Je, chombo hiki kitaweza kuhakikisha watumiaji wa simu za mkono Wa Tanzania... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, chombo hiki kitaweza kuhakikisha watumiaji wa simu za mkono Wa Tanzania...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 30, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  ...wanapunguziwa gharama kubwa mno za simu hizo ukilinganisha na nchi za magharibi?


  Date::11/29/2008
  Watumia simu za mikononi wapata wa kuwatetea kimaslahi
  Exuper Kachenje
  Mwananchi

  HAKI za watumiaji wa simu za mkononi pamoja na wengine wa huduma za mawasiliano nchini, sasa watafaidika kwa sababu zitalindwa na kutetewa kwa mujibu wa sheria za nchi.

  Utetezi na ulinzi wa haki hizo utafanyika kupitia Baraza la Ushauri kwa Watumiaji Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC) lililoundwa chini ya Kifungu cha 37 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano namba 12 ya mwaka 2003.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Joseph Kessy, alisema kuwa "Baraza hilo limeundwa kwa madhumuni ya kulinda na kutetea maslahi na haki za mtumiaji wa huduma za mawasiliano."

  Alisema kuwa baraza hilo lenye wajumbe saba ambao huteuliwa na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ni kiungo muhimu kati ya wadau wa sekta ya mawasiliano na linafanya kazi ya macho na masikio ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano.

  Alifafanua kuwa baraza hilo lina jukumu la kufanya mashauriano na wadau mbalimbali katika sekta hiyo ikiwemo serikali, mamlaka, watoa huduma na makundi mengine na kwamba limeundwa katika kanda saba kulingana na jiografia ya nchi huku kila kanda ikiwakilisha kwenye baraza.

  Alisema kuwa dira ya baraza hilo ambalo tayari linafanya kazi mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara ni kutetea kwa nguvu maslahi ya watumiaji, kuhamasisha na kuelimisha watumiaji juu ya haki na wajibu wao.

  Kessy alibainisha kuwa tayari upo utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kwa watumiaji wa huduma ya mawasiliano ambapo wanatakiwa kupeleka malalamiko kwa maandishi kwa mtoa huduma na iwapo hakuridhika atayawasilisha TCRA-CCC

  Alisema kuwa baraza hilo lipo tayari kuwasaidia watumiaji huduma za mawasiliano watakaoathirika, na kwamba wana haki ya kulipwa fidia, kupata taarifa sahihi pamoja na faragha huku wakiwajibika kulinda miundombinu, kutunza mazingira na kutoa taarifa.

  Kessy aliongeza kuwa baraza hilo tayari limeunda kamati kusimamia maeneo muhimu aliyoyaainisha kuwa ni elimu kwa watumiaji na malalamiko, mahusiano na wadau pamoja na utawala, kuandaa utaratibu wa kukutana na wadau pamoja na kusimamia rasilimal za wadau.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sijafahamu kazi ya baraza hilo ,aliyefahamu tafadhali hebu atuelimishe maana mambo ya simu za mkononi yamejaa duniani na sijasikia kuundiwa baraza. Ila nikiongezea kama wangeweza kumkamata mtu anaepigia watu simu za vitisho hapo ningekubaliana nao kimikakati ila bado naulizia kazi yao !
  Yaani mtu ananunua simu na kadi yake halafu anaishi sehemu hata hakuna mnara wa simu ,anarudi analalamika ndio tuseme watamsikiliza ?
   
Loading...