Je, CDF na IGP wakifikisha miaka 60 wanaweza kuongezewa muda au lazima wastaafu?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kwa mujibu wa katiba na Sheria za nchi yetu viongozi waandamizi wa polisi, Jeshi la Wananchi na wengineo wakistaafu wanaruhusiwa kuomba kuongezewa muda au mteule wao anaweza waongezea muda?

Kama wataongezewa muda, ukomo wakuwaongezea muda ni miaka mingapi?

Je, ipo mifano ya viongozi wa vyombo hivi ambao wamewahi kuongezewa muda wakiutumishi baada yakuvuka umri wa kustaafu?
 
Huwa wanaongezewa mwaka mmoja mmoja akipenda mwenye mamlaka..ila kazi ya kiutumoshi ataifanya hado maika 65 ..baada ya hapo ndo hustaafu rasm atatumika kama mstaafu tu.
Sirro atafikisha miaka 60 mwaka 2023
 
Jibu sahihi kwa TPDF ni kwamba inatagemea mambo matatu; (1) Kama deputy wake bado ni kijana: kwa mfano iwapo Chief of staff ana miaka kama 55 hivi basi anaweza kupanda kuwa CDF kwa miaka mingine mitano, lakini iwapo CoS naye ana miaka hiyo 59 au 60, basi Rais anaweza kumweongezea muda wa mwaka mmoja CDF na kuteua Chief of Staff kwa mwaka mmoja kabla hajampandisha kuwa CDF. (2) Kama kuna operation ambayo Rais anataka ikamilike kwanza kabla ya kubadilisha uongozi wa jeshi; kwa mfano hawezi kustaafisha CDF wakati nchi iko vitani hata kama kweli kafikia miaka 60. (3) Ikimpendeza rais, anaweza kuamua lolote kwa sababu yoyote ile au bila kuwa na sababu yoyote.
 
Hakuna mtu anayependa kustaafu muelewe,waacheni nao wale mema ya nchi
Una maana gani kusema hamna mtu anayependa kustaafu? Yaani hiyo kauli yako unaiona iko sawa kabisa. Kama mtu amechoka na kazi na muda kuondoka umefika na kikokotoo chake kipo tayari kwanini asipende!
 
Jibu sahihi kwa TPDF ni kwamba inatagemea mambo matatu; (1) Kama deputy wake bado ni kijana: kwa mfano iwapo Chief of staff ana miaka kama 55 hivi basi anaweza kupanda kuwa CDF kwa miaka mingine mitano, lakini iwapo CoS naye ana miaka hiyo 59 au 60, basi Rais anaweza kumweongezea muda wa mwaka mmoja CDF na kuteua Chef of staff kwa mwaka mmoja kabla hajampandisha kuwa CDF. (2) Kama kuna operation ambayo rauis anataka ikamilike kwanza kabla ya kubadilisha uongozi wa jeshi; kwa mfanoi hawezi kustaafisha CDF wakati nchi iko vitani hata kama kweli kafikia miaka 60. (3) Ikimpendeza rais, anaweza kuamua lolote kwa sababu yoyote ile au bila kuwa na sababu yoyote
Siyo lazima CoS amrithi CDF, ye yote kuanzia Brigadier General anaweza kuwa CDF. Ni mapenzi ya Rais kuamua.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom