Uchaguzi 2020 Je, CHADEMA itamuunga mkono Maalim Seif kule Zanzibar na Membe atamuunga mkono Tundu Lissu katika nafasi ya Urais huku Bara?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,521
30,222
Najua kuwa mazungumzo bado yanaendelea kati ya Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na Chama cha ACT Wazalendo ya namna ya kuachiana nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mazingira niliyoyaona Leo kwa mgombea wa Urais wa chama cha Chadema, Tundu Lissu kuibuka kwenye mkutano mkuu wa ACT Wazalendo, natabiri kuwa mazungumzo ya kuachiana kwa nafasi mbalimbali, yanaendelea vizuri sana na yapo mategemeo makubwa sana ya kufikia muafaka kwa vyama hivyo.

Nafahamu pia hakuna mtanzania asiyefahamu nguvu ya kisiasa ya Maalim Seif, kule Zanzibar.

Kwa hiyo itakuwa kwa maslahi mapana ya upinzani wa nchi hii, kuweza kuunganisha nguvu kwa vile vyama makini, ambavyo kwa sasa naviona kuwa ni hivi vyama viwili vya Chadema na ACT Wazalendo, ili kuwezesha wasizigawe kura hizo kwa hao wagombea.

Nayatakia kila la kheri mazungumzo hayo yanayoendelea, ili hatimaye yafikie muafaka kwa maslahi mapana kwa upinzani nchini na naamini yatakuwa ni "maumivu" makubwa sana kwa jamaa zetu wa chama tawala cha CCM, iwapo mazungumzo hayo yatazaa matunda
 
Screenshot_20200805-165712.jpg
 
Hata kama wangeachiana vyumba vya kulala. Swali la kujiuliza hivi vyama vina influence gani kwa wananchi? Eti CHADEMA watamuunga mkono Maalim Seif Zanzibar. CHADEMA wanainfluence gani Zanzibar? Maalim Seif anahitaji kweli support ya CHADEMA Zanzibar? Huu si utapeli?
 
Waungane wasiungane hawawezi kushinda watamsindikiza magufuli kwenye ushindi wake wa kishindo,wao wataendelea kuitwa wapinzani mpaka kufa kwao,nje na CCM wakukamata dola hajazaliwa
Lissu hajawahi kugombania akashindwa, alishinda u Rais wa Tanganyika Law Society licha ya Mwakyembe akiwa Waziri wa Sheria kumuwekea mapingamizi.
 
Uchaguzi gani unaouzungumzia unafanyika Zanzibar? Kwani rais wa zanzibar si keshajulikana? Wapinzani wanapoteza muda wao bure, ni heri wajiepushe na mikutano ya kampeni na watafute ya maana wafanye.

Kwani si sote tumeona namna alivyopokelewa mrithi wa urais zanzibar alipotembelea visiwa vyake hivi karibuni. Sote tumeona namna alivyokuwa analindwa sio lindo la mgombea urais bali ni lindo la rais.

Linalosubiriwa zanzibar ni siku sherehe ya kurithishwa madaraka ya urais tu sio uchaguzi.
 
Hata kama wangeachiana vyumba vya kulala. Swali la kujiuliza hivi vyama vina influence gani kwa wananchi? Eti CHADEMA watamuunga mkono Maalim Seif Zanzibar. CHADEMA wanainfluence gani Zanzibar? Maalim Seif anahitaji kweli support ya CHADEMA Zanzibar? Huu si utapeli?
Maalim Seif Sharif anamkubali sana Tundu Lissu na Tundu Lissu anamkubali sana Maalim Seif. Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa kihistoria kuliko ule wa 2015. Namuona mzee wa push up aki panic🤣


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
CDM wanalazimika kuungana na ACT kwa Zanzibar sababu hawajawahi hata kuwa na "sheha" visiwani toka kuasisiwa kwao 1992 labda yule viti maalum na si elected.

Kilichomtoa Membe CCM ni urais na si urais tu bali Urais 2020.

Kilichomfanya Membe ahamie ACT na si chama kikuu cha upinzani CDM ni uhakika wa kuwa mgombea urais 2020.

Na isingekuwa Membe kuwa ACT,CDM wasingejihangaisha hata na kuungana na Zitto kama ilivyokuwa 2015.

Je Membe atakubali ndoto zake zisitimie kwa kumuunga mkono Lisu?
 
Lissu hajawahi kugombania akashindwa, alishinda u Rais wa Tanganyika Law Society licha ya Mwakyembe akiwa Waziri wa Sheria kumuwekea mapingamizi.
Aligombea ubunge kupitia nccr mageuzi akashindwa au hujui Hilo? Turudi kwenye mada uchaguzi huu ataingia kwenye list ya wagombea wa chadema walioshindwa kwenye uraisi Kama wenzake waliogombea
 
Back
Top Bottom