Je, Corona ni nyenzo ya mchujo wa ‘evolution’? (Natural selection & elimination)

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,011
40,681
Waamini wa nadharia ya ‘evolution’ hupenda sana kutumia mfano wa twiga waliokuwa na shingo fupi ambao walikifa njaa kwa kushindwa kufikia majani laini ya juu ya miti na wale wenye shingo ndefu kushika hatamu. Vivyo hivyo tunaona leo jinsi tembo wenye pembe fupi wanavyoanza kushika hatamu kidogo kidogo kwa kuwa huwa hawauwawi kwa kasi na majangili kama wale wenye mdovu kubwa, hii ndio evolution by ‘natural/artificial selection/elimination’.

Naanza kupata picha kwamba Corona inafanya mchujo na kusababisha evolution isonge mbele zaidi, baada ya Corona, binadamu watakaobakia watakua ni wale wenye uimara sana, na hivi ndivyo vinasaba vya binadamu vilivyoweza kisonga mbele, amini usiamini,hapo awali bila shaka watu walikufa hata kwa mafua ya kawaida tu, ila baada ya dhahama ya vifo kuisha basi wakabaki binadamu imara ambao mafua kwao hawauchukulii kama ugonjwa tena bali ni usumbufu wa kawaida tu.
Baada ya Corona, nchi ambazo watu wake wako lockdown bado watakuwa hawajakamilisha mchujo, kwani kuna vinasaba dhaifu ambavyo vilikuwa vimefichwa majumbani ambavyo vilipaswa kuchujwa, hivyo bado vitachujwa lockdown ikiisha, kwa wasio na lockdown kwao mchujo utakuwa umekamilika na vimebaki vyuma vya pua tu, na ndio maana waChina wanaogopa waAfrika maana wanaweza wakakaa na magonjwa bila kuonuesha dalili huku wakiambukiza.
JPM is a scientist na anajua kwamba huu ugonjwa sio wa kuisha kesho au kesho kutwa, hivyo ni either uweke Lockdown miaka 10 au no Lockdown at all, let evolution run its course and we shall emerge as strong as anyone can be, sacrifises have to be made to attain that superior genome!
 
Back
Top Bottom