Je, Chadema kuwa Na. 2 jimbo la Uzini Udini umeshindwa?

Tukubaline kitu gani mkuu? Ujue JF sehemu ya porojo ukija njoo na facts na data za kutosha eti Chadema hakuwa na mgombea Uzini uchaguzi uliopita.

Hakuna udini hapo hivi Chadema kupata kura 281 Uzini, ni mafanikio makubwa kwa Chadema?

ni mafanikio makubwa sana,si unajua znz ni ngome ya serikali ya umoja wa kitaifa,inakuaje mmoja wa wanandoa atoke nje? Yaonekana imani ya ndoa iyo ni finyu.hongera cdm
 
Narudia tena acha uongo wako hapa CDM haikusimamisha mgombea uwakilishi.Nenda kwenye web ya ZEC.CDM walisimamisha mgombea ubunge aliyeshindana na Seif Khatib.Sasa niambie kati yangu mimi na wewe nani muongo.Umekalia uongo na udini unashindwa hata kusema kitu jinsi kilivyo.Shame on you

Molome, hivi mtu kuwa muislam ndio udini ebu acheni unafiki wenu bana mnajiona wasafi kumbe hakuna lolote! Ebu niambie udini wangu upo wapi? Mnajifanya nyie sio wadini unafiki ni kitu kibaya sana.
 
Mods,

nakuomba uwaombe Mods wakusaidie kutafuta hayo maneno aliyobainisha kwani mimi nasimamia hapo hapo.
Mkuu wa Chuo.

Kumbuka kuwa sijakuambia bali niliandika. maana yake sikumbuki wapi nilikwambia.

Lakin kama ipo sehemu niliandika hivyo. nakuomba uiweke hapa ili tuijadili na kama ikithibitika hivyo nitakuwa wa kwanza kujipiga BAN milele pasi na kuwasubiri Mods.

ok sawa Dr Hamza Yousuf, uliandika kwasababu ukuniambia.
 
Mkuu, hivi Chadema kupata kura 281 Uzini ni mafanikio labda nikuulize uchaguzi uliopita Chadema walipata kura ngapi Uzini?
Natarajia sa hizi uko magomeni ukitokea posta kuelekea bonyokwa ukiwa kama ulivyozaliwa.
 
Salaam kwa Malaria Sugu, Rejeo, Ritz, Faizay Fox na wengine wanaoamini katika udini.

Tumeaminishwa kwamba chadema ni chama cha wakristo lakini kimeshika namba 2 kwenye uchaguzi wa jimbo la Uzini, Zanzibar mbele ya CUF ingawa wapo wanaoamini kwamba CUF ni chama cha Waislamu kimekuwa namba 3.

Hakuna chama cha kidini nchi hii.

Uchaguzi huu umetusaidia kujua kwamba kauli mbiu ya udini inachochewa na kundi la watu wachache kwa maslahi yao binafsi lakini naapa hawatashinda. Wenye haki ya kuzuia udini watashinda.

Faizay Fox na wenzake wamejaribu sana kuitangaza chadema ni chama cha wakristo, mnasemaje kuhusu hili JF.

hata kama uchaguzi haukuwa wa itikadi za dini. Jana waislamu bara na visiwani walipeana elimu juu ya katiba ya sasa na mchakato wa ile mpya ijayo na kwa msisitizo wakaambizana washiriki kwa wingi katika mchakato huo kusudi katiba isijeenda mikononi mwa "watu". Uliwaelewa juu ya kauli yao hii? Na je unaamini kuwa katiba ijayo inalenga maslahi ya nchi au itkadi ya dini fulani? tena basi ile ya kulenga kuihalalisha nchi kuwa chini ya hats na alhds.
 
Mtoto wa Rais Mwanaasha Kikwete pia amefanya vibaya kumbe kwa sababu katibu wa baraza la mtihani ni Mkristo? Kama Rais ana hakika mtoto wake ana akili asingeliacha hili jambo la uonevu lipite hivi hivi. kumbuka katibu huyo ni mteule wa Rais. Tumuogope Mungu.

unajua watu wanafikiri zaidi ndani ya box, hawataki kujishughulisha kufikiri zaidi, yaani wanasubiri mtu awasaidie kufikiri, ndio maana sheikh alipoongea vile wakapiga makofi!
 
alikuwa ana maneno machafu, sasa Hamza naomba nikuulize eti kipindi kile ulipopata Div I point 10 ukachaguliwa Ilboru katibu wa necta alikuwa dini gani maana kuna sheikh ametoa sababu za kisayansi eti katibu ni sababu ya shule na wanafunzi wa kiislamu kufanya vibaya. Na watu wakampigia makofi.

Mtoto wa Rais mkuu wa nchi amepata Div. 4 peke yake au ni wa mwisho darasani kwake Feza girls kwa nini wengine kila jambo wanaliangalia kidini?
 
Naomba niwaonye wadini wote kwamba Arumeru propaganda hiyo haitafua dafu.Chunguzeni watu wanaoishi Arumeru.Poleni sana.

Kwani wewe umechunguza Zanzibar ni kina nani?

Hayo maneno yako yanaonyesha wewe ni mdini mkubwa...mkuu acha unafiki basi.
 
Molome, hivi mtu kuwa muislam ndio udini ebu acheni unafiki wenu bana mnajiona wasafi kumbe hakuna lolote! Ebu niambie udini wangu upo wapi? Mnajifanya nyie sio wadini unafiki ni kitu kibaya sana.

Narudia tena vita yenu ya udini mliyopigana uzini isiishie hapo.Hamieni na Arumeru kwa propaganda hiyo hiyo halafu majibu yake mtapata
 
ok sawa Dr Hamza Yousuf, uliandika kwasababu ukuniambia.

Sasa naomba hata kama unakumbuka title ya thread mimi nitakusaidia kuitafuta na waombe Mods vile vile wakusaidie ili tuiweke hadharani nami nijipige BAN kama itathibitika kuwa nimeandika hicho ulichonena.

Nakushauri sana uwe makni na yakini sana katika kuthibitisha kile unachoandika.

Kwani wewe umechunguza Zanzibar ni kina nani?

Hayo maneno yako yanaonyesha wewe ni mdini mkubwa...mkuu acha unafiki basi.

Mkuu mimi sio mdini ila nina chuki kubwa sana na watu wanaochochea udini.Uzini vilisambazwa vikaratasi vingi sana vya kuchochea udini na kukashifu CDM hata nakala yake ninayo.Hapa JF akina Barubaru kwa makusudi waliandika uongo viongozi wa CDM watazindua kampeni kutokea kanisani.Hii ni dhambi kubwa na mbaya sana.Mkuu utanisamehe nikionyesha hisia zangu kali kulaani wahuni wa aina hii.Tutaligawa taifa letu vipandevipande bila sababu za msingi.
 
Molome, hivi mtu kuwa muislam ndio udini ebu acheni unafiki wenu bana mnajiona wasafi kumbe hakuna lolote! Ebu niambie udini wangu upo wapi? Mnajifanya nyie sio wadini unafiki ni kitu kibaya sana.

Tuko mbioni kuanzisha na kuyatambua rasmi majina ya wadini kwa matendo yao hapa JF wewe utakuwa mmojawapo. Usifikiri wengine hatuna dini lakini kwenye mvutano wa kidini jitahidi kuwa kati (neutral) kama unataka tusikuite udini kwa sababu nyumba (Tanzania) tunayoishi ni moja ikiungua wote tunakufa.
 
Mkuu mimi sio mdini ila nina chuki kubwa sana na watu wanaochochea udini.Uzini vilisambazwa vikaratasi vingi sana vya kuchochea udini na kukashifu CDM hata nakala yake ninayo.Hapa JF akina Barubaru kwa makusudi waliandika uongo viongozi wa CDM watazindua kampeni kutokea kanisani.Hii ni dhambi kubwa na mbaya sana.Mkuu utanisamehe nikionyesha hisia zangu kali kulaani wahuni wa aina hii.Tutaligawa taifa letu vipandevipande bila sababu za msingi.

Kwa kuanzia na hapa Jf wadini walaaniwe na kizazi chao chote milele na milele
 
Ha ha haaaa, niliposikia matokeo nikajua utani hadi baada ya kupata news kamili humu jamvini ndio nikajua kumbe kweli KIMENUKA kwa CUF. Tunasuburi jimbo la Wawi ili hatimaye CDM iingie rasmi visiwani. Hongera CDM kwa kushika upili Uzini, hii ni confidence boost ahead of Arumeru election.

Moto waliokuwa nao CUF Zanzibar miaka iliyopita haukuwa wa kawaida na siku zote walilalamikia kuchakachuliwa na CCM, kwa matokeo ya Uzini, je CHADEMA nao wamechakachua? Matokeo haya yanaonyesha kuwa CCM bado ni chama kinachopendwa na hivyo vyama vyama vya upinzani vitaibuka na kujimaliza vyenyewe... hata kama CDM wameshika nafasi ya pili si tishio kwa CCM.
 
Tuko mbioni kuanzisha na kuyatambua rasmi majina ya wadini kwa matendo yao hapa JF wewe utakuwa mmojawapo. Usifikiri wengine hatuna dini lakini kwenye mvutano wa kidini jitahidi kuwa kati (neutral) kama unataka tusikuite udini kwa sababu nyumba (Tanzania) tunayoishi ni moja ikiungua wote tunakufa.

Mpo mbioni kuyatambua nyie ni kina nani mkuu?

Kwa kweli mie sitishiki na hayo maneno yako kama kuwa muislam ndio kuwa mdini basi jina langu liweke la kwanza.

Ebu niambie udini wangu ni upi?
 
Kwa kuanzia na hapa Jf wadini walaaniwe na kizazi chao chote milele na milele

Bila kutoa tafsiri ya MDINI ni nani? Nafikiri itakuwa vigumu
mosi. Kwa mtu mwenyewe kujitambua kama ni mdini na hivyo kuacha tarbia hiyo mara moja.
Lakin Pili itakuwa vigumu kwa Muumba kumlaani.

Tunaomba tafsiri yako. Mdini ni nani?

Narudia tena vita yenu ya udini mliyopigana uzini isiishie hapo.Hamieni na Arumeru kwa propaganda hiyo hiyo halafu majibu yake mtapata

Mkuu Molemo,
Ebu niambie udini wangu ni upi? Au mtu kuwa muislam ni tatizo kwako ndio unapata tafsiri ya udini?
 
Moto waliokuwa nao CUF Zanzibar miaka iliyopita haukuwa wa kawaida na siku zote walilalamikia kuchakachuliwa na CCM, kwa matokeo ya Uzini, je CHADEMA nao wamechakachua? Matokeo haya yanaonyesha kuwa CCM bado ni chama kinachopendwa na hivyo vyama vyama vya upinzani vitaibuka na kujimaliza vyenyewe... hata kama CDM wameshika nafasi ya pili si tishio kwa CCM.

Siasa za Znz ni tofauti.

Je unajuwa kwanini CUF wapo tayari kurudia uchaguzi jimbo la WAWI kule kwa Hamad Rashid.

Kumbuka kile chama kule kina ngome zake na hizo piga ua majibu utayapata.

Kumbuka 2003 uchaguzi wa majimbo ya Pemba, nani alipata kura nyingi (kura zilizoharibika na zile zisizo haribika) na kuleta utata mkubwa sana kwenye Sheria za uchaguzi.

Nilibainisha hilo ni somo tosha kujua Hakuna kutumia nguvu nyngi wakti unajuwa fika utashindwa.

Tunampongeza Mh Raza.
 
Back
Top Bottom