Je, CCM Inajifunza Kutoka Kwa Hoja au Inategemea Propaganda?

Kafara

JF-Expert Member
Feb 17, 2007
1,396
411
Kutokana na hali ya kisiasa na kiuchumi inayoendelea hapa Bongo, nimejikuta nikijiuliza, "Je, inawezekana na CCM nao wanajifunza?" Swali hili limenijia baada ya kutafakari majibu yanayotolewa na CCM na serikali ya CCM kwa hoja mbalimbali zinazotolewa na wadau kuhusu mstakabali wa kisiasa na uchumi wa Tanzania.

Je, inawezekana kuwa katika kipindi chote cha utawala wake, CCM imewekeza kiasi kikubwa katika nyanja ya propaganda kuliko katika ujengaji wa hoja? Je, uwezekano huu ndio unasababisha CCM kutowaamini makada wake waliotapakaa karibu nchi nzima katika kujibu hoja mbalimbali mpaka inalazimika kutuma mawaziri?

Je, inawezekana CCM ilibweteka katika kuimarisha propaganda baada ya kubaini kwamba umma wa Watanzania unaonekana kukubali propaganda hizo? Wakati huo huo, CCM ikasahau kwamba umma wa Watanzania nao unabadilika kama jamii nyingine yoyote katika historia na hivyo kufika mahali umma huo kutaka kusikia zaidi hoja kuliko propaganda.

Kutokana na mabadiliko hayo, CCM sasa inabidi ianze kujifunza kujenga hoja zaidi kuliko propaganda. Kwa maneno mengine, CCM ni wageni katika ujenzi wa hoja na wasipojifunza kwa kasi, basi wanaweza kujikuta siku zote wanajaribu kujibu hoja za wengine mpaka 2010 na matokeo ya hali hiyo yaweza kuwa historia.

Nawasilisha.
 
Dunia imebadilika,Tanzania imebadilika lakini CCM Ilisimama haikuenda na mabadiliko yangu 2015 Ikawa inategemea nguvu za Dola na kujivunia hili,wakasahau usia wa Kikwete kuwa chama kiache kutegemea nguvu za dola kiwekeze kwenye nguvu za hoja.
Matokeo yake makada wote wakabweteka hakuna mwenye nguvu za hoja wote propagandists wasio enda na wakati, Teknolojia inawapiga teke vibaya Sana Kila wanapomaliza kudanganya wanaumbuliwa na Teknolojia kwa ufupi bado wanadanganya kizamani.
 
Back
Top Bottom