Rais Wa 16 Wa Marekeni Abraham Lincoln Alieleza Demokrasia Kama Serikali Ya Watu, Kwa Ajili Ya Watu Na Iliyowekwa Na Watu. Kwa Kipindi Hiko Alipokuwa Anaelezea Demokrasia Alikuwa Akifafanua Umuhimu Wa Uhuru Kamili Kwa Wamarekani Na Alifanikiwa Kukomesha Utumwa Kwa Wamarekani Na Kuwaunganisha Pamoja Na Kuwa Taifa Kubwa Sana Kama Tunavyoliona Leo.
Miaka Mingi Demokrasia Imekuwa Ikitumika Kama Njia Ya Kuleta Upatanisho Baina Ya Pande Mbili Ama Zaidi Na Imeonekana Kuleta Matunda Kwa Sehemu Hizo Na Hatimaye Suluhu Kupatikana.
Leo Hii Demokrasia Imekuwa Ikitumika Ndivyo Sivyo Na Limegeuka Chaka La Kuficha Agenda Za Siri Za Mabeberu. Demokrasia Imekuwa Ikifananishwa Na Uhuru Usio Na Mipaka. Watu Wafanye Watakavyo Ndio Huitwa Demokrasia?. Hakuna Serikali Yeyote Ambayo Inampa Raia Wake Uhuru Usio Na Mipaka Na bado Zinaitwa Nchi Za Kidemokrasia hata Marekani haimpi raia wake uhuru usio na mipaka.
Hali Ni Tofauti Kwa Nchi Za Kiafrika Ambako Sheria Zikiwekwa Ili Kulinda Mipaka Ya Uhuru Wa Watu , Nchi Za Mabepari Hudai Hakuna Demokrasia. Na Ndio Maana Nimesema Demokrasia Ni Chaka La Kuficha Agenda Za Siri Za Mabepari Kwa Sababu Mabepari Wanajua Kuwa Mipaka Ya Watu Huwekwa Kwa Mujibu Wa Sheria Na Taratibu Za Nchi Na Kwa Kuwa Hawana Uhuru Wa Kuingilia Sheria Za Nchi Huru Basi Hutumia Hilo Chaka La Demokrasia Kuhalalisha Mawazo Yao.
Karibu Nchi Zote Ambazo Mabepari Waliingia Kimabavu Na Kuwatoa Viongozi Wake Madarakani Waliingia Kwa Gia Ya Kuminywa Demokrasia.
Utu Wetu Wa Kitanzania Bado Haujawa Tayari Kukubaliana Na Baadhi Ya Matendo na tamaduni za kigeni kama Ushoga Na Usagaji Na Kisheria Mtu Anayefanya Matendo Hayo Ni Muhalifu Lakini Mabeberu Wanataka Kuhalalisha Ushoga Na Usagaji Na Mambo Mengine Yaliyo Kinyume Na Sheria Za Nchi Yetu Kwa Kigezo Cha Kuminya Demokrasia Ambazo Mimi Naziita Agenda Za Siri.
Upatikanaji Wa Taarifa Ni Muhimu Kwa Kila Mtu Lakini Serikali Ikazuia Upatikanaji Wa Taarifa Zisizo Sahihi Kwa Sababu Taarifa Inapotolewa Inasikika Na Kila Mtu Hata Mtoto Mdogo. Taarifa Zisizofaa Si Vizuri Kusikiwa Na Watoto Wadogo Kimaadili Hivyo Serikali Ina Jukumu La Kudhibiti Taarifa Hizo Ili Kulinda Maadili Ya Nchi Yetu.
Serikali ya tanzania inajaribu kuweka mipaka ya uhuru kwa watu wake kupitia sheria na taratibu na si kuminya demokrasia. Demokrasia isitumike kama chaka la kuficha agenda za siri za mabepari pale nchi inapotenda kwa mujibu wa sheria na taratibu zake.
Labda mimi ndio sijui kama demokrasia inampa uhuru usio na mipaka mtu lakini kama demokrasia haimpi mtu uhuru usio na mipaka wacha serikali yetu idhibiti uhuru huo kupitia sheria na taratibu zilizowekwa.
demokrasia isitumike kama njia ya kukwamisha nchi yetu kufuata taratibu na sheria tulizojiwekea bali itumike kama njia ya kutafuta maamuzi ya pamoja
Karlo Mwilapwa