Je China inazibebesha nchi masikini madeni yasiyo himilivu??

lwambof07

JF-Expert Member
Jul 12, 2016
4,593
5,203
Utoaji mikopo wa China kwa miradi ya ujenzi kote ulimwenguni umeonekana kuwa na utata

China imekuwa ikikosolewa kutokana na tabia yake ya kutoa mikopo kwa nchi maskini, ikishutumiwa kuziacha zikitatizika kulipa madeni na hivyo kukabiliwa na shinikizo kutoka kwa Beijing.

Lakini hilo linapingwa na China, ambayo inashutumu baadhi ya nchi za Magharibi kwa kuendeleza madai hayo ili kuchafua sifa yake.

Inasema: "Hakuna nchi hata moja ambayo imeanguka katika [a] kinachojulikana kama 'mtego wa madeni' kutokana na kukopa kutoka China."

Je tunajua nini kuhusu mikopo ya China?
China ni mojawapo ya mataifa makubwa zaidi duniani yanayokopesha mataifa mengi.

Mikopo yake kwa mataifa ya uchumi mdogo na uchimi wa kati imeongezeka kwa zaidi ya mara tatu ndani ya muongo mmoja uliopita na kufikia jumla ya dola bilioni 170 (£125bn) kufikia mwisho wa mwaka 2020

Hata hivyo, ahadi za jumla za mikopo za China zinaweza kuwa kubwa zaidi kuliko takwimu hizi zinavyopendekeza.

Utafiti wa shirika la maendeleo la kimataifa katika Chuo Kikuu cha William & Mary nchini Marekani, AidData, unaona kuwa nusu ya mikopo ya China kwa nchi zinazoendelea haijaripotiwa katika takwimu rasmi za madeni.

Mara nyingi huwekwa nje ya mehesabu ya serikali, huelekezwa moja kwa moja kwnye makampuni na benki zinazomilikiwa na serikali, mashirika yenye ubia au taasisi za binafsi, badala ya moja kwa moja kutoka kwa serikali hadi serikali.

Hivi sasa kuna zaidi ya nchi 40 za kipato cha chini na cha kati, kulingana na AidData, ambapo deni lao kwa wakopeshaji wa China ni zaidi ya 10% ya ukubwa wa pato lao la kila mwaka la uchumi (GDP) kutokana na "deni hili lililofichwa".

Nchi za Djibouti, Laos, Zambia na Kyrgyzstan zina deni kwa Uchina sawa na angalau 20% ya Pato lao la kila mwaka.

Mengi ya madeni yanayodaiwa China yanahusiana na miradi mikubwa ya miundombinu kama vile barabara, reli na bandari, na pia sekta ya madini na nishati, chini ya Mpango wa maendeleo ya miundombinu wa Rais Xi Jinping.

'Mitego ya madeni' ni nini na kuna ushahidi gani kwao?
Katika mahojiano na BBC, Richard Moore, mkuu wa shirika la kijasusi la kigeni la Uingereza MI6, alisema China inatumia kile alichokiita "mitego ya madeni" kupata faida juu ya nchi zingine.

Madai ni kwamba China inazikopesha fedha nchi nyingine, ambazo baadae hulazimika kuacha udhibiti wa mali muhimu ikiwa haziwezi kukidhi ulipaji wa deni lao tuhuma ambazo zimekanushwa kwa muda mrefu na Beijing.

Mfano mmoja unaotajwa mara nyingi na wakosoaji wa Uchina ni Sri Lanka, ambayo miaka iliyopita ilianza mradi mkubwa wa bandari huko Hambantota chini ya uwekezaji wa China.

Lakini mradi huo wa dola bilioni uliotumia mikopo na wakandarasi kutoka Uchina uliingia katika utata na ulipambana kuthibitisha kuwa unaweza kutekelezwa na kuiacha Sri Lanka ikiwa na deni kubwa.

Hatimaye, mwaka wa 2017, Sri Lanka ilikubali kuwapa Wafanyabiashara wa China walio chini ya serikali, umiliki wa kudhibiti 70% ya hisa katika bandari kwa kukodisha kwa miaka 99 ili kupata uwekezaji zaidi wa China.

Watu wa Sri Lanka waandamana dhidi ya hisa iliyopendekezwa ya kampuni ya Kichina katika bandari ya Hambantota (2017)

Uchambuzi wa mradi wa bandari hiyo uliofanywa na shirika la wataalam la Chatham House lenye makao yake nchini Uingereza umehoji kama simulizi ya "mtego wa madeni" inatumika kikamilifu, ikizingatiwa kwamba mpango huo uliendeshwa na msukumo wa kisiasa wa ndani, na kwamba China haikuwahi kumiliki rasmi bandari hiyo.

Inasema kwamba sehemu kubwa ya deni la jumla la Sri Lanka lilikuwa linadaiwa na wakopeshaji wasio Wachina na kwamba hakuna ushahidi kwamba China imetumia fursa ya nafasi yake kupata mkakati wa kijeshi kutoka katika bandari.

Licha ya hayo, kuna shaka kidogo ushiriki wa China kiuchumi nchini Sri Lanka umeongezeka katika muongo mmoja uliopita na wasiwasi unaendelea kuwa hii inaweza kutumika kuendeleza matarajio yake ya kisiasa katika eneo hilo.

Kuna sehemu zingine za ulimwengu ambapo ukopeshaji wa Wachina pia umeonekana kuwa na utata na kandarasi ambazo masharti yake yanaweza kuipa China nguvu juu ya mali muhimu.

Lakini hakuna kesi, kati ya mamia ya mipango ya mkopo iliyochunguzwa na AidData na watafiti wengine ya wakopeshaji wanaomilikiwa na serikali ya China kunyakua mali kuu katika tukio la kutolipa mkopo.

Je, mikopo ya China inalinganishwaje na mingine?
Uchina haichapishi rekodi za mikopo yake ya nje na mikataba yake mingi ina vifungu vya vilivyofumbwa ambavyo vinazuia wakopaji kufichua yaliyomo.

Inasema kuwa usiri kama huo ni kawaida kwa kandarasi za mkopo za kimataifa.

"Makubaliano ya usiri ni ya kawaida sana katika mikopo ya kibiashara ya kimataifa", anasema Profesa Lee Jones wa Chuo Kikuu cha Malkia Mary cha London.

"Na sehemu kubwa ya ufadhili wa maendeleo ya China kimsingi ni operesheni ya kibiashara." aliongeza

Mataifa mengi makubwa yaliyoendelea kiviwanda hutoa maelezo kuhusu shughuli zao za ukopeshaji kupitia uanachama wa kile kinachojulikana kama Klabu ya Paris (Paris Club)..

Ila China imechagua kutojiunga na kikundi hiki, ingawa kwa kutumia data inayopatikana ya Benki ya Dunia, ripoti ya ukuaji wa haraka katika utoaji wa mikopo ya Uchina ikilinganishwa na zingine unaweza umewekwa wazi.

Je, mikopo ya Wachina ni migumu kurejesha?
China ina mwelekeo wa kukopesha kwa viwango vya juu vya riba kuliko serikali za magharibi.

Takriban 4%, mikopo hii iko karibu na viwango vya soko la kibiashara na takriban mara nne ya mkopo wa kawaida kutoka Benki ya Dunia au nchi binafsi kama vile Ufaransa au Ujerumani.

Muda unaohitajika wa kurejesha mkopo wa China pia kwa ujumla ni mfupi ambapo ni chini ya miaka 10, ikilinganishwa na karibu miaka 28 kwa mikopo ya masharti nafuu ya wakopeshaji wengine kwa nchi zinazoendelea

Viwango vya riba kwa mikopo ya China ni vya juu kuliko vile vya wakopeshaji wengine

Wakopeshaji wanaomilikiwa na serikali ya China pia kwa kawaida huhitaji wakopaji kudumisha salio la chini kabisa la pesa katika akaunti ya nje ya nchi ambayo wakopeshaji wanaweza kufikia.

"Kama mkopaji atashindwa kulipa deni lake," anasema Brad Parks, Mkurugenzi Mtendaji wa AidData, "China inaweza kutoa pesa kutoka kwa akaunti [hii] bila kulazimika kukusanya deni kupitia mchakato wa mahakama."

Mbinu hii haionekani sana katika mikopo inayotolewa na wakopeshaji wa nchi za magharibi.

Hivi sasa kuna mpango wa mataifa ya G20 - nchi zenye uchumi mkubwa na unaokua kwa kasi kutoa msamaha wa madeni kwa nchi masikini ili kuzisaidia kukabiliana na athari za janga la corona.

Uchina imejiunga na hii na inasema kuwa imechangia "kiasi kikubwa zaidi cha ulipaji wa deni" kuliko nchi yoyote inayoshiriki katika mpango huo.

Benki ya Dunia inasema kwamba tangu Mei 2020, jumla ya zaidi ya dola bilioni 10.3 imewasilishwa katika msamaha wa deni na nchi za G20 chini ya mpango huu.

Lakini tulipouliza Benki ya Dunia kwa mchanganuo wa nchi, ilisema isingeweza kusema na kutoa taarifa hiyo.
IMG_20220106_170649.jpg
IMG_20220106_170708.jpg
IMG_20220106_170628.jpg
 
Back
Top Bottom