hapo naomba kujuzwa madhara ya diclopar Kama kidonge cha kutuliza maumivu mfano mtu anapoumwa na Jino akiweka kwenye jino linalouma Mara moja maumivu yanakata afu pia hua nasikia mama aliyejfungua kwa oporeshen haruhsiw kutumia ikiwa nyuzi bado hazijatolewa.


Nawasilisha
Ok niliaahidi natafafanua kidogo ninachokifahamu juu ya hii Dawa,Diclopar kama Diclopar naona SkyEclat kishaisema.
Tuelimishane kidogo juu ya neno madhara yanayotokana na matumizi ya dawa,hapa kitaalamu wanayagawanya katika sula mbili,"Side effect & adverse effect"
Side effect
Haya ni madhara mwambata ambayo mgonjwa anatarajiwa kuyapata pindi anapotumia dawa fulani,na dawa hiyo iko katika dozi sahihi inayotumiwa na mgonjwa,madhara haya huwa yanajulikana /yanategemewa kumpata mgonjwa,mfano ukimeza pirton ili kutibu mafua ,madhara mwambata ni kiusingizi ,ukimeza flagyl utapata shida ya radha kinywani kubadilika pamoja na kichwa kuuma ingawa .nk.Madhara haya hayaepukiki na kiwango cha athari hizi kutokea inategemea mtu na mtu.

Adverse drug effect/ adverse drug events
Haya ni madhara mabaya(harmfull) yasiyotegemewa ambayo yanaweza kumpata mgonjwa wakati wa matumizi ya dawa katika dozi sahihi.Madhara haya hutoa tahadhari/onyo ya matumizi ya dawa husika habo baadae.ikiwa ni pamoja na kupunguza dozi ya dawa husika,kuacha matumizi kabisa na kutumia dawa nyingine kama mbadala.

Hii inaweza kupangwa katika muonekana wa madaraja yasiyopungua sita;



    • Matokeo mabaya kulingana na kiwango cha dozi aliyotumia mgonjwa-Dose related(augumented)
    • Madhara yanayompata mgonjwa bila kujali kiwango cha dose-Non dose related (Bizare)
    • Madhara ya muda mrefu -Dose related & time related (Chronic)
    • Madhara yanayompata mgonjwa kulingana na muda aliotumia dawa mgonjwa-time related(Delayed)
    • Madhara baada ya kuaacha dawa -Withdraw (End use)
    • Madhara kutokana na dawa kutokutoa matibabu kwa mgonjwa-Therapy failure.

Mtazamo wa madhara haya mawili uko hivi;
side effect-namna gani dawa inaweza kuleta matokeo mabaya mwambata kwa mtumiaji .
Adverse effect -Namna gani mtumiaji wa dawa husika amepata madhara kutokana na matumizi ya dawa fulani.

Diclofenac
Ni dawa inayotumika kwa matumizi makuu ya msingi-kupunguza uvimbe (antiinflamatory),kupunguza maumivu(Analgesic),shida za mifupa ( osteoarthritis) , na viungo (Rheumatoid arthritis) na pia shida ya Gout.
Diclofenac iko katika kundi la acetic acid,hivyo kiasilia pamoja na kuwa na uwezo wa kutuliza maumivu,kuondoa uvimbe dawa ni asidi asilia.Utaratibu wake wa kufanya kazi huzuia utengenezwaji wa vichocheo vinavyoitwa "Prostaglandins" amabavyo humfanya mgonjwa kupata hisia za maumivu pamoja na kuchochea taaratimbu za kuleta uvimbe mwilini.kupitia njia ya Cox,
Pamoja na kuwa ni kisababishi cha hayo niliyoyataja hapo juu,bado prostaglandini (PGs) ina manufaa mengi mwilini kulingana na aina husika ya PGs , inahusika katika kulinda ukuta wa tumbo (Gastric mucosa),Prostaglandin husaidia mji wa mimba kuwa na mazingira yanayosaidia mlango wa uzazi kufunguka pamoja na mji wa mimba wa mama mja mzito kusinyaa wakati uchungu anapotaka kujifungua,PGs pia husaidia utengenezwaji wa TXa ambayo ni muhimu kwa ugandishaji wa damu.
sitataka kwenda ndani kwenye hili cha msingi tutizame baada ya Prostaglandin kuzuiwa na utengenezwaji wake mtu anapotumia Diclofenac nini kinafuata:

Manufaa:
  • Hisia za maumivi hutoweka (analgesia) na mgonjwa hataweza kusikia maumivu.
  • Umvimbe kupungua na kuisha(Hii itatengemea na kisababishi pamoja na muda mgonjwa atakaotumia dawa) /Antiinflamatory effect.
Damu kuwa nyepesi (through inhibition of Cox no PGs no TXa as blood coagulation factor),wagonjwa wenye shida za moyo na sickle cell crisis huwa wanapewa dawa za familia hii ili kuifanya damu iwe nyepesi mfano ni Apirin junior.

Madhara :
  • maumivu ya tumbo,Choo kuwa kigumu,kiungulia, kama vile Kupata vidonda vya tumbo hii ni baada ya kuzuia utengenezwaji wa PGs.(Mengine wadau washaeeleza)
  • Kuzuia ugandishwaji wa damu,mgojwa anaweza kupata excessive bleeding.
  • Kwa mama mwenye uchungu wa kujifungua hali hii itachelewesha kutokana na zuio la utengenezwaji wa PGs.
Pracetamol
Lengo kuu la kuunganisha Paracetamol na Diclofenac ni kupata matokeo bora ya tiba (Supra additive) yenye dhamira ya kuweza kupunguza joto(kushusha homa ),kupunguza uvimbe na maumivu mwili kwa uzuri kabisa bila kuwa na idadi ya vidonge vingi.
Diclofenac haifanyi vizuri kwenye kupunguza jote la mwili,"hyperthemic" lakini ni dawa bora kwenye kupunguza maumivu na uvimbe ,wakati huohuo Paracetamol haifanyi vizuri kwenye kupunguza uvimbe lakini inafanya kazi vizuri sana kwenye kushusha joto la mwili "potent antipyretic" pamoja na maumivu.
Ufananisi wa Paracetamol(Panadol)
Paracetamol hufanya kazi kwenye mfumo wa fahamu ili kupunguza joto na maumivu ya mwili kama Diclofenac kwa kuzuia utengenezwaji wa PGs(Centrally) ,haina athari kwenye utaratibu wa ulinzi wa ukuta wa tumbo,kwenye ugandishwaji wa damu wala haina athari kwa uchungu wa mama mja mzito,kifupi ni salama zaidi ukilinganisha na Diclofenac.

Madhara
Umeng'enywaji wa Paracetamol hupitia mifumo miwili katika ini (Phase I & Phase II-Glucoronic conjugation).Unapotumia hii dawa kwa Dozi kubwa (mf.zaidi ya 3gm kwa siku kwa mtu mzima) inamaana kiwango cha dawa inayopita kwenye ini kwa ajili ya kumeng'enywa kitakuwa kingi kuzidi uwepo wa vimeng'enya na mwisho wa siku seli za ini zitaharibiwa na kiwango hicho kikubwa cha dawa.
Madhara makuu ya Pracetamol ni kwenye ini (Hepatotoxicity) ambayo unaweza usiyaoone leo lakini yakatokea hata baada ya miaka 10>.
Nimejaribu kutoa maelezo kwa kifupi,wenye ueelewa zaidi watapita kujazia nyama.
 
D
Kama uzi tajwa hapo naomba kujuzwa madhara ya diclopar Kama kidonge cha kutuliza maumivu mfano mtu anapoumwa na Jino akiweka kwenye jino linalouma Mara moja maumivu yanakata afu pia hua nasikia mama aliyejfungua kwa oporeshen haruhsiw kutumia ikiwa nyuzi bado hazijatolewa.


Nawasilisha
Hii Dawa inatakiwa kunywa wala si kuweka kwenye eneo husika lenye tatizo,isipokuwa utafanya kwa product ambayo ni "special for application on the localized area"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom