Nilikuwepo Februari 1977, nilishiriki paredi ya chipukizi wa chama kipya cha CCM, wakati ule hata Mwenyekiti na viongozi wenzake hawakujivika mavazi yenye rangi kama bendera.
Leo wanafiki wanavaa hadi boxer zao ni bendera lakini ni wezi, wala rushwa, wanajilimbikizia mali na madaraka kwa njia haramu.
Chama hiki cha sasa kimefilisika sera na hoja wanaanza kurejesha uchifu na ubaguzi wa kikabila ili wajirejeshee umaarufu.
CCM imekuwa ya kuogopa kukosolewa na kujitetea kwa ni kuua upinzani/wapinzani?
Unawezaje kujinasibu kuwa unakubalika ilhali hauthubutu kujadili Katiba ya nchi au kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi?
Ndiyo maana najiuliza, Hivi CCM ile ya Wakulima na Wafanyakazi ipo au ilikufa pamoja na Azimio la Arusha?
Kwa kuwa Tanzania ni kubwa kuliko vyama, sisi Wananchi wa Tanzania tunataka kuandika Katiba yetu upya ili kuirudisha nchi kwa wenyewe kutoka mikono ya wanasiasa wanaotawala kwa utashi wao.