CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
Nadhani huyu ndiye atakuwa Waziri Mkuu mstaafu wa mwisho kuwepo Chadema. Nikitizama Salim, Warioba, Msuya, Pinda na hata Majaliwa sioni uwezekano wowote wa Chadema kupewa fursa ya kumhifadhi Waziri Mkuu mstaafu tena.
Ukichunguza kwa makini utabaini kuwa ujio wa mawaziri wakuu umeiumiza mno chadema. Wanaweza kupuuza kama ilivyo desturi yao lakini hakika majeraha ni makubwa mno.
Ukianza na Lowasa hasara aliyowatia mwaka 2015 katikati ya uchaguzi mkuu ilikuwa kubwa. Nitaje Tu hasara chache.
CHADEMA ilipoteza hoja ya ufisadi. CHADEMA ilipata mshika bendera ambaye hakika hakuwasaidia sana kwenye kampeni. CCM ilipata fursa ya kuibomoa CHADEMA kutokana na mgombea wao.
Ukija kwa Sumaye ni hivyo hivyo. Hoja ya ufisadi isingesimama. Lakini Sumaye kaongeza jeraha baya mno. Kadhihirisha kuwa CHADEMA hakuna demokrasia.
Watamkashifu wee lakini kawaumbua. Jina haliendani na matendo ndani ya chama. Zile tuhuma kuwa Mbowe ndie kila kitu zimethibitika! Zile tuhuma kuwa kuna "inner cabinet" imethibitika. Hiki ndio kimemkimbiza Profesa Safari!
Je, CHADEMA itathubutu tena kupokea wakubwa kutoka CCM? Hakika sasa watakuwa na hofu. Je walioko Chadema na walitoka CCM wako salama? Haswa Nyalandu! Je kuna waliopo CCM watatamani kwenda CHADEMA? Mhhhh!
Hakika Chadema badala ya faida imeambukia hasara! Sasa wataelewa msemo wa "oil chafu"?
Badala ya kumshambulia Sumaye ni vyema wayafanyie kazi mapungufu ambayo Petrobus, Prof Safari na Sumaye wameyaonyesha. Tayari kuna dalili za mpasuko kanda ya Pwani!
Wana UKAWA mtaweza kwenda na CHADEMA? Kama ndani mwao ndio hivi vipi nyie wakuja?