Je dalili za uchungu kuanza, zinaweza kuanza wiki moja kabla ya siku ya makadilio!?

GIPAMA

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,103
541
Wakuu habari, mfano mwanamke akawa majamzito, wakaweka makadilio kuwa atajifungua tarehe fulan, mfano tarehe 20.04.2019, Je dalili za uchungu kuanza, zinaweza kuanza wiki moja kabla ya siku ya makadilio!? Je dalili hizo zinaweza kudumu mpaka ikafika tarehe aliyokadiliwa ndio akajifungua!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana huwa yanaitwa makadirio kwa maana hakuna uhakika mimba ilitungwa tarehe ngapi na mama atajifungua tarehe ngapi.

Muhimu kama mama akianza kuona dalili za maumivu makali yanayokuja na kupotea, au kupasuka kwa chupa ya uzazi (kutokwa na maji mengi ukeni) au damu na majimaji awahi haraka hospitali au kituo cha afya.

Kumbuka niliposema makadirio... dalili hizi huenda akaziona kabla au hata baada ya tarehe ya makadirio.
Hakikisheni mama anakuwa na watu karibu kuelekea siku za mwisho kujifungua, bila kusahau usafiri wa uhakika.
Vinginevyo... kila la kheri.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hiyo tarehe uliyoambiwa ni tarehe ya makadilio ya mwanamke kujifungua. Sio lazima iwe exactly tarehe hiyo. Inawezakuwa wiki mbili kabla ya iyo tarehe au wiki mbili mbele baada ya hiyo tarehe. Cha kuzingatia ni hiki. Endapo ukiona dalili za mama kutokwa na damu au maji maji au uchafu wa rangi yoyote au tumbo linauma na maumivu hayaachi basi fika kituo cha afya kilichopo karibu nawe kwa msaada wa kitabibu au kidactari.
ASANTE........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habari, mfano mwanamke akawa majamzito, wakaweka makadilio kuwa atajifungua tarehe fulan, mfano tarehe 20.04.2019, Je dalili za uchungu kuanza, zinaweza kuanza wiki moja kabla ya siku ya makadilio!? Je dalili hizo zinaweza kudumu mpaka ikafika tarehe aliyokadiliwa ndio akajifungua!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Dalili za uchungu huwa hazitabiriki na zinaweza kutokea siku hiyo hiyo na akajifungua, sio lazima zianze wiki moja kabla. Unaweza ukaamka mzima kbs na ukafanya kazi zako vzr tu na ukashangaa ht mida ya mchana hali inabadilika, uchungu unaanza.

😊 umenikumbusha,hali hiyo ilinitokea mimi.
Niliamka na kufanya kazi zangu kama kawaida,jioni nikaenda kufanya mazoezi kama ilivyo ada,na usiku nikaanda chakula cha familia,lakini ghafla saa mbili usiku uchungu ukaanza
 
Je huwa inawezekana zikaanza mapema pia!?

Sent using Jamii Forums mobile app
samahani,naomba nijaribu kukujibu ingawa hukuni-qoute mimi.
Kwa uelewa wangu,huwa kuna false labor na true labor

False labor huwa inatokea mapema zaidi,yaani hata mwezi mmoja kbl ya tar ya makadirio na hapo mama hupata maumivu ya tumbo(kama uchungu) ambayo hudumu kwa muda usiozidi dk 5 then yanatulia,Maumivu hayo hujirudia tena baada ya dk 20-45 badae.

True labor ndio ule uchungu wenyewe sasa,maumivu juu ya maumivu.
 
Asante, nimekupata vizuri, Hvo anaweza kuanza mapema alafu baadae hali ikatulia baada ya hizo siku 5

ni dk 5 mkuu ,sio siku 5.

Ndio, mama anapata maumivu ya muda mfupi then yanapoa,anakaa kwa muda dk nyingi kdg halafu maumivu yanajirudia tena.

Nakumbuka mm nilipitia hiyo hali kiasi cha kwenda hosptl nikihisi ndio uchungu wenyewe,nilipewa bed rest na na doctr akanambia hizo ni false labor,napaswa kufanya mazoezi zaidi.

Nilijifungua baada ya mwezi mmoja tangu niliporuhusiwa hospt
 
Asante kwa kueleza jambo ulilo na uzoefu nalo, Je dalili za uchungu ambao ni wa ukweli huwa ni zip, ambazo kwa 100% lazma ajifungue?

Japo anaweza asipate hiyo ya kwanza, uchungu ukaja ule ule wenyewe. Sema kuna wengine huwa wanahangaika ht siku mbili, tatu n.k.
Japo kwangu huwa inakuja moja kwa moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa kueleza jambo ulilo na uzoefu nalo, Je dalili za uchungu ambao ni wa ukweli huwa ni zip, ambazo kwa 100% lazma ajifungue?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu siku ikifika, yale maumivu yake km ni mkeo utajua tu hapa ngoma imetick.
Ila mi huwa najulia kwenye chai, nikiwa kwenye hali hiyo basi siku zikikaribia nikihisi tu maumvivu nakunywa chai. Nisiposikia maumivu makali najua hapa bado.
Ila nikinywa hlf nikasikia km wembe umepita basi najua soon kinajipa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom