Je, CCM wana nia ya kweli ya kutupa Tume Huru ya Uchaguzi? Basi twaweza sema: Good objective, wrong approach henceforth, no results

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Wasielewa waelewe hili;

Kwamba, CCM ni chama cha siasa kama vilivyo vyama vingine vyote hapa nchini kwa maana ya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi, ACT WAZALENDO nk nk.

Malengo ya chama chochote cha siasa huwa ni yale yale kubwa likiwa ni kushika dola.

CCM kwa sasa na pengine tangu uhuru 1961 katika majina tofauti TANU (1961 - 1977) na CCM (1977 mpaka leo) ndicho kimeongoza dola kipindi chote hicho iwe ni kwa hila au kwa uhalali.

Kuwatoa madarakani, si kazi rahisi kwa sababu ni sawa na kuwaambia waache kuwa chama siasa chenye lengo la kushinda uchaguzi, kuunda serikali na kuongoza dola.

Ni ukweli usiopingika pia kuwa, mara nyingi kama siyo zote, CCM wamekuwa wakishinda chaguzi zote kwa HILA zinazoambatana na MABAVU kwa kutumia advantage ya vyombo vya dola kama Polisi, TISS, NEC, Mahakama ambavyo kwa mfumo wa kisheria na kikatiba wa nchi yetu, vyombo hivi mara zote vinatii na kuwatumikia watawala walioko madarakani chini ya CCM kwa sasa.

Whether we like it or not, ikitokea muujiza leo CCM wakafurushwa madarakani na kujikuta wako nje ya dola/serikali kuwa chama cha upinzani (wakipata bahati hiyo) na chama kingine chochote mfano CHADEMA au CUF au ACT WAZALENDO kikashika dola na kuunda serikali, chini ya mfumo wa kisheria na kikatiba huu tulio nao sasa, obviously, chama hicho hakiwezi kufanya tofauti na wanavyofanya CCM leo yaani kutumia weakeness ya kisheria na kakatiba kujipendelea ikiwemo kujishindisha uchaguzi kwa nguvu.

On the other hand, vivyo hivyo CCM kikiwa kwenye nafasi ya chama cha upinzani kama vilivyo vyama vingine vya upinzani kwa leo, basi kitapitia madhila na nyakati ngumu kama wanavyopitia CHADEMA au ACT WAZALENDO au NCCR Mageuzi na vingine vya namna hiyo.

For instance, matokeo ya CCM kujipendelea na kutumia HILA na MABAVU kushinda uchaguzi madhara yake yalifikia kilele katika chaguzi za 2019 (uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji/mitaa na vitongoji) na 2020 (uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani)

Chaguzi hizi zote ziliporwa na CCM mchana kweupe bila aibu kwa makusudi kuanzia mchakato wake hadi matokeo yake na chenyewe kujishindisha kwa nguvu kwa karibu 99.99%.

Hii ikaleta mgogoro wa kisiasa mkubwa kwa vyama vyà upinzani vikiongozwa na CHADEMA kukataa kuyatambua matokeo yote ya chaguzi hizo na kundi kubwa la wananchi kuwaunga mkono.

Since then, serikali iliyoingia madarakani kwa hila na mabavu imekuwa ikiendesha nchi kwa mkono wa chuma kwa kulazimisha mambo huku ikiogopa na kukimbia kivuli chake yenyewe.

Mgogoro ukawa mkubwa. Na bila shaka yoyote ni kuwa, UOVU wa serikali ya CCM wa kilichoitwa "chaguzi" za 2019 na 2020 chini ya aliyekuwa Rais Hayati John P. Magufuli ndiyo chanzo hasa na halisi cha kifo chake mwenyewe aliyeamuru kufanyika kwa dhuluma hiyo ambayo ni kinyume cha haki.

Sasa tunaye mrithi wake. Huyu ni mwanamke na alikuwa makamu wa Rais na sasa ni Rais kamili. Hakupigiwa kura ila amerithi madaraka au kiti cha Urais kwa mujibu wa katiba ya JMT ya 1977.

Ni kama ana nia ya kuweka mambo sawa. Ni kama anajibu mbinyo (pressure) toka kwa makundi mbalimbali ya kijamii vikiwemo vyama vya siasa, Asasi za kiraia na kidini, vioñgozi wa dini na wananchi mmoja mmoja kuhusu madai ya umuhimu wa kuwa na KATIBA MPYÀ.

Serikali ya CCM chini ya Rais SSH ni kama kidogo inakubaliana na mbinyo huu. Lakini naona ameanza na hitaji la TUME HURU YA UCHAGUZI.

Kwangu Mimi nasema ni jema na ni mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye full national political reconciliation.

Kama nilivyosema serikali hii inaongozwa na CCM na lengo la CCM kama chama cha siasa ni kama lilivyo la CHADEMA au CUF au TADEA au UDP ya John Cheyo, yaani kushinda uchaguzi na kuunda serikali na kuongoza dola.

Of course, lengo kuu la pressure groups ni kufanya OVERHAUL ya mfumo mzima wa kisheri, kiutawala na kikatiba kwa kuandika KATIBA MPYA YA NCHI.

Lakini kama CCM wamekubali kuanza na TUME HURU YA UCHAGUZI, basi twendeni nao lakini lililo muhimu tuhakikishe njia sahihi zenye kuleta matokeo sahihi ndizo zinazotumika kuleta TUME HURU YA UCHAGUZI ambayo ni huru kwa maana ya HURU KWELIKWELI.

Kwa hiyo, nguvu ielekezwe hapo na kwa upande mwingine madai ya katiba mpya moto wake usipungue hata kidogo, uendelee kama ulivyoaanza.

SASA TUMEONA, namna mchakato wa uundwaji wa NEC HURU ulivyoanza. Ni kama kuna utani fulani vile unaendelea dhidi ya wananchi. Ni kama vile Rais SSH anafanya kwa shingo upande, kwamba ili mradi waone kuwa tumekubali.

This is wrong, tukatae na tusiukubali utani wao huu.

Kwani ni mjinga gani asiyejua kuwa hitaji la TUME HURU YA UCHAGUZI ni lazima liendane na mabadiliko ya katiba ibara ya 74 na sheria inayounda TUME YA UCHAGUZI (NEC) na ile ya kusimamia uchaguzi?

Kama kila mtu anajua na serikali inajua, ni nini role ya msajili wa vyama vya siasa kwenye hili kiasi cha mchakato kupata NEC huru uanzie kwake kwa kuunda kitu kinachoitwa "TASK FORCE" ili kupendekeza kinachoitwa namna ya kupata NEC huru.

Wote tunafahamu kuwa swàla kupatikana kwa TUME HURU YA UCHAGUZI ni swala la kisheria na kikatiba na chombo chenye jukumu la kazi hii ni bunge.

Sasa kwanini kutumia njia ndefu yenye gharama za ziada zinazoweza kuepukika huku tukitambua kuwa mwisho wa siku ni lazima turudi square one kwenye njia sahihi?

Kwanini mswaada wa mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi na ile inayounda NEC usianzie bungeni au kwa waziri na kisha uende bungeni?

Yes, we clearly know that almost 100% ya wabunge ni CCM na kwa maana hiyo possibility kubwa ni kutoleta mabadiliko yoyote ya maana.

Lakini at least tukubali kufuata utaratibu wa kisheria uliopo wa kufanya mabadiliko ya sheria zetu. Nia kama njema, hata kama wabunge wote kuwa ni wa CCM, wanaweza kuja na kitu kizuri kwani nao sheria hizo zitawahusu kesho watakapokuwa nje ya mfumo wa kiserikali

Ndiyo kusema kuwa, "labda" SSH na CCM yake wameshaukubali mbinyo (pressure) ya wananchi kutaka KATIBA MPYA lakini kwa muono wao wameanza kuwapoza watu kwa kuanza na TUME HURU YA UCHAGUZI.

Ni jambo zuri. Lakini NIA NDIYO NI YA MASHAKA kwa sababu kama LENGO jema lakini ukakosea approach yake, obviously utapata matokeo mabaya tu.

Ndivyo serikali ya CCM wanavyolitekeleza jambo hili na kwa maana hiyo haitaondoa shida bali itaendelea kwa kasi zaidi.
 
Wale wajumbe pamoja na mwenyekiti wao walitakiwa wachaguliwe na makundi mengine ya kiraia, wasio na vinasaba vya kisiasa, hao wanasiasa wanaowakilisha vyama walitakiwa wote wawe wajumbe isitokee chama kimoja kikawa na wajumbe wengi ambao muelekeo wao wa itikadi unafahamika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom