Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Uchaguzi wa Marudio wa Ubunge Jimbo la Dimani utafanyika Januari 22, 2017. Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Hafidh Ally Tahir.
Mtakumbuka kuwa CHADEMA na UKAWA walisusia uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 2016. Swali ambalo Lizaboni na wadau wengine wanajiuliza, Je CUF na UKAWA watashiriki uchaguzi huo ambao kampeni zake zitaanza Desemba 23 au wataendelea kususia? Kama CUF watashiriki, ni chombo gani cha Maamuzi kitakachopitisha jina la Mgombea? Mtakumbuka kuwa kwa sasa kuna CUF Lipumba na CUF Maalim Seif ambapo kwa huku Bara majukumu yake yanatekelezwa na Julius Mtatiro.
Ikiwa wataamua kushiriki uchaguzi huo, Je hawaoni kuwa huko ni kula matapishi yao? Na je hawaoni kuwa kitendo hicho ni kwenda kinyume na msimamo wao waliouonesha Machi 2016?
Na kama wataendelea kususia, hawaoni kuwa ni kukizika chama chao Zanzibar na kwamba watapoteza fursa ya kuikosoa Serikali hasa baada ya kuzuiliwa kwa mikutano ya hadhara?