Je changamoto ya malaria jibu ni net tuu au tuangalie pia elimu, uchumi, makazi na utamaduni??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je changamoto ya malaria jibu ni net tuu au tuangalie pia elimu, uchumi, makazi na utamaduni???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salas, Jul 11, 2011.

 1. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Vijana wakiwa wameweka net za asante bush katika goli ikiwa ni muendelezo wa kukuza vipaji katika fani ya mpira.

  changamoto inayojitokeza hapo Je kulikuwa na uhitaji wa net hizi???????? Je jamii ilishirikishwa vipi hadi kufikia hatua ya tatizo la malaria ni ukosefu wa net???? Hatimaye mkuu wa kaya kupitisha bakuli la kuomba net???

  Je net tu ndio suluhisho la haya yote??? Je wizara husika kwa kupitia Muundo wake wa preventive care ambao mabwana afya wanaaajiriwa na kutumia kodi zetu wanazungumzaje hapa??

  Hakika kupanga ni kuchagua................. Malaria= Net, .....................Kilimo kwanza = Mbolea ???? umeona tatizo ni rutuba ya udongo au una sababisha soil cake........................... Mavuno= GMO SEEDS....sasa ngojea waziweke darini wazirudishe shambani kama zitaota....

  .............Elimu= Majengo ya madarasa...........................kazi kweli kweli

  simu 026.jpg
   
 2. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Nchi hii, kila uamuzi sio wa kuwasaidia wananchi bali matumbo ya watu.

  Jiulize maswali haya:
  Malaria na Vyandarua:
  1. WaTZ wangapi ni walengwa kwenye kampeni hii.
  2. Kati ya hao walengwa, wangapi wana vitanda vya kulalia (ambavyo vinaweza kufungwa net)
  3. Vitanda hivyo viwe na vipimo vya kutosheleza hizo nets
  4. Nyumba wanayoishi waweze kufunga net
  5. Idadi ya wanaolala humo waweze kutosha kwenye net 1 au mbili

  Kilimo kwanza:
  1. Kuna wagani wangapi vijijini
  2. Eneo la kulima ni kiasi gani
  3. Mazao gani yanatiliwa mkazo
  4. Masoko yapi yanalengwa
  5. Asilimia ngapi ya mabilioni ya Kilimo kwanza inakwenda kwa mkulima
  6. Mvua zipi za kuleta mavono (Asilimia ngapi ya pesa hizo zimeelekezwa kwenye umwagiliaji)

  Shule za kata, the same problems!!! Etc etc

  Je, Kweli kuna wataalamu (wasio vibaraka wa watawala) walioshirikishwa kuandaa mipango hii? Kama ni ndio ni wa aina gani wanaotia aibu usomi kwa jinsi hii? Ukikutana na watu kwenye makongamano ya kimataifa unaona aibu kujiita MTZ maswala kama haya yanapojitokeza.

  YETU MACHO...
   
Loading...