Je dr Batilda Buriani ataiweza Dar?

Abraham

Senior Member
Oct 9, 2008
115
11
Wadau, kuna tetesi kuwa Batilda Buriani anaweza kupewa U-RC Dar, je atauweza?
 
Wadau, kuna tetesi kuwa Batilda Buriani anaweza kupewa U-RC Dar, je atauweza?

Kwanini Batilda na wala siyo Masha, Diallo, Marmo, Shamsa Mwangunga, Prof. Msola, Paul Kimiti, Mzindakaya, Chiligati, Khatibu?
 
mmmh hapo atachemsha saaaana tu labda wampe huko mkoani


Kwani anapewa ili aweze? Mbona hamuelewi, anapewa ili aweze kujikimu kimaisha, suala siyo kuweza. Kwani ni nani mwenye rekodi ya kuiweza Dar akiwa kama Mkuu wa Mkoa?
 
Hanged.jpg
 
Unapaswa kuelewa kwamba CCM na Serikali yake haiangalii uwezo wa mtu katika utendaji bali kinachoangaliwa ni MASLAHI yagawanywe namna gani ndani ya wenye chama na serikali. Batilda ni mtu wa karibu kwa vigogo wengi wakubwa ndani na nje ya serikali ya sasa hivyo basi hatutashangaa endapo atapewa ULAJI HUO. Batilda aligombea jimbo la Arusha Mjini akashindwa pamoja na jitihada na nguvu nyingi kuifanywa na vigogo ashinde ikashindikana. Katika mchakato huo wa uchaguzi fedha nyingi za vigogo pamoja na zile za Batilda mwenyewe zilipotea ili kuzirudisha ni muhumu kumweka katika nafasi nyeti kama ya Dar ili walichopoteza katika uchaguzi yeye na watu wake waweze kurudisha. Hivyo basi swala si uwezo bali ni mtu wetu kupatiwa nafasi yenye kipato na ULAJI ili kurudisha fedha zilizotumika kununua kura na vilevile kutengeneza ziada kwa ajili ya 2015.
 
Duh! au apelekwe arusha akapambani na Lema kama JK alivyofanya kule kwa Mwakyembe na Mwakipesile
 
Hata Asijaribu maana atakuwa amemmaliza kisiasa. Historia inasema wanawake wote walio wahi kuwa Ma RC DSM wamekwisha kisiasa. unamkumbuka Mary Chipungahelo?
 
Sababu zitakazofanya Batilda apewe nafasi ya URC Dar ni kwamba Mwana mama huyu yupo katika hali mbaya kifedha kutokana na mchakato wa kura za jimbo la Arusha. Madeni aliyonayo hayalipiki mwanangu. Si Masha, Diallo, Shamsa, Msola, Kimiti, Mzindakaya, Chiligati, wala Khatibu walio na shida aliyonayo Batilda. vilevile nafasi aliyokuwa nayo awali haikuwa na ulaji wa kutosha. Huwezi kumlinganisha na Shamsa ambale alikuwa Wizara ya utalii na maliasili- Kumbuka kwa Shamsa Makusanyo ya siku moja tu ya watalii wanaopita Gate la Ngorongoro Conservation Area yanamtosha kuishi yeye na uko wake miaka ishirini bila kufanya kazi, hivyo kwa kuwa ni mwanachama wa genge la walanchi lakini hana tatizo alilonalo Batilda na ndio maana msaada unahitajika kununusu maisha yake kwa kupewa nafasi nyeti ya URC Dar.
 
Hata Asijaribu maana atakuwa amemmaliza kisiasa. Historia inasema wanawake wote walio wahi kuwa Ma RC DSM wamekwisha kisiasa. unamkumbuka Mary Chipungahelo?

siungi mkono batilda kuwa RC dar ila historia unayosema kwa kumtaja mtu mmoja tu? labda tutajie na mwanamke mwingine aliyewahi kuwa RC dar na akafa kisiasa. Hatumtaki huku aende Arusha
 
kwani we hujui weakness ipo wapi haswa

Mijadala mingine inawaponza wanasemwa hata kama mwenye mamlaka alikuwa na mpango wa kumfikiria, kila mtu anastahili kupata mkate wake wa kila., ataupataje na wapi nayejua ni mola wake.
 
Back
Top Bottom