Je, CCM kuwawajibisha Mafisadi Butiama?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,039
Kingunge: Hatuendi Butiama kuomba baraka

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MWANASIASA mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru, amesema chama hicho hakiendi Butiama kufanya mkutano mkuu kwa lengo la kupata baraka za hayati Mwalimu Nyerere.
Akizungumza na gazeti hili, hivi karibuni kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, alisema suala la kupata baraka za Mwalimu halifanikiwi kwa kwenda Butiama, isipokuwa hiyo ni moja ya taratibu za CCM kuzunguka mikoani wakati wa mikutano yake.

“Ni maneno ya mitaani, sisi hatuendi Butiama kwa lengo la kutaka baraka za hayati Mwalimu Nyerere wala kuwawajibisha wanachama wanaosemekana kushiriki katika ufisadi, bali tumeamua kurudisha utaratibu wa zamani wa kuzunguka mikoani kwa mujibu wa CCM,” alisema Kingunge.

Alisema, utaratibu wa kufanya mkutano mkuu katika sehemu mbalimbali si jambo jipya na kwamba, ulikuwapo tangu enzi za TANU, lakini kutokana na sababu za kifedha haukuendelea.

Alibainisha kuwa, utaratibu huo unawapa nafasi wajumbe wa mkutano huo kufahamu mazingira ya sehemu husika, kwani hupata nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali kabla ya kuanza kwa mkutano.

Kuhusu kuwashughulikia wanaotuhumiwa ufisadi, alisema Kamati ya Maadili ya CCM ndiyo chombo chenye kurekebisha na kuwawajibisha wanachama ambao watabainika kwenda kinyume cha maadili.

“Kupotoka kwa maadili ndani ya CCM si jambo geni, kwani kila sehemu yenye mkusanyiko wa watu kunakuwa na watu wenye tabia tofauti, lakini muhimu zaidi ni kuwepo na vyombo vya kuwawajibisha waliopotoka,” alisema Kingunge.

Mkutano Mkuu wa CCM unatarajia kukutana Machi 29, mwaka huu, Butiama kwenye kijiji alichozaliwa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere kujadili masuala mbalimbali ya chama hicho.Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 10 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
KUFANYA TOBA YA KWELI WAKATI MTU ANAPOGUNDUA KUWA AMEKOSEA NI SEHEMU YA UUNGWANA. KWA HIYO KAMA KWELI KUNA MPANGO WA KUJIRUDI NA KUFANYA TOBA, HILO SI JAMBO BAYA. ILI MRADI WANATUBU KWA MUNGU NA SI KWA MTU, HALAFU WANAWAOMBA SAMAHANI WALIOWAUMIZA. HUU NI USTAARABU. WAKIANZA KUUJENGA, NI FARAJEA KWA NCHI.

na Jickymm, UK, - 21.03.08 @ 02:57 | #3108

Jamani, kuna mtu anaweza kumfunga kinywa huyu mzee.. sasa watu wakiwajibishwa kule Butiama, yeye atamung'unya nini?na Mwanakijiji, US, - 21.03.08 @ 09:01 | #3117

We kingunge acha porojo za kisiasa,hii nchi inamatatizo mengi sana na waliyoifikisha hapa ni pamoja na wewe,kumbukeni malipo ni hapa duniani kwani machungu wanayopata Wa-Bongo zaidi ya milion 30 ni makali sana hivyo ni vema mkafanya toba ya kweli na si kujikosha kwenye vyombo vya habari,

Nani asiyejua kama wewe ndo ulimshauri rais kuunda Baraza la mafisadi kwa kisingizio cha mtandao?sasa mambo hayaendi Mungu anawaumbua ndo mnamtafuta Marehemu baba wa Taifa,kama ni kuzunguka mikoani kwanini msianzie Kigoma au Tabora?acha porojo mzee

na DANNY, kenya, - 21.03.08 @ 09:34 | #3122

Kingunge ingekuwa ni utaratibu wa kuzungukia mikoa mgeanzia Lindi ili Kikwete akampe pole mkwewe kwa yaliyomsibu alipokuwa anakwenda Hijja!! Mzee acha fiksi zako umeishakuwa mtu mzima unatakiwa uwaambie vijana ukweli!!

na Ngwada, Iringa, - 21.03.08 @ 10:48 | #3130

we mzee kingunge si mstaarabu,kwani kwenda kuomba msamaha ni tatizo ni jambo la kawaida,ila sio ishu wenyewe mnajua mnaenda kufanya nini,ila huyo marehemu mwalimu kweli anaweza kuwapa msamaha kwa yote yale mliyofanya,na km kweli msamaha huo utafanya kazi basi mi sitakua na imani tena na waliotutangulia mana ccm mmewaasi wananchi wa tz na kuwakumbatia watu wa nje wakina rostam,dewji,na wazungu wengi ambao mnawaita wawekezaji.

na mstari wa mbele, calif/usa, - 21.03.08 @ 09:02 | #3132

Mzee kingunge kwanza ungekuwa na busara kwa sasa ulitakiwa unyamaze kabisa kwani ni wewe pamoja na wenzako ndio mmetufikisha hapa tulipo kwa kupenda rushwa watu wengi waliok madarakani mmewatetea baada ya kuwa wamewahonga hayo yote yanajulikana ulishindwa kumshauri rais kwa ukweli kuteua viongozi mlichokuwa mnaangalia ni wanamtandao siku zitafika lazima mtalipa jifunzeni kutokana na migogoro ya nchi zingine mtaachia familia zenu taabu na mashaka mambo mengi mliyoyafanya baba wa taifa alikataa wakati wa uhai wake alipofariki ndio mkapata nafasi wewe kingunge na wenzako siku zinakuja lazima mlipe wewe mwenyewe mkeo anafanya biashara kwa kutumia chama hayo yote yanajulikana mzee

na ngeli maazan, DSM, - 21.03.08 @ 12:16 | #3150

MZEE KINGUNGE UMEYASAHAU MANENO YA JK NYERERE?? (USISUBIRI MPAKA UKANGAKULIWA WAKATI UMESHAFIKA NGAKUKA ULE MAZAO ULIYOCHUMA)WAKATI WAKO UMESHAPITWA

na Andrew, Tanzania, - 21.03.08 @ 13:46 | #3155

Mzee Kingunge,jickmm kaongea vema,nadhani ungetangulia kusema kuwa huu ni mda wa toba ya dhati. Pale kizita juzi mwenyekt wako alizima upuuzi wa mafisad,eti chakula cha jioni. Wote huo ni uovu aliunyamazisha na mnao hao watu ndan ya ccm. Hiyo TANU unayosema ilifikia hatua tuionayo? Sikuwepo,lkn baadh ya vitabu nikisoma naona viongozi bora ndani ya TANU. Usitungushe mzee, nenden kwa mwl akawakumbushe maana alifundisha vya kutosha. Vipi mzee,au unadhan propaganda unazijua alone? Nakuomba kwenye mambo ya mcingi ukubali tu. Mapinduzi ya chama yalilenga kutetea utu siyo MAFISADI.

na kulata, tz, - 21.03.08 @ 15:23 | #3161

Angalau Mzee Kingunge ameweza kusema ukweli, ingawa anaweza kuwa amefanya hivyo bila kujua!!

Ni kweli utaratibu wa kuzungusha vikao mikoani ulikuwepo lakini ulisitishwa kutokana na ukosefu wa fedha. Hapo tuko pamoja.

Sasa wameamua kuurudisha kwa sababu ukosefu huo umekwisha, maana sasa Chama kina fedha nyingi inayotokana na ufisadi. Asante Mzee wetu. Kwetu kuna msemo kwamba siri ikifika kwa Mzee sana kijijini basi hiyo si siri tena.

Na kuna ukweli ndani yake. Sitashangaa kusikia kwamba CCM ina pesa kuliko Labour Party na Conservative Party vya Uingereza!! (Rejea Deep Green, Mahindra cars, etc, etc, etc)

Wahenga walisema unaweza kuiba kadri ya uwezo wako na ukajificha unavyoweza, lakini ukumbuke vilevile kwamba za ***** ni arobaini! CCM nao wasitegemee Mungu awapendelee na kuwapatia 41, 42 n.k. Ni 40 tu!!

na Amk, dar, - 21.03.08 @ 15:25 | #3162

Mtu yeyote mwenye akili anajua kuwa CCM wanakwenda kujikosha Butiama kama ilivyo kawaida yao. CCM ni mafundi wa kutumia jina la Mwalimu ili wapate wanachotaka bila hata kujali hali ya familia ya mwalimu.Inashangaza kuona mafisadi wote wanafaidi na kutamba kwa kutumia jina la mwalimu Nyerere wakati Serikali imepuuza hata kufuatilia jinsi gani wajukuu za mwalimu watasoma. Tunafahamu wajukuu wa Nyerere ambao wako Marekani na Tanzania wamekosa ada ya shule. Kweli Serikali haioni aibu wakizingatia yote aliyoyafanya nchini,nani asiyejua kuwa bila ya nyerere hawa mafisadi wote wangekuwa hawatambi. Tena hawa hawa mafisadi ndio wameidharau familia ya mwalimu kwa kuwa mwalimu hakuwa na mali mpaka alipoaga dunia. Hii ni kwa sababu alikuwa mwaminifu.Kwani nyinyi mawaziri ambao mna utajiriwa mpaka kuwahamisha watoto wenu na kuwafadhili nchini kama Marekani mishahara yenu ni kiasi gani? Mbona mwalimu Nyerere hakuwa na utajiri wowote pamoja na kwamba alikuwa Rais.Mimi ushauri wangu ni kwako Rais Kikwete ,achana na ushauri unaoupata kutoka kwa Mafisadi wako, kumbuka uliko toka bila Nyerere usingekuwa madarakani.Pengine hufahamu hali halisi ya familia ya mwalimu wajukuu wake hawana uwezo wa kusoma kwa sababu familia haina uwezo.Kumbuka kuwa ukitaka kummaliza mtu mnyime elimu. Hiki ndicho kitakachotokea kwenye familia ya Nyerere, familia itafutika baada ya muda si mrefu kwa kukosa Elimu.Inasikitisha kuona serikali haina utaratibu wowote wa kuwaendeleza watoto na wajukuu wa Nyerere.Hivi mkienda Butiama mnajadili mambo gani muhimu wakati wajukuu wa nyumba hiyo mmewaacha Dar wanahangaika wakiomba omba kwa marafiki ili wawalipie ada ya shule.Kuna wenzao wengi wako hapa Marekani pia wanahangaika na kuchekwa na wala watoto wa mafisadi waliojilimbikizia mabilioni na ndiyo maana hawana tatizo la ada ya shule wala pesa za matanuzi ya kila aina.

na Abdallah Ncho, USA, - 21.03.08 @ 17:21 | #3173

 
Je kuna yeyote amewajibishwa au mambo ni shwari na hakuna hata moja lilosemwa likafanyika ???
 
Back
Top Bottom