Je, CHADEMA wampe ulinzi Salum Mwalimu maana ushindi wake Kinondoni uko wazi?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu mwingine wa rehma.

CHADEMA msilifanyie mzaha jambo hili maana nina uhakika kwa jinsi watu walivyochukizwa na wasaliti wachache walivyotuingiza kwenye gharama za uchaguzi bila sababu yeyote, lazima zitapigwa kura za hasira kiasi kwamba hata msaliti asipate kura za hata moja. Hakuna mwananchi atakayekua tayari kwenda kusimama kupigia kura kwa mtu aliyewasaliti kwa sababu ya hovyo halafu kisha akaitaka tena nafasi hiyo. Huyu mtu ni msaliti na haaminiki tena.

Kwahiyo kuna kila sababu ya CHADEMA kufanya kila namna kua kiongozi huyu Salum Mwalimu anapatia security ya kutosha kabla na wakati wa kuingia uchaguzi, wanaweza kujitokeza maadui wengi watakaotaka kutumia hila za kila namna ili kuhakikisha kua anakosa ushindi huo ulio dhahiri.Hawa watu wana mbinu nyingi sana sio la kubeza hili.

Ifahamike bayana kua Maulidi Mtulia hauziki kabisa Kinondoni, sio kwa sasa hata 2015 yenyewe alishinda tu kwa vile ulikua ni mwavuli wa UKAWA na kuchokwa kwa CCM. Kwa kawaida hiyo 2015 UKAWA wangelala wala asingeshinda na huo ndio ukweli wenyewe. Salum Mwalimu ni mjengaji mzuri wa hoja na anauzika sana bila shaka hilo halina ubishi, apatiwe ulinzi wa kutosha kijana huyu kulingana mahali atakapogombea na aina ya watu atakaopambana nao.

Nafasi yake ya unabu katibu mkuu inatosha tu kumpatia ulinzi, ni wajibu wa chama Chake kufanya hivyo.
 
Wazo lako ni mujarabu kabisa. Hakuna MTU Wa kumpatia kura msaliti. Yaani watu 2015 walihatarisha maisha yao kumchagua na kulinda kura lakini yeye ameona azime matumaini yao na bado bila aibu anataka tena achaguliwe...Hell Noooo....alichohongwa na ccm kinamtosha.​
 
Halafu walioteuliwa kugombea nafasi hizo hawatoki/ si wakazi wa maeneo hayo wanayogombea kuyawakilisha bungeni. Kamati kuu imeyakata majina ya walioteuliwa na majimbo husika kugombea nafasi hizo na badala yake kuwapa wajumbe wa kamati hiyo hususani huyo Salum Mwalimu. Hata kama sheria haiwazuii lakini wananchi wa maeneo hayo hawawezi kukubali.
 
Awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu mwingine wa rehma.

CHADEMA msilifanyie mzaha jambo hili maana nina uhakika kwa jinsi watu walivyochukizwa na wasaliti wachache walivyotuingiza kwenye gharama za uchaguzi bila sababu yeyote, lazima zitapigwa kura za hasira kiasi kwamba hata msaliti asipate kura za hata moja. Hakuna mwananchi atakayekua tayari kwenda kusimama kupigia kura kwa mtu aliyewasaliti kwa sababu ya hovyo halafu kisha akaitaka tena nafasi hiyo. Huyu mtu ni msaliti na haaminiki tena.

Kwahiyo kuna kila sababu ya CHADEMA kufanya kila namna kua kiongozi huyu Salum Mwalimu anapatia security ya kutosha kabla na wakati wa kuingia uchaguzi, wanaweza kujitokeza maadui wengi watakaotaka kutumia hila za kila namna ili kuhakikisha kua anakosa ushindi huo ulio dhahiri.Hawa watu wana mbinu nyingi sana sio la kubeza hili.

Ifahamike bayana kua Maulidi Mtulia hauziki kabisa Kinondoni, sio kwa sasa hata 2015 yenyewe alishinda tu kwa vile ulikua ni mwavuli wa UKAWA na kuchokwa kwa CCM. Kwa kawaida hiyo 2015 UKAWA wangelala wala asingeshinda na huo ndio ukweli wenyewe. Salum Mwalimu ni mjengaji mzuri wa hoja na anauzika sana bila shaka hilo halina ubishi, apatiwe ulinzi wa kutosha kijana huyu kulingana mahali atakapogombea na aina ya watu atakaopambana nao.

Nafasi yake ya unabu katibu mkuu inatosha tu kumpatia ulinzi, ni wajibu wa chama Chake kufanya hivyo.
Ndio tatizo lenu mnaanza na matarajio makubwa lakini mkipata loss mnaanza kusingizia wengine
 
Back
Top Bottom