Uchaguzi 2020 Je, CHADEMA itamuunga mkono Maalim Seif kule Zanzibar na Membe atamuunga mkono Tundu Lissu katika nafasi ya Urais huku Bara?

Uchaguzi gani unaouzungumzia unafanyika Zanzibar? Kwani rais wa zanzibar si keshajulikana? Wapinzani wanapoteza muda wao bure, ni heri wajiepushe na mikutano ya kampeni na watafute ya maana wafanye.

Kwani si sote tumeona namna alivyopokelewa mrithi wa urais zanzibar alipotembelea visiwa vyake hivi karibuni. Sote tumeona namna alivyokuwa analindwa sio lindo la mgombea urais bali ni lindo la rais. Linalosubiriwa zanzibar ni siku sherehe ya kurithishwa madaraka ya urais tu sio uchaguzi.
Waziri wa ulizi lazima apewe ulizi ila ule uliongezwa kwa kuwatisha wazanzibari tu.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Najua kuwa mazungumzo bado yanaendelea kati ya Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na Chama cha ACT Wazalendo ya namna ya kuachiana nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mazingira niliyoyaona Leo kwa mgombea wa Urais wa chama cha Chadema, Tundu Lissu kuibuka kwenye mkutano mkuu wa ACT Wazalendo, natabiri kuwa mazungumzo ya kuachiana kwa nafasi mbalimbali, yanaendelea vizuri sana na yapo mategemeo makubwa sana ya kufikia muafaka kwa vyama hivyo.

Nafahamu pia hakuna mtanzania asiyefahamu nguvu ya kisiasa ya Maalim Seif, kule Zanzibar.

Kwa hiyo itakuwa kwa maslahi mapana ya upinzani wa nchi hii, kuweza kuunganisha nguvu kwa vile vyama makini, ambavyo kwa sasa naviona kuwa ni hivi vyama viwili vya Chadema na ACT Wazalendo, ili kuwezesha wasizigawe kura hizo kwa hao wagombea.

Nayatakia kila la kheri mazungumzo hayo yanayoendelea, ili hatimaye yafikie muafaka kwa maslahi mapana kwa upinzani nchini na naamini yatakuwa ni "maumivu" makubwa sana kwa jamaa zetu wa chama tawala cha CCM, iwapo mazungumzo hayo yatazaa matunda
Watatuweza kweli!?!...Aaah wapi
Hatawaunganee!?!....

Upinzani waungane wasiungane ushindi CCM upo pale pale (Bara & Zanzibar)
 
Hata kama wangeachiana vyumba vya kulala. Swali la kujiuliza hivi vyama vina influence gani kwa wananchi? Eti CHADEMA watamuunga mkono Maalim Seif Zanzibar. CHADEMA wanainfluence gani Zanzibar? Maalim Seif anahitaji kweli support ya CHADEMA Zanzibar? Huu si utapeli?
Utapeli wa mchana jua linawaka
 
Ni suala la muda kidogo tu watanzania mta-smile tena!! We fikiri kitendo cha Lissu kutia mguu ACT leo kukutana ana kwa ana na Zitto na Membe, Msajili kashasema kaenda kufanya nini wakati mkutano si wake!! Nafikiri watasema kaenda kufanya fujo kwa shughuli ya wenzake.

Ni lazima ushuhudie mengi wakati Marehemu anakata roho!!
 
Waungane wasiungane hawawezi kushinda watamsindikiza magufuli kwenye ushindi wake wa kishindo,wao wataendelea kuitwa wapinzani mpaka kufa kwao,nje na CCM wakukamata dola hajazaliwa
Jina la mtu huwa haliandikwi kwa kuanza na herufi ndogo. Upinzani ni afya na utakuwepo hata baada ya kufa kwako.
 
Uchaguzi gani unaouzungumzia unafanyika Zanzibar? Kwani rais wa zanzibar si keshajulikana? Wapinzani wanapoteza muda wao bure, ni heri wajiepushe na mikutano ya kampeni na watafute ya maana wafanye.

Kwani si sote tumeona namna alivyopokelewa mrithi wa urais zanzibar alipotembelea visiwa vyake hivi karibuni. Sote tumeona namna alivyokuwa analindwa sio lindo la mgombea urais bali ni lindo la rais. Linalosubiriwa zanzibar ni siku sherehe ya kurithishwa madaraka ya urais tu sio uchaguzi.
Umenikumbusha kipindi cha kampeni ulinzi wa Magufuli ulikwa balaa!, komakoma siku anatoka mwanza kwenda chato kupiga kura ,ilikua siku ya j,pili,msafara wake ulikuwa unatembea na layne zote barabarani,hakuna gari ya kupishana na msafara wake.
Ukweli rais hupangwa na kundi flani ndani ya nchi,sisi wengine hutimiza tu takwa la kikatiba kwa kupiga kura,lakini kura za urais haziamui labda za ubunge na udiwani
 
Baraza la Mawaziri- 2020-2025

Raisi- Tundu Antipas Lissu

Makamu Raisi- Salum Mwalimu

Waziri Mkuu- Bernad C Membe

Waziri/Nje- Lazaro Nyalandu

Waziri/ Fedha- Zitto Kabwe

Waziri Ulinzi- Esther Bulaya

Waziri Sheria- Halima Mede

Waziri Afya- Juma Duni Haji

Waziri Muungano- Ismail Jussa

Waziri/ Viwanda, Biashara na Uwekezaji- Freeman Mbowe

Waziri/ Tamisemi- Mnyika

Waziri/ Ndani- Godbless Lema

Waziri/ Michezo Burudani- Joseph Mbilinyi

Waziri Watoto Maendeleo ya Jamii- Suphian(kutoka ACT)

Waziri Uchukuzi- John Heche

Waziri Madini- Fatma Karume

Waziri Mafuta/ Gesi- Esther Matiko

Waziri Maliasili/ Utalii- Mch Msigwa

Waziri Ardhi- Godlisten Malisa

Waziri/Maji- Ado Shaibu

Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu- Maria Sarungi

Katibu Mkuu/ Kiongozi- Prof Assad
 
Yaani Mimi kilio changu ni Tume iliyo Huru na ya Haki.Uchaguzi wa mwaka huu ungependeza!
 
Uchaguzi gani unaouzungumzia unafanyika Zanzibar? Kwani rais wa zanzibar si keshajulikana? Wapinzani wanapoteza muda wao bure, ni heri wajiepushe na mikutano ya kampeni na watafute ya maana wafanye.

Kwani si sote tumeona namna alivyopokelewa mrithi wa urais zanzibar alipotembelea visiwa vyake hivi karibuni. Sote tumeona namna alivyokuwa analindwa sio lindo la mgombea urais bali ni lindo la rais. Linalosubiriwa zanzibar ni siku sherehe ya kurithishwa madaraka ya urais tu sio uchaguzi.
Are you serious Mtanzania?

Hivi hujui alichokifanya huyo mtu wenu Jecha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015?

Hivi mtu aliyewahenyesha mno katika uchaguzi mkuu wa 2015, ndiyo leo umuite si lolote wala chochote?
 
Opposition parties in Tanzania need to join forces when the country goes to the polls, to change the course of history and ensure that future generations get the chance to enjoy a brighter life.

[https://s3-eu-west-1]
Sio sasa labda baada ya katiba mpya.
Personal interests are greater than national interest
Wacha vizazi vya baade waanzie kwenye msingi watumie akili zisizo na kasumba.
 
Waungane wasiungane hawawezi kushinda watamsindikiza magufuli kwenye ushindi wake wa kishindo,wao wataendelea kuitwa wapinzani mpaka kufa kwao,nje na CCM wakukamata dola hajazaliwa

Ni mwandiko wa jitu lisilo na akili linajua tumia simu tu ku comment kitu hajui kaandika nini...baba ako akiona hii post atajuta kwann lile bao hakumwaga baharini samaki wale hata
 
Najua kuwa mazungumzo bado yanaendelea kati ya Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na Chama cha ACT Wazalendo ya namna ya kuachiana nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mazingira niliyoyaona Leo kwa mgombea wa Urais wa chama cha Chadema, Tundu Lissu kuibuka kwenye mkutano mkuu wa ACT Wazalendo, natabiri kuwa mazungumzo ya kuachiana kwa nafasi mbalimbali, yanaendelea vizuri sana na yapo mategemeo makubwa sana ya kufikia muafaka kwa vyama hivyo.

Nafahamu pia hakuna mtanzania asiyefahamu nguvu ya kisiasa ya Maalim Seif, kule Zanzibar.

Kwa hiyo itakuwa kwa maslahi mapana ya upinzani wa nchi hii, kuweza kuunganisha nguvu kwa vile vyama makini, ambavyo kwa sasa naviona kuwa ni hivi vyama viwili vya Chadema na ACT Wazalendo, ili kuwezesha wasizigawe kura hizo kwa hao wagombea.

Nayatakia kila la kheri mazungumzo hayo yanayoendelea, ili hatimaye yafikie muafaka kwa maslahi mapana kwa upinzani nchini na naamini yatakuwa ni "maumivu" makubwa sana kwa jamaa zetu wa chama tawala cha CCM, iwapo mazungumzo hayo yatazaa matunda
Nawatakia kila la kheri katika hili; ingawa TAKE MY WORD hakuna mgombea yoyote au yeyote kati hao wote walioteuliwa na vyama vyao kukubali kuachiana nafasi za ngazi ya ueais. Wote wana tamaa ya kufa mtu na wote wanaamini watashinda na kuwa rais wa Tanzania. Hivyo hivyo hata kwenye ngazi ya Ubunge, wote wanataka hiyo RUZUKU kwa kufa na kupona na hapo ndipo KUSHINDWA KWAO KUNAPOANZIA. Subiri uone!
 
Achana na upepo wa Lowasa na ukawa,kama walishindwa 2015 akuna tena wakuitikisa CCM,tena hii CCM ya Magu ndo kabisaa.
 
Yaani Mimi kilio changu ni Tume iliyo Huru na ya Haki.Uchaguzi wa mwaka huu ungependeza!
Wewe hujawahi sikia onyo alilolitoa mgombea Urais Tundu Lissu?

Ameshawaonya hao Tume ya uchaguzi kuwa uchaguzi wa mwaka huu unatakiwa uwe huru na haki kikweli kweli, ama sivyo atawaelekeza wapiga kura wake waingie barabarani
 
Back
Top Bottom