Je CCM kuondolewa madarakani ni maslahi "ya taifa"? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je CCM kuondolewa madarakani ni maslahi "ya taifa"?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 7, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [h=6]Maslahi ya taifa ni nini basi? ni kwa CCM kuondolewa madarakani na sera na mifuko yake iliyotufikisha hapa kuvunjwavunjwa na kutupiliwa mbali kwenye shimo la usahaulifu la historia. SIYO maslahi ya taifa kuona CCM inajaribu tena kutawala vizuri. Mpinzani anayejaribu kuisaidia CCM 'ijitahidi' au itawale vizuri kwa sababu ni 'maslahi ya taifa' sidhani kama ameelewa vizuri dhana hii ya 'maslahi ya taifa'. It is to the interest of the nation for CCM to be removed from power; nothing more, nothing less.[/h]
  Maslahi ya taifa ni zaidi ya watu kujitahidi kutawala vizuri; ni watu sahihi kutawala vizuri. Ni makosa makubwa kufikiria kuwa CCM sasa hivi inaweza kutawala vizuri zaidi ya ambavyo imekwishatawala kwa miaka hamsini iliyopita. Swali hata hivyo ambalo litapaswa kujibiwa ni je CCM inaweza kutumainiwa kuleta utawala bora miaka miwili na nusu iliyobakia? Je yawezekana kweli CCM ikabadili sera zake zilizoshindwa na ikaanza kuja na sera mpya ambazo zikabadilika the trajectory of leadership in the country?

  Je CHADEMA inaweza kutoa ushauri mzuri kwa CCM kuweza kutawala vizuri halafu CDM ifurahie kuwa "tumeisaidia serikali na sasa inatawala vizuri"? Je, ni maslahi gani CDM au chama kingine chochote cha upinzani inayo kwa CCM kujaribu kutawala vizuri zaidi? Je siyo maslahi ya chama cha upinzani kuidhoofisha serikali ya chama tawala iliwa wananchi waikatae?
   
 2. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,371
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA na itakuwa bora zaidi kwani tutakuwa tumejifunza through CCM's mistakes.
   
 3. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,786
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Ili isionekane kuwa Vyama vya upinzani ndivyo vinavyosababisha serikali iliyopo madarakani inashidwa kufanya kazi yake ya kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo kutokana na hujuma za vyama hivyo. Napendekeza itumike lugha hii " Je siyo maslahi ya chama cha upinzani kuonyesha uovu/ubovu wa kiutendaje wa serikali ya chama tawala kwa raia ili chama tawala kikataliwe na wananchi?

  Kudhoofisha nahisi simahala pake hapa, maana watu waweza kuwaza kuwa Chama Tawala kinafanya vizuri kuleta maendeleo lakini wapinzani (vyama vya upinzani) ndiyo wanaharibu(dhoofisha) juhudi hizo.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  CHADEMA has no business counseling CCM. CHADEMA should keep on hoping that CCM fails miserably if they want to get elected into power.
   
 5. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nashindwa kuelewa kwanini hatuja capitalize vizuri kwenye suala la Baraza la mawaziri na mafyongo yake yote.
  UTAIFA mbele ni kuisulubisha CCM to the core
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mzee kati ya vitu vinavyonikera ni hivyo. Wapo watu wa CDM na hata wapinzani wengine ambao wanajitahidi kuishauri CCM ifanye nini ili 'nchi itawalike vizuri' matokeo yake wanajikuta kimsingi hawataki CCM iondolewe madarakani bali iboreshwe tu kwa ajili ya maslahi ya taifa.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Lakini siyo wote wanaamini Tanzania bila CCM inawezekana!
   
 8. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu, jibu rahisi kwa hayo maswali yako yote mawili ni kuwamba, HAIWEZEKANI. Kwa hiyo maslahi yoyote ya taifa LAZIMA yalenge kuiondoa ccm madarakani.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Lakini yawezekana wapo watu ambao wanaona kuiondoa CCM madarakani ni kama uhaini au usaliti fulani vile; kwao Tanzania bila CCM haiwezekani.
   
 10. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hao watu ni wachovu wa kufikiri. Tanzania bila ccm inawezekana kabisa. Sisi wananchi tuna haki kabisa ya kuiondoa ccm madarakani, na tutaiondoa.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji haya ndio makosa makubwa ya wanasiasa wetu wanaojaribu sana kuishauri CCM ifanye kadha wakadhaa kama vile wao CCM hawajui wanachokifanya. Siku zote mtu yeyote mwanasiasa unapokuwa chama cha Upinzani ni kwa sababu unaitaka nafasi ya wewe kuongoza nchi na unajua fika kwamba sera zako ndizo bora zaidi ya mtawala, sasa kama ni swala la kushauri basi hapakuwepo na sababu ya ushindani maana ushauri hata hao CCM waliopo madarakani wanapewa ushauri juu ya sera zao na unaweza hamia huko ukautoa ushauri vizuri zaidi.

  Kinachonishanga sana Tz ni pale Mbunge wa Upinzani au mwanasiasa anayepingana na itikadi pamoja na sera za CCM anapojaribu kuishauri CCM ifanye vizuri wakati kisiasa kila mpinzani hutaka chama tawala kishindwe na kuonyesha udhaifu wake kwa wananchi na hapo ndipo unapopigilia msumari. Siasa ni mchezo mchafu sana na ukitaka kuufanya Netball au Volleyball mchezo wa usiniguse, basi hizo sio siasa hata kidogo japokuwa hutakiwi kujenga chuki na uadui hata kidogo..

  Maslahi ya Taifa ndiyo yaliyojenga Upinzani ni philosophic skepticism wa itikadi na sera za mtawala hata kama anafanya vizuri wewe utadai ungefanya vizuri zaidi kwa kutumia itikadi na sera zako. Ila unaweza kumsifia mtu wa upande wa pili alofanya jambo zuri (haki yake unampa kama binadamu) lakini kamwe sio itikadi na sera wala kumshauri ila unaweza jenga bipartisan policy na wakichukua tu zenu mnajitapa.
   
 12. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani nini wananchi wanachotaka?

  Kwani wananchi wanataka chama au maisha yenye haki,usawa,na uadilifu.

  Kwa taarifa yako mwanakijiji, wananchi hawataki chama, chama chochote so long kinawapatia wananchi kile

  wananchokitaka basi ni sahihi kutawala! Kukubaliana na kupingana katika siasa kwa lengo la kuwatumikia wananchi ndio

  lengo la hivi vyama sio chuki na kupinga kila linaloanzishwa na upande wa pili.

  CCM kuondolewa madarakani (ambayo ni ndoto) ni kwa maslah ya taifa only if wanaowaondoa watatekeleza kile

  walichokiahidi, kwa TZ hakuna chama mbadala wa CCM kama alivyosema Bana, hao opposition wapo disorganized,

  hawana malengo yanayofanaa na ndio maana kila wasimamapo majukwaani wanatoa maneno yenye contradiction.

  Its log way to go.
   
 13. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkandara ndugu yangu leo umepotoka,

  Kama hayo unayoyasema ndio malengo ya vyama vya upinzani, basi milele wananchi hawatokuja wapate maendeleo,

  masikini na walalahoi watateseka sana maana mtakachokifanya ni kushauri vibaya kwa lengo la kuharibu ambapo waathirika wakuu ni

  wananchi ili wakichukie chama tawala. Kama hivyo ndio basi hata nyie mkiingia madarakani itakuwa zamu ya kile chama kingine kufanya

  fitna, na mwisho wake watakao umia ni wananchi.

  Labda nikuulize swali: Kwani upinzani hawawezi kujena trust kwa kule kushauri kwao vyema na wakakubalika? kiasi cha kuaminiwa kupewa dola?

  Mkandara kaka yangu leo umechemka sana.
   
Loading...