Je, CCM tutamkumbuka Tundu Lissu Bungeni na Mahakamani kwa hoja na akili kubwa?

Tundu Lissu kuna wakati tuliamini kama wana CCM anatumia dawa au ngekewa kutuchezesha segere na ngoma ya mpwito Bungeni na Mahakamani kumbe ni akili kubwa tu.

Kila mtu ana mapungufu yake lakini penye ukweli mabaya hujitenga, Tundu Lissu ndie mbunge na mwanasheria bora mbele za wananchi kwa muda wote (Goat) kwa kuchambua sheria, kujenga hoja na kuelimisha jamii haki zao.

Bungeni hakuna sheria wala mswada uliopita kirahisi mbele yake hata ukaletwa Ghafla na kwa dharula ndani ya siku moja, aliweza kuchambua kwa kichwa na kwa haraka kipengele kwa kipengele huku akielezea kwa undani kwa kichwa akiacha wabunge wa CCM mdomo wazi pamoja na Spika mwenyewe.

Haya mambo ya tozo Hakika angekuwepo Bungeni pangechimbika, Tundu lissu aliwaza dakika laki mbili mbele ya wabunge wenzake

Mimi binafsi aliwafanya watoto wangu wapende kuangalia Bunge na kujifunza kujiamini na kujenga hoja.

Mahakamani ilikuwa raha sana pale umuanapo na Peter Kibatala hasa kwenye kesi za kubambikia, Hakika tuliokuwa tunahudhuria mahakamani kama wana CCM moyoni tulijiuliza mengi sana, Uwezo mkubwa wa kuchambua haraka mambo ya kisheria kwa vifungu na kwa haraka mahakamani uliutoa wapi.

Pale jopo la mawakili wa serikali walipoomba wakajifikirie Tundu lissu alishapata suluhisho mbele ya Hakimu muda huo huo, Ilikuwa hakuna kulala.

Bunge Leo hii limepoa kabisa, Hakuna mtu wa kuamsha amsha kama Tundu Lissu, Sheria zinapita bila wananchi kujua, Tunashtuka Ghafla umeme tozo mara M Pesa na Tigo Pesa tozo, Tukiuliza wabunge wetu wa ccm hawana la kujibu wanasema tutaliangalia upya.

Binafsi kuna mambo ya kihistoria huwa sikuyajua lakini nilijifunza toka kwa Tundu lissu wakati wa Bunge la katiba hasa huu Muungano wetu na kitu gani kilifanyika miaka ya 1960 kuelekea uhuru na Muungano, Kidogo huwa najazia historia za mambo Haya ya Muungano toka kwa Jakaya Kikwete.
Maneno ya aina hii huwa mnayasema mara tu baada ya kutoka kwenye mfumo! Ila mkiwa ndani ya huo mfumo (wa ulaji wa ccm), huwa mnamuona Tundu Lissu kama msaliti na kibaraka wa mabeberu! Kisa tu ni mpigania haki na mtetezi wa kweli wa wanyonge.
 
Back
Top Bottom