Je Dawa za minyoo zinatoa mimba?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Dawa za minyoo zinatoa mimba??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jul 2, 2009.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  Wandugu wapendwa,
  poleni sana na kazi za ujenzi wa taifa na kujitafutia mkate wa kila siku.
  Ninaishi na girl friend wangu ambaye siku ni mfanyakazi wa kampuni moja ya bima hapa DSM.
  Wiki iliyopita aliniambia kuwa amepata ujauzito na anahisi una umri wa mwezi mmoja.
  binafsi nilifurahishwa sana na taarifa hizo kwani sasa ka umri kamekimbia na sina hata mtoto wa kusingiziwa. Lakini mwenzangu hakuwa anaonekana amefurahishwa na jambo hilo la ujauzito wake na akanishauri kuwa atoe, nikagoma.
  leo ameamka mapema sana na ameniaga kuwa anaenda kununua dawa za minyoo zinazoitwa Zentel.
  Je hizo dawa haziwezi kuharibu ujauzito wake?
  NA NI NINI MADHARA YA DAWA HIZO KWA MTU MWENYE UJAUZITO MCHANGA KAMA HUO WA MWEZI MMOJA?
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  sina utaalam wa kitabibu lakini huyo mwenzi wako amewahi kusumbuliwa na tatizo lolote na akahisi ana minyoo? amewahi kwenda hosp?kama ni mjamzito asinywe hizo dawa mpaka ashauriwe na daktari. umewahi kumuuliza kwa nini hataki kuzaa kwa sasa na mpaka anataka kutoa huo ujauzito?

  NB:kwa nini unaendelea kukaa na binti wa watu bila ndoa? maana hapa umesema ni gf wako.
   
 3. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bwana Bujibuji, this is very interesting my dear, amekwambia kuwa ana mimba lakini akakushauri kuwa anataka kutoa. Hivi kutoa si ndio abortion? au nakosea? What does this mean so far? Sitaki kukukatisha tamaa lakini chunguza kwanza kuhusiana na uhalali wa hiyo mimba kama ni ya kwako au la. Kwa fikira zangu nilitegemea huyu GF wako angefurahi kusikia wewe umeipokea hiyo mimba kwa moyo mkunjufu
   
 4. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  pole sana mkuu nilishawahi kukutana na situation kama hiyo.mchumba wangu alikuwa na mimba na hakuwa tayari kuzaa,nilijitahidi sana kumconvince yeye alichokuwa anataka ni abortion tu.Sababu nilikuwa nahitaji mtoto tena wa kwanza mda wote nilikuwa na hofu ya mimba kutolewa,hata alipokuwa akiniaga anakwenda mjini nilichokuwa nawaza ni hicho tu,aliyenisaidia alikuwa ni bestfriend wake ambaye alimwambia ukitoa mimba bila ruhusa ya mwenye mimba waweza kufa na akamwambia watu wengine kwenye koo zao mimba zao huwa hazitoki ukizitoa waweza kufa hivyo itabidi ushauriane na mwenye mimba.Alipokuja kwangu alijifanya kunitega kwa maswali kama kwetu watu wanakufaga kwa kutoa mimba.sababu best yake alishaniambia mchezo wote aaah kwangu ilikuwa kama kuua tembo kwa ubua.nilimpa takwim za uongo tena huku machozi yakinilengalenga.now i am a dad of three months healthier baby!!.Dawa za minyoo hazitoi mimba ila kwa ushauri Hasinywe dawa yoyote bila ushauri wa daktari sababu mimba ni special case na hata wauza madawa hawakubali kutoa dawa kwa wajawazito bila cheti labda isiyoonekana kama ya girlfriend wako.
   
 5. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kweli dunia ina mambo, xperience tamu lakini iko very brief, tuandikie in detail utaokoa wengi mshikaji
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hizo dawa zimeandikwa kuwa asitumie mama mja mzito. Kwamba zinatoa mimba au kuharibu sijui. Ila wanawake wengi hujaribu kutoa mimba kwa njia za hatari hatari sana kwa sababu hawana elimu ya uzazi. Matokeo yake huishia na madhara kibao hadi kifo kwa wengine. Kama mimba haitakiwi si aende kunakohusika ajieleze apewe ushauri nasaha?
   
 7. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu Bujibuji,kuwa makini sana na huyo rafiki yako,kama ulivyo sema yeye akufurahia icho kitendo cha yeye kupata ujauzito na akakushauri mkaitoe,naona hapo kuna kamchezo anachotaka kukuchezea,anaweza kutumia hiyo dawa alafu akuambie mimba imearibika kutokana na hiyo dawa.Ushauri: mwambie asitumie hiyo dawa kwani mimba yake bado ni changa,na anapaswa kutumia dawa kutokana na ushauri wa daktari tu na sio vinginevyo.

  Kama anahisi ana minyoo mpeleke hospitali mwenyewe akachekiwe.kitu kingine mkuu ebu jaribu kumchunguza kama yupo tayari kukuzalia mtoto maana usije kuta huyo msichana yupo na wewe tu kwa sababu zake binafsi na hana lengo lolote na wewe.
  Swala la kuzaa mkuu sio la kukurupuka tu na kuchukua maamuzi ya ghafla,kaa nae chini mzungu mzie jambo hilo kwa makini.
   
 8. M

  Msindima JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Pole kaka,chunguza kwa umakini kwa nini anataka mimba itolewe,yawezekana hauko peke yako na inawezekana kabisa hiyo mimba si yako thus why anataka ku-abort,jaribu kukaa nae na umweleze madhara ya kufanya abortion yako mengi tu.

  Nina wasiwasi kama anakupenda kwa dhati,au isije ikawa anakupima aone msimamo wako,maana wakati mwingine dada anaweze kuamua kukuchemsha. Hii story yako imenikumbusha issue kama hii ilitokea mwaka jana,jamaa ana gf wake akamwambia hivyo kuwa ana mimba,jamaa kafurahia,mara dada akamwambia nataka kuitoa,jamaa akabaki anashangaa kwa nini anataka kuitoa,akanifata kuniomba ushauri nikamwambia akae na gf wake aongee nae ampe strong reasons kwa nini anataka kutoa,jamaa kajitahidi kukaa na huyo dada waongee kwani mdada anaelewa,ikabidi jamaa amtafute rafiki yake wa karibu na gf wake aongee nae,alipoongea na rafiki yake akamweleza kuwa wala hana mimba shida yake ilikuwa ni pesa maana alikuwa chuoni kwa wakati huo,jamaa alichoka. Kwa hiyo kaka hebu jaribu hata kumtafuta rafiki yake wa karibu inawezekana amemgusia hiyo issue.
   
 9. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ninavyofahamu mimi,mama mjamzito hatakiwi kutumia sawa za minyoo.In the recent days nikamsikia daktari mmoja akaniambia anazuiliwa kutumia dawa hizo katika miezi mitatu ya kwanza ya ujazito wake baada ya hapo anaruhusiwa kutumia.Sina hakika kama zinatoa ujauzito,lakini nina hakika zina teratogenic effect(naomba mwenye kufahamu kwa kiswahili alezee).Alisema mama wajawazito wenye HIV wanapewa dawa za minyoo,its a policy,Lakini ni baada ya hiyo miezi mitatu
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyo demu hajakumind wala nini.Demu aliyekumind hawezi kusema anataka kutoa.Ninavyojua mimi wanaume ndio wanakuwa hawahesabu mtoto mpaka azaliwe na ngoma yao inakuwa ngumu kwa sababu mara nyingi wanawake wanataka watoto, sasa hapa tunaona reversal of roles.Kibongobongo abortion is murder, na kwa mwanamke ambaye ana a biological connection na mtoto ku advocate hili zaidi ya mwanaume inaonyesha yuko heartless na hana mapenzi na wewe.

  kuna kina mama wamezaa shule au katika stage muhimu sana za careers zao kwa hiyo hamna excuse hapa, unless kama kuna medical reasons ambazo hujazitoa.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  Jamani asanrteni sana kwa ushauri na maoni yenu mbalimbali.
  Mmenifungua akili yangu finyu na nimetua lile zigo la mawazo nililokuwa nalo.
  Nasema asanteni sana.
  Kweli hiki ni kisima cha maarifa.
   
 12. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #12
  Jul 2, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ukisoma maelezo ya hiyo dawa (zentel) imeandikwa kabisa kuwa wajawazito wenye mimba changa wasitumie hiyo dawa ,na utafiti wao walioufanya kwa kumjaribu panya mwenye mimba unaonyesha panya huyo alipata matatizo yalio pelekea mimba kuharibika.
   
Loading...