Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,917
- 24,674
Je, Duniani tumekuja kama Adhabu baada ya kufanya Makosa mbinguni?
Kabla ya baadhi yetu kuja Duniani inawezekana sisi binadamu wote makazi yetu na Nyumbani kwetu kwa Asili ni mbinguni,
Na hapa duniani ni kama Gerezani tu tunakuja baada ya kufanya makosa huko tunaletwa hapa ili kutumikia kifungo cha Adhabu (Gerezani).
inaonekana Nyumbani kwetu kwa Asili ambako ni mbinguni kuna Teknolojia ya Hali ya juu na ndio maana ukihukumiwa kifungo chako unaletwa gerezani ambako ni duniani kwa namna ya Ajabu bila kujitambua
Kwanza unafutwa kumbukumbu zako zote halafu unaletwa duniani (kifungoni) kama mtoto, utaishi kulingana na muda uliohukumiwa kutumikia
Na baada ya kumaliza kifungo chako Unakufa na kurudi utokako (Mbinguni) kama Roho alafu kwa sababu ya ukubwa wa Teknolojia iliyopo kule Roho yako inarudishwa kwenye umbo lake na kuruhusiwa kuendelea kuishi na jamii yako,
Wapo watakaouliza kama hii ni kweli inakuaje kwa wale watoto wanaotolewa mimba kabla ya kuzaliwa kifungo chao kilikuwaje?
Hapa jibu ni kwamba kule mbinguni kwenye Nchi yetu ya Asili hukumu zake zinatolewa kulingana na ukubwa wa kosa ulilolitenda,
Mfano kuna Ambao waliohukumiwa wiki mbili Gerezani, Mwezi, siku na ndio hao (Mimba) zinazotolewa(kifungo kimeisha wanarudi mbinguni )
Na kuna ambao waliohukumiwa miaka kadhaa (Ndio sisi tuliozaliwa ishi na wengine kuzeeka). Kifungo kikiisha tunakufa tunarudi tulikotoka.
Kuna ambao wamehukumiwa kifungo na Mateso makubwa, Kuna wa vifungo tu, pia kuna wale wamehukumiwa vifungo na kazi nzito.
Na ndio maana Duniani (Gerezani ) kila binadamu anaeishi ana Shida zake, ndio maana binadamu hatuko sawa tunatofautiana,
Ni kwa sababu hapa ni Gerezani kila binadamu anatumikia kifungo chake kwa mujibu wa hukumu na makosa aliyoyafanya akiwa Mbinguni.
Siku tukimaliza Vifungo Vyetu tunarudi kule tulikotoka kujumuika na Jamaa zetu.