Je dawa za kupunguza unene zinaweza kusababisha matatizo ya uzazi?

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
26,563
48,680
Nimefanya jitihada za kujipunguza uzito ila naona nimeshindwa nazidi tu kuongezeka siku baada ya siku. Wenzangu wakiongeza mahela mimi naona naongeza kilo.

Mazoezi nafanya kidogo naacha naona uvivu. Chakula naacha najikuta nimerudia tena tuseme ukweli jamani hakuna asiependa vitu vitamu, nitakula malimao mpaka lini? Ni adhabu kuishi kwa diet acheni tu.

Natamani kutumia madawa ya kupunguza uzito ila naogopa yasije yakaniathiri mfumo wangu wa uzazi.

Naombeni ushauri haya madawa ya kupunguza mwili yana shida yoyote kwenye uzazi?

Asanteni
 
Kabla ya kukimbilia kujinyima vyakula ili kupunguza uzito, inabidi uamue ni uzito gani unaouhitaji. Wataalamu hawashauri kushusha uzito ghafla kwa zaidi ya kilo 22 ndani ya wiki.

NJIA ZA ASILI ZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO:
1. Tambua Mahitaji ya Karoli(Nguvu)
Kabla hujaamua jinsi ya kula, unapaswa kufahamu ni Kalori(Nguvu) kiasi gani unahitaji kwa siku. Hii inaweza kupatikana kwa kikokotozi maalumu cha Kalori (Nguvu) kinachotumia kimo, uzito, umri na shughuli za mhusika.

2. Jifunze Kutumia Matunda na Mboga za Majani
Unahitaji walau vipande vitano vya matunda na mboga za majani. Kufanya hivi kutaweka mwili wako vizuri kwa kuwa matunda na mboga za majani vina nyuzi muhimu(valuable fibres) na vitamini muhimu. Pia vinajaza tumbo lako na hufanya usihitaji kula vyakula vya Kalori(Nguvu) sana.

3. Angalia Kiwango cha Chakula unachotumia
Jizuie kula vyakula vyenye Kalori(Nguvu) sana mfano maharage ya soya, mafuta ya samaki, soseji, karanga n.k na ukilazimika kula kwa kiwango kidogo sana. Dondoo ya muhimu ni kutafuna chakula chako taratibu na kwa muda unaofaa ili kurahisisha umeng'enyaji wa chakula na hii itakusaidia kula kidogo.

4. Usiruke Mlo!
Wengi wanaotaka kushusha uzito huona kujinyima milo mfano kuacha kula mchana au asubuhi au usiku ndio njia sahihi wakati sio sahihi, kula chakula kidogo kutafanya mwili uwe na afya. Unaweza hata kugawa ile milo mitatu mikubwa katika vijisehemu vitano au sita vya muda mfupi.

5. Matunda na Mboga Safi ya Asili ndio sahihi zaidi
Vyakula vilivyosindikwa viwandani vina sodiamu na mafuta kwa wingi. Unatarajiwa sana kushusha uzito ukitumia vyakula asili.

6. Usidhibiti sana Matumizi ya Vyakula
Unaweza kuendelea kula vyakula unavyopenda kama vipande vya keki lakini hakikisha unatumia kwa tahadhari kubwa vitu hivyo vyenye sukari ili visiwe vipingamizi vya kushusha uzito wako.

7. Usiamini kila kitu Kilichoandikwa kwenye Lebo za Vyakula
Lebo zinazosema haina mafuta haimaanishi kuwa kuna kiwango kidogo cha Kalori(Nguvu). Ni sawa na zile lebo zinazosema kiwango kidogo cha sukari(low sugar).

8. Dhibiti kiwango cha Vinywaji vya Sukari unavyokunywa
Unywaji wa soda na juisi za viwandani huongeza utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kufanya uzito kuongezeka. Jitahidi kunywa glasi 8 za maji safi na salama ambayo yatasaidia kutoa sumu na uchafu
mwilini.

9. Ainisha vyakula utakavyokula
Kuandika mpangilio wa vyakula utakavyokula kutakulinda na kuhakikisha vyakula vya kutia nguvu unavyokula ni sahihi na pia ni kikumbusho cha kila wakati juu ya ni vyakula gani unahitaji.

10. Kumbuka kufanya mazoezi siku hadi siku
Dakika 30-60 za mazoezi kila siku zitalinda afya yako na kukusaidia kupunguza uzito. Mazoezi ya kunyanyua vitu vyenye uzito ni mazuri zaidi kwa kuwa huchoma Kalori iliyopo mwilini.
 
nimefata ushauri huu sana mkuu nina mwaka sinywi sukari,soda , juice za viwandani.nakula mboga kama mbuzi lakini wapi? nimechoka jibu tu swali langu
 
basi nenepa tu hakuna namna,kikubwa kama shemeji karidhia haina shaka,ila mazoezi usiache no matter how fat u get!
 
Gegedana mwezi mzima kila siku, kutwa mara tatu kwa mwezi, lazima you'll burn calories
 
Mkuu, Jaribu bidhaa za EDMARK. Ni 100% guaranteed. Usipopungua utarudishiwa fedha zako.

Hakika utaja kunishukuru humu. Utapungua ndani ya Wiki mbili.
 
Hebu lete menu yako Kwa Siku Kwa wastani unakula nini na Kwa namna gani,? Maana wengine hali asubuhi wala mchana Ila usiku anakula with overtime , yani usiku anakula Chakula kingi kulipiza cha asubuhi na mchana! Halafu kafanye vipimo vya homoni na Kama kuna Dawa unatumia muda mrefu zitafakali! Epuka kulala lala penda kufanya shughuli za hapa na pale, panda ngazi acha lifti na Magari !
 
nakula jioni tu ila msosi wa hataree.situmii dawa yoyote mkuu.kutembea siwezi jua kali
 
Back
Top Bottom