Uchaguzi 2020 Je, CCM mnajifunza lolote toka Kenya tunapoelekea kwenye Uchaguzi 2020?

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Jirani zetu wa Kenya jana wakiongozwa na Rais Uhuru Mwigai Kenyatta wamezindua report yao ya BBI(Building Bridges Initiative)kwa kusudi la kuwaunganisha Wakenya na kuondoa Ubaguzi, ukabila na vurugu za Kisiasa hasa wakti wa vipindi vya Uchaguzi.



Wakati hayo yakiendelea hapo Kenya, hapa kwetu Tanzania hali ni tofauti kabisa chini ya Utawala wa CCM ya Magufuli.

Kuna kila dalili ya Utawala wa CCM kutaka kuigawa Tanzania vipande vipande kwa misingi ya UCHAMA na Ukanda. Katika kipindi hiki cha Kampeni Utawala wa CCM umeendelea kuminya Haki, Uhuru, Demokrasia na Usawa kwenye mfumo huu wa Vyama vingi. Rais Magufuli ameonekana kuwa na CHUKI binafsi na vyama vya Upinzani kiasi cha kutaka kuwashawishi Watanzania kuwa UPINZANI NI UADUI!

ameshindwa kuiongoza Tanzania kukamilisha mchakato wa KATIBA MPYA kwa hofu ya kuporwa Mamlaka aliyonayo ambayo anayatumia vibaya kukandamiza, kunyanyasa na kujaribu kuua vyama pinzani. Magufuli kwa miaka 5 amekataa kukamilisha mchakato wa KATIBA MPYA kwa madai kuwa hicho hakikuwa kipaumbele chake alipoinga madarakani.

Sifa na heshima ya Tanzania kama Kisiwa cha Demokrasia, Amani na Umoja zimeanza kupotea hasa kipindi hichi cha utawala wa Magufuli.

Kama Watz watakosea na kumpa mitano tena, basi Hali ya Demokrasia, Uhuru na Maendeleo ya Raia Watanzania itaendelea kuwa mbaya sana!
 
CCM ni mazezeta hawajui tunahitajiana. " ...maendeleo hayana chama.....mkichagua...mtajuta.... siwafichi...mumejichelewesha wenyewe...."
 
CCM ni mazezeta hawajui tunahitajiana. " ...maendeleo hayana chama.....mkichagua...mtajuta.... siwafichi...mumejichelewesha wenyewe...."
Hapa Tanzania kikitokea chama chochote cha siasa chenye demikrasia na kisicho na ukanda ama udini, nitahama CCM
 
Back
Top Bottom