Je, CCM wamejifunza kitu kupitia uchaguzi wa Kenya?

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Wanao fikiria kuwa CCM imejifunza kitu kupitia uchaguzi mkuu wa Kenya na watakuwa tayari kufanya marekebisho ktk KATIBA mpya ili tume huru iwepo mnajidanganya.

Kuwaza hivyo ni sawa na kumchukua CHIZI pale hospitali ya Milembe kwenda kumtembeza maeneo ya chuo kikuu halafu ukamrudisha hospital ukitegemea huyo chizi ataonesha tabia njema Kama za watu alio waona chuo kikuu ukiamini kuwa atakuwa amejifunza kitu.

CCM ni waroho wa Madaraka kuliko hata nguruwe aonapo shamba la mihogo, wapo tayari kuuwa kutesa na kuangamiza ili wasaliee madarakani. Hawawezi kuachia Madaraka kwa Amani kwa kutumia makarakasi wenye Akili wajue hivyo.

Kama ktk uchunguzi wa KENYA kungekuwepo matukio Kama ya kupora wapinzani fomu, kuwateka wapinzani, kuwaua, kupitisha wagombe wa serikalli bila kupingwa, kuingia na masangunduku ya kura vituoni kutowapisha mawakala wa upinzani na Ujinga mwingine hapo tungeweza kusema kweli CCM WAMEJIFUNZA.

CCM watatoka madarakani kwa njia Ile inayo tumika pindi mtu akichomwa na mwiba au msumari. Pale mwiba au msumari ingilia ndipo hutolewa kupitia eneo Lile Lile.

CCM wamesha wapuuza wananchi wa nchi hii na kuwafanya mateka na majuha na ndio maana hawaheshimu tena uchaguzi kwa kuwa wanajua fika huwa hawachaguliwi na wananchi na kwa Sasa wanatawala kijeshi chini ya mwamvuli wa demokrasia uchwara na ubazazi.

Ni heri tuwaache CCM watawale kimabavu huku wakijua kuwa hatujawachagua na sisi tukijipanga kuwakabiri kimabavu hata Kama itachukua miaka kumi au ishirini kuwafurumusha kuliko kwenda kupoteza muda kupanga foleni kupiga kura ambayo unajua itahesabiwa na Mahela na genge lake la wanyanga'anyi na kuifanya kutokuwa na thamani.

Maendeleo hayana Vyamaa.
 
Yupo mmoja alisema wakenya Bado sana wanatakiwa waje kujifunza Kwa Mzee mafweza🤸
 
Mpk siku watanzania (wananchi) tutakapoamka ndipo ccm wataanza kuheshimu mamlaka na matakwa ya wananchi. Lkn kwa uzombi na uzumbukuku uliopo miongoni mwa watanzania hawa. CCM itatawala mpk mwisho wa dunia.

Just imagine;-
1. Mtu umejitunzia fedha zako benki eti unakatwa TOZO (siyo kodi).
2. Mtu unataka kumrushia mama/bibi ama ndugu yako mwingine unakatwa TOZO (siyo kodi).

Nchi zenye wananchi pasingekalika, pangechimbika.
 
Kwanini unataka tujifunze kupiga kura kwa kuangalia ukabila??
 
Kipo walichojifunza, nacho ni kutobadili katiba kamwe. Uchaguzi wa Kenya umewafungua macho zaidi juu ya athari ya badiliko la katiba.
Hawotokuja kukubali matokeo yaweze kupingwa mahakamani maana jinsi walivyo majizi kila siku wataishia kizimbani.

Silaha pekee waliyo nayo CCM ni katiba ya sasa na hawatokuwa tayari kuibadili labda kumwagike damu.
 
Mpk siku watanzania (wananchi) tutakapoamka ndipo ccm wataanza kuheshimu mamlaka na matakwa ya wananchi. Lkn kwa uzombi na uzumbukuku uliopo miongoni mwa watanzania hawa. CCM itatawala mpk mwisho wa dunia.

Just imagine;-
1. Mtu umejitunzia fedha zako benki eti unakatwa TOZO (siyo kodi).
2. Mtu unataka kumrushia mama/bibi ama ndugu yako mwingine unakatwa TOZO (siyo kodi).

Nchi zenye wananchi pasingekalika, pangechimbika.
Jeuri ya CCM ni upumbavu wa wananchi wa Tanzania. Tumeaminishwa sana kuwa amani ni kila kitu na kuwa ni CCM pekee ndio wanaweza tunza amani hiyo. Lakini kiuhalisia wananchi hatuna amani ya nafsi wala maisha.

Wapo watakaomka na kuiondoka CCM lakini si kizazi hiki chetu. Sisi ni mabingwa wa mikwara ya mitandaoni lakin hadharani ni kunguru wakubwa.
 
Wapo watakaomka na kuiondoka CCM lakini si kizazi hiki chetu. Sisi ni mabingwa wa mikwara ya mitandaoni lakin hadharani ni kunguru wakubwa.
Mtwara walijaribu kupinga kuhusu gesi wakapigwa mpk mashangzi zao. Mikoa mingine hatukuwasaidia.

Madaktari chini ya Ulimboka walijaribu wakaishia kung'olewa meno na kufukuzwa kazi. Makundi mengine hatukuwasaidia

Wanafunzi wa vyuo vikuu walijaribu sana miaka ya nyuma. Wakaishia kupigwa na kufukuzwa vyuo. Hatukuwasaidia.

Vyamq vya siasa (CUF, NCCR na Chadema) vilijaribu Sana kuipinga ccm. Viongozi wao wakaishia kukamatwa na kufungwa. Hatukuwasaidia.

Acha tuendelee kuumia kwa ujinga wetu
 
The Kenyan so-called Independent Electoral and Bureau Commission-IEBC entirely exposed to compromises by the politicians as every member has personal interests in its functions focusing to suffice the interests of the people of his/her favorite as it happened recently whereas the members of teh commission locked horns publicly without shame.

Tume hiyo sio huru imeundwa na wana chama wa vyama vya siasa wanaokinzana wenyewe kwa wenyewe kwamaslahi binafsi badala ya kuzingatia taalumu, kutetea sauti ya wananchi na kutokuwa mwanachama wa chama chochote; therefore no true democracy in Kenya rather there exists deceptive political game maneuverability to fool the international community for political mileage fame.
 
Mtwara walijaribu kupinga kuhusu gesi wakapigwa mpk mashangzi zao. Mikoa mingine hatukuwasaidia.

Madaktari chini ya Ulimboka walijaribu wakaishia kung'olewa meno na kufukuzwa kazi. Makundi mengine hatukuwasaidia

Wanafunzi wa vyuo vikuu walijaribu sana miaka ya nyuma. Wakaishia kupigwa na kufukuzwa vyuo. Hatukuwasaidia.

Vyamq vya siasa (CUF, NCCR na Chadema) vilijaribu Sana kuipinga ccm. Viongozi wao wakaishia kukamatwa na kufungwa. Hatukuwasaidia.

Acha tuendelee kuumia kwa ujinga wetu
CCM ina mtaji inao utumia wa mijitu mijinga na viongozi wanajua hivyo na wenye Akili timamu wachache sana tunajua hivyo.
 
CCM itafunzwa siasa na kuondolewa madarakani na kizazi cha 1980 na 2000. Hawa wazee waache waendelee kula mema ya Nchi.
 
Back
Top Bottom