Je CUF wako sahihi katika hili la Zanzibar

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,011
2,165
SWALI; kwanini CUF wanashiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani, Zanzibar wakati walisusia uchaguzi wa marejeo wa Machi, 2016.., Je, CUF wako sahihi kwenye hili..!?

JIBU;

>> Wabunge wale unawaona wa CUF katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walitokana na uchaguzi mkuu wa oktoba 25, 2015..,

>> Katika uchaguzi wa mwezi Machi, 2015 (wa marejeo) CUF hawakushiriki.., uchaguzi ambao CUF walisema kuwa ni batili.., (pia CUF hawana wabunge katika baraza la wawakilishi hafi sasa).., uchaguzi wa marejeo ulikuwa wa kutafuta 'wajumbe wa baraza la wawakilishi' siyo 'wabunge wa JMT'..,

>> CUF walisusia chaguzi zilizoko chini ya Mamlaka ya moja kwa moja ya ZEC [Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar], ambayo iko chini ya SALUM JECHA.., haswaa chaguzi za kuwatafuta wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar..,

>> ndiyo.., uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani (ambao utafanyika 22-01-2017) ni wa kuchagua mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na siyo mjumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar.., CUF walisusia chaguzi za ZEC (Jecha) na siyo NEC..,

Hivyo CUF wako sahihi katika hili.., hakuna sehemu wamekosea katika kauli zao za mwanzo..,

Ahsante ;

Martin Maranja Masese (MMM)
 
Kwa hiyo CUF wanaimani na NEC ila ZEC hawana imani nayo.!
Kwa kiasi fulani NEC walifanya hujuma za kujificha lakini ZEC ilikuwa hujuma ya moja kwa moja hivyo CUF hawana sababu za msingi hata kama hawana imani na NEC kususa!
 
Sasa kama ni ZEC ndio hawana imani nayo iweje walikuwa wanamlaumu mamlaka ya JMT pamoja na NEC huku wakijua wazi kuwa JMT haina mamlaka juu ya ZEC na wala Rais wa JMT hana mamlaka juu ya ZEC? Wamekwenda hadi mataifa ya nje wakishusha shutuma kwa serikali ya JMT.
 
Waliilaumu mamlaka kwa kuwa baada tu ya kuingia madarakani iliahidi ingepatia uvumbuzi suala la Jecha kujecha uchaguzi, lakini badala yake ikadai kuwa itapeleka majeshi na atakayeleta vyovyoko itamshughulikia!
 
SWALI; kwanini CUF wanashiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani, Zanzibar wakati walisusia uchaguzi wa marejeo wa Machi, 2016.., Je, CUF wako sahihi kwenye hili..!?

JIBU;

>> Wabunge wale unawaona wa CUF katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walitokana na uchaguzi mkuu wa oktoba 25, 2015..,

>> Katika uchaguzi wa mwezi Machi, 2015 (wa marejeo) CUF hawakushiriki.., uchaguzi ambao CUF walisema kuwa ni batili.., (pia CUF hawana wabunge katika baraza la wawakilishi hafi sasa).., uchaguzi wa marejeo ulikuwa wa kutafuta 'wajumbe wa baraza la wawakilishi' siyo 'wabunge wa JMT'..,

>> CUF walisusia chaguzi zilizoko chini ya Mamlaka ya moja kwa moja ya ZEC [Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar], ambayo iko chini ya SALUM JECHA.., haswaa chaguzi za kuwatafuta wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar..,

>> ndiyo.., uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani (ambao utafanyika 22-01-2017) ni wa kuchagua mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na siyo mjumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar.., CUF walisusia chaguzi za ZEC (Jecha) na siyo NEC..,

Hivyo CUF wako sahihi katika hili.., hakuna sehemu wamekosea katika kauli zao za mwanzo..,

Ahsante ;

Martin Maranja Masese (MMM)
Huu ndiyo utaalamu bandia. Zanzibar nu sehemu ya Muungano inajitegemea kwa baadhi ya mambo yake kama Wawakilishi na ZEC. CUF waasisi wake na vipngozi wake na nyumbani kwao ni chama cha Zanzibar wanapigania maslahi ya Zanzibar. Seif anajitangaza ni rais wa Zanzibar kipenzi cha Wazanzibar. Sera yake rasmi ni kuvunja muungano ili tuwe na wa Mkataba. Ni ajabu leo aende uchaguzi wa Muungano.
 
Back
Top Bottom