Je, CHADEMA wampe ulinzi Salum Mwalimu maana ushindi wake Kinondoni uko wazi?

Je inawezekana Mtanganyika kugombea ubunge visiwani?
Katiba inasemaje kuhusu hili, mwenye kujua afafanue japo kidogo.
Nendeni mahakamani mkaweke pingamizi maana kosa la kiufundi mmeshalifanya na wana CCM asilia aka wafia chama hawana nguvu tena kwa kitendo mlichowafanyia.
 
Chadema mnashangaza sana
Nini kimebadilika kimfumo katika tume ya uchaguzi?
Bado sio wateule wa ccm?
Bado wakurugenzi hawasimamii uchaguzi?
Suala ni sisi wananchi wa kinondoni tutamchagua salum,ila wao kwa mabavu wamuweke huyo msaliti
 
Awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu mwingine wa rehma.

CHADEMA msilifanyie mzaha jambo hili maana nina uhakika kwa jinsi watu walivyochukizwa na wasaliti wachache walivyotuingiza kwenye gharama za uchaguzi bila sababu yeyote, lazima zitapigwa kura za hasira kiasi kwamba hata msaliti asipate kura za hata moja. Hakuna mwananchi atakayekua tayari kwenda kusimama kupigia kura kwa mtu aliyewasaliti kwa sababu ya hovyo halafu kisha akaitaka tena nafasi hiyo. Huyu mtu ni msaliti na haaminiki tena.

Kwahiyo kuna kila sababu ya CHADEMA kufanya kila namna kua kiongozi huyu Salum Mwalimu anapatia security ya kutosha kabla na wakati wa kuingia uchaguzi, wanaweza kujitokeza maadui wengi watakaotaka kutumia hila za kila namna ili kuhakikisha kua anakosa ushindi huo ulio dhahiri.Hawa watu wana mbinu nyingi sana sio la kubeza hili.

Ifahamike bayana kua Maulidi Mtulia hauziki kabisa Kinondoni, sio kwa sasa hata 2015 yenyewe alishinda tu kwa vile ulikua ni mwavuli wa UKAWA na kuchokwa kwa CCM. Kwa kawaida hiyo 2015 UKAWA wangelala wala asingeshinda na huo ndio ukweli wenyewe. Salum Mwalimu ni mjengaji mzuri wa hoja na anauzika sana bila shaka hilo halina ubishi, apatiwe ulinzi wa kutosha kijana huyu kulingana mahali atakapogombea na aina ya watu atakaopambana nao.

Nafasi yake ya unabu katibu mkuu inatosha tu kumpatia ulinzi, ni wajibu wa chama Chake kufanya hivyo.
Tuombe maana watu hawaaminiki kwenye kupiga kura hasa watanzania miminsiwaamini. Ingelikuwa Kwnye ushindi ukikuwabwazi, they are self conscious compared ti Tanzanians. Kama watu na elimu zao wanaweza kununukiwa, naogopa
 
CHADEMA vigeugeu tunawajua nyie mlimtukana Lowasa ni fisadi kwa miaka 10...mkampa nafasi y kugombea urais ndani ya wiki moja 1.....
Kwani hao kina mtulia na yule wa siha kwenye kampeni za 2015 walikuwa wanawasifia? Mbona wamepewa kugombea bila hata kufuata taratibu kubalika?huo sio ukigeugeu au ukigeugeu ni wa cdm kwa lowasa tu? Mbona ameitwa arudi kwenye chama kama kweli ni fisadi?
 
Hussein Mwinyi ana makazi Mkuranga na Unguja. Baba yake ana makazi Mikocheni na Unguja. Ni sawa kwa mfano alivyo Mbowe ambaye ana makazi Kinondoni na Hai. Au alivyo Lowassa ana makazi Monduli na Kinondoni. Hivyo hawa wanaweza kugombea sehemu mojawapo ya makazi yao. Salum Maalimu makazi yake yako Unguja tu, huku Kinondoni hana makazi. Haitakuwa rahisi kuwawakilisha wakazi wa Kinondoni.
Kama unaweza kujitoa akili kiwango hiki una haja ya kujibiwa?
 
Wewe mtu wa bara kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar kwanza atakupa nani?

Huwezi kugombea huwezi kupiga kura kama huna.

Na ili ukipate lazima uwe Mzanzibar by birth.
Hayo yanafanyika ili ccm iendelee kuwa madarakani huko unguja ama hujui
 
Yaani mpiga kura wa Kinondoni sehemu inayojulikana asilimia kubwa ya wakazi wake ni waelewa, atoke nyumbani kwenda kumpigia kura Mtulia, mtu anaye wafanya watu wazima watoto...nitaamini maneno ya Trump na nitafuta kwenye msamiati wangu kwamba Tanzania kuna wakazi wa mjini na vijijini.
 
Back
Top Bottom