Uchaguzi 2020 Je, CHADEMA itamuunga mkono Maalim Seif kule Zanzibar na Membe atamuunga mkono Tundu Lissu katika nafasi ya Urais huku Bara?

eeeh kweli aisee 😂 😂 😂 😂 😂

Vijana wa polepole hao Mkuu, kodi zetu zinatumika vibaya sana. Kununulia wapinzani, kuwalipa ninyi elfu saba saba na kuhudumia maharawa wa mkulu kama akina jocate na wenzake.
 
Baraza la Mawaziri- 2020-2025

Raisi- Tundu Antipas Lissu

Makamu Raisi- Salum Mwalimu

Waziri Mkuu- Bernad C Membe

Waziri/Nje- Lazaro Nyalandu

Waziri/ Fedha- Zitto Kabwe

Waziri Ulinzi- Esther Bulaya

Waziri Sheria- Halima Mede

Waziri Afya- Juma Duni Haji

Waziri Muungano- Ismail Jussa

Waziri/ Viwanda, Biashara na Uwekezaji- Freeman Mbowe

Waziri/ Tamisemi- Mnyika

Waziri/ Ndani- Godbless Lema

Waziri/ Michezo Burudani- Joseph Mbilinyi

Waziri Watoto Maendeleo ya Jamii- Suphian(kutoka ACT)

Waziri Uchukuzi- John Heche

Waziri Madini- Fatma Karume

Waziri Mafuta/ Gesi- Esther Matiko

Waziri Maliasili/ Utalii- Mch Msigwa

Waziri Ardhi- Godlisten Malisa


Waziri/Maji- Ado Shaibu

Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu- Maria Sarungi

Katibu Mkuu/ Kiongozi- Prof Assad
ulaji huo wizara zisiwe nyingi labda na nane tu
Wizara ya Ulinzi na mambo ya ndani
Wizara ya Viwanda na Biashara
Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
Wizara ya Sheria na ustawi wa jamii
Wizara ya elimu michezo na utamaduni
Wizara ya Maendeleo ya kilimo ufugaji na Mazingira
Wizara ya fedha
Wizara ya mail asili
....... haya weka mawaziri hapo
 
Mara hii upinzani umejiandaa tofauti na mawazo ya Ccm. Ikitokea wamemuengua mgombea yeyote kwa hila wasitegemee mteremko. Usishangae hata TADEA wakachukua urais.
 
Najua kuwa mazungumzo bado yanaendelea kati ya Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na Chama cha ACT Wazalendo ya namna ya kuachiana nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mazingira niliyoyaona Leo kwa mgombea wa Urais wa chama cha Chadema, Tundu Lissu kuibuka kwenye mkutano mkuu wa ACT Wazalendo, natabiri kuwa mazungumzo ya kuachiana kwa nafasi mbalimbali, yanaendelea vizuri sana na yapo mategemeo makubwa sana ya kufikia muafaka kwa vyama hivyo.

Nafahamu pia hakuna mtanzania asiyefahamu nguvu ya kisiasa ya Maalim Seif, kule Zanzibar.

Kwa hiyo itakuwa kwa maslahi mapana ya upinzani wa nchi hii, kuweza kuunganisha nguvu kwa vile vyama makini, ambavyo kwa sasa naviona kuwa ni hivi vyama viwili vya Chadema na ACT Wazalendo, ili kuwezesha wasizigawe kura hizo kwa hao wagombea.

Nayatakia kila la kheri mazungumzo hayo yanayoendelea, ili hatimaye yafikie muafaka kwa maslahi mapana kwa upinzani nchini na naamini yatakuwa ni "maumivu" makubwa sana kwa jamaa zetu wa chama tawala cha CCM, iwapo mazungumzo hayo yatazaa matunda
Huu mchezo mtamu saaaana
 
Mara hii upinzani umejiandaa tofauti na mawazo ya Ccm. Ikitokea wamemuengua mgombea yeyote kwa hila wasitegemee mteremko. Usishangae hata TADEA wakachukua urais.
Hawa CCM safari hii wametaitiwa kisawasawa!

Ngoja tuone ngoma itakavyochezwa hapo mwezi wa October
 
chilubi
Naku-quote ulivyosema

Ni lazima CCM ilindwe Zanzibar!

Kwa maana hiyo kwa uliyoyasema, hakuna haja ya uchaguzi Zanzibar!

Nikuambie tu kuwa Maalim Seif ameshaonya kuwa hatakuwa tayari kwa yale aliyoyaona 2015, kwa Jecha "kupindua" matokeo

Hivi unadhani nini kitatokea kwa nyinyi CCM kujiapiza kuwa NI LAZIMA ZANZIBAR ILINDWE?

Tunamuomba Mungu atuepushe na hali hiyo na awape busara nyinyi CCM, kuwa mheshimu uamuzi utakaofanywa na wananchi wa Zanzibar kupitia sanduku la kura. OVA
Kwani aliekwambia mie CCM nani?

Mimi nazungumza ukweli halisi, wewe unaendelea kuishi kwenye ndoto.Mtakapoamka ndipo mtakapopewa serikali. Hizo Kauli za Maalim Seif zisikushuhulishe, mwisho wa siku yeye mwenyewe huwa ndio anaishia kuwatuliza watu. Yeye kama kiongozi, awe mstari wa mbele katika kutekeleza onyo lake, sio wanaumia wengine yeye kajichimbia sehemu.

Walishasema dhahir shahir, nchi haitolewi kwa makaratasi.

CCM zanzibar bila kulindwa na ya bara hamna kitu. Au hujui siku zote CCM zanzibar inalindwa tu? Hivi unafikiri CCM ichukue bara Zanzibar akae Maalim Seif pana Muungano hapo?
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom