Je, chombo cha Habari cha Umma cha TBC kinapewa maelekezo na watawala wetu wa CCM ya nini cha kutangaza na kipi si cha kutangaza?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Tupo katika kipindi muhimu sana cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, mwishoni mwa mwaka huu.

Ni matarajio ya Watanzania wote kuwa vyombo vyetu vya habari vya Umma vitatekeleza wajibu wao kwa usawa bila kupendelea chama chochote cha siasa.

Tumeshuhudia chombo cha habari cha television ya Taifa cha TBC, kikirusha mubashara mkutano mkuu wa chama cha CCM, uliofanyika jijini Dodoma siku chache zilizopita.

Tumeshuhudia chombo hiko cha Umma cha TBC "kikiwagomea" chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, kurusha matangazo mubashara walipofanya mkutano wao mkuu, mwanzoni mwa wiki, pale katika ukumbi wa Mlimani city.

Tumeshudia pia chombo hicho cha Umma cha televisheni ya Taifa ya TBC "kikigoma" kwa mara nyingine tena kurusha mubashara mkutano mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, uliofanyika pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee hapo jana.

Hata hivyo nimeshangaa sana kuona chombo hicho cha Umma cha televisheni ya Taifa kikirusha LIVE mkutano mkuu wa chama "kidogo" cha NCCR, ambao unafanyika katika ukumbi wa Diamond hivi leo.

Ndipo hapo nilipojiuliza hivi hii TBC inatumia vigezo gani vya kuchagua chama kipi kiwape LIVE coverage na chama kipi cha siasa kisiwape hiyo nafasi?

Tujikumbushe pia kuwa hiyo TBC inaendeshwa kwa kodi za watanzania wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kwa maana chimbo hicho kinahudumiwa na walipa kodi wote wa nchi hii, yaani wanachadema,.wanaccm na wa vyama vingine vya siasa bila kujali itikadi zetu za kisiasa.

Kwa hiyo kitendo kinachofanywa na TBC cha "kupendelea" vyama fulani fulani kwa "maagizo" ya watawala wetu wa CCM ni makosa makubwa sana na kitasababisha mpasuko mkubwa sana kwa Taifa hili.
 
Watawala wetu "wameiagiza" TBC itangaze LIVE mikutano mikuu ya CCM na "CCM-B" NCCR Mageuzi na wakawaelekeza wasitangaze mikutano mikuu ya vyama makini vya siasa vya Chadema na ACT Wazalendo
 
Halafu kuna mtu atasema NCCR ni cha pinzani,upuuzi mtupu! Mbatia hajifunzi kwa Lipumba aliyetumiwa kama condom na CCM kisha kutupwa baada ya matumizi!
 
Labda wapo kibiashara zaidi...

Inawezekana Ccm walilipia matangazo yao na Nccr pia wamefanya hivyo...Inawezeka Cdm na Act wao hawakulipia
 
Your observation is very interesting such a way that research can be done on the this... .
TBC kwa maana ya jina ni SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TAIFA. naomba usiwafananishe na mashirka kama BBC ama DW, TBC ni jina tu si shirika huru ni shirika linaloendeshwa kwa matakwa ya CCM. Na kwa matiki hiyo kamwa haliwezi kujiendesha kibiashara kwani linawateja wachache japo ni kituo kikongwe. Fanya tafiti wangapi wanatazama matangazo TBC, na kwanini wengi eanakisusa. Tatizo hawawezi kujibalasi kwani wanalazimika. Kama unabisha kamuulize TIDO MUHANDO.
 
Back
Top Bottom