Je, CDF na IGP wakifikisha miaka 60 wanaweza kuongezewa muda au lazima wastaafu?

Viongozi Hawa wawili wametumikia nchi na wanaendelea kutumikia nchi kwa weledi na uwezo waliojaliwa, wamefanya sehemu yao na sasa wanaelekea uzeeni ambapo watakabidhi mikoba kwa vijana waendelee kulinda nchi yetu.

Viongozi waandamini na hata wa chini ndani ya majeshi haya tunawafahamu kwa kuwa wanatoka kwenye familia zetu.

Nchi ni Mali ya wananchi na wananchi ndo sisi, je kwa kuzingatia kasi ya awamu ya tano, muda wa kustaafu hawa viongozi utakapofika, unadhani nani anafaa kupokea kijiti? Kwanini unadhani anafaa?
 
Jeshini sio sawa NSSF au TAZARA,kwamba utafanya mabadiliko kizembe zembe tu
Kule Misri,hayati Mubarak alikua na mkuu wa majeshi akiitwa field Marshal Tantawi,kile kibabu kilikua na miaka 70,akaingia Morsi akakifyekelea mbali na majenerali wengine Kama 50 hivi
Morsi bila utafiti au kwa kudhani kamaliza masalia ya Mubarak,akamteua Jenerali Al Sisi kuwa mkuu wa majeshi
Kumbe Wana usongo nae,Sisi alikwenda tu ikulu akamwambia pisha hapo,Kisha bwana Morsi akapelekwa jela
 
Hawaombi bali Rais ana mamlaka ya kuwaongezea muda wa mwaka mmoja mmoja na kwa idhini yao wenyewe wakakubali. Kwa mfano Gen. Mwamunyange aliongezewa mwaka mmoja, aliteuliwa wa pili kwasababu za kiafya alimuomba mh. Rais apumzike akakubaliwa. Pia Kama sijasahau Ins. Gen wa police Mahita naye aliongezewa mwaka mmoja kama si miwili.
Jibu rahisi ni kwamba inawezekana mkuu
 
Siyo lazima CoS amrithi CDF, ye yote kuanzia Brigadier General anaweza kuwa CDF. Ni mapenzi ya Rais kuamua.
Utaratibu wa jeshi hauko hivyo mkuu. Huko Kuna kitu kinaitwa hierarchy yaani anayefuatia kingazi ndiye anayetwaa madaraka ya mbele yake. Kwa cheo cha CDF kinatwaliwa na Mnadhimu mkuu wa jeshi pia hapo hapo Katiba ya jeshi ikimtambua kama Military Financial Controller MFC ambaye sharti awe na rank ya Lieutenant General.
Jeshi sio kama polisi kwa Commissioner of police yeyote anaweza kuwa Inspector General.
 
Kumbuka case ya Mabeyo urudie tena kusema.
 
Kwa kifupi Rais anauwezo wa kuwaongezea miaka pindi kukiwa na ulazima wa kufanya hivyo. Na sio tu kwa CDF au IGP bali hata kwa maofisa wajuu pindi itakapo bidi.
 
Kumbuka case ya Mabeyo urudie tena kusema.
Nimekwambia huo ni utaratibu wa kijeshi kutokana na Katiba ya TPDF. Kuvunja Katiba kwa kiongozi wa nchi sio kuhalalisha kitendo kuwa utaratibu. Kama tunasema ni mvunja katiba wadhani alianzia wapi? Au mangapi ambayo ameenda nje ya utaratibu wa Katiba? So usishangae mkuu
 
Wewe ni mjeshi?
 
Mkuu, una mzee wako huko jeshini so unajaribu kupiga ramli kuona kama ana ushawishi?

Maana hivi vyeo viwili vinakutesa
 
Back
Top Bottom