Je CCM inapima mgombea wa uchaguzi ujao? Au wame-panic na upinzani?

Profesa

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
905
624
Mkutano huu sioni kama una mantiki kubwa kama nilivyotarajia, zaidi ya kile nilichosema awali, show-off dhidi ya CHADEMA, na kukurupuka pale unaposikia hoja za upinzani kiasi cha kuji-contradict wenyewe. Sasa hapa sijajua kampeni za uchaguzi ndio zimeanza au?

Kwanza niwaambie, watu wanaimini CCM ila tabia zenu viongozi ni mbovu kiasi cha kushindwa hata kujipima, na hamtaki kukosolewa, kiasi sasa watu wako tayari wanede kwenye chama chochote kutafuta matumaini. Hivyo CCM haiaminiki kwasababu ya viongozi wake sio chama chenyewe.

Uwiano wa mafanikio una kasoro kubwa sana utaeleweka kwa mtu ambaye hajaenda shule ila ukintajia idadi ya infrustructures, au idadi ya wanafunzi au vyuo ni lazima ueleze kulingana na idadi ya watu an ukubwa wa nchi, zaidi ya hapo ni kuwa wewe kama kiongozi unaamini unaowahutubia ni mambumbu so nani yuko hapo uwanjani ukiacha viongozi? Je ndio maana hamtaki kuwekeza kwenye elimu na vyuo na utafiti badala yake mnawekeza kwenye yale yatakayowaweka madarakani milele ikiwemo vyombo vya dola na siasa zenu? Huku mkihakikisha no critical mind emerge or prosper, ikiwemo kupuuzia kudumisha ubora wa elimu badala yake mnatudanganya na quantity!!! Unaweza kulinganisha Tanzania na Burundi kwa wingi wa barabara dah!

Ninachokiona ni kueleza serikali imefanya nini.... simply a typicle order from JK, sababu ndio stile yake ya hotuba habadiliki... angalau Mwakyembe ingawa nae sehemu kubwa pia alinasa kwenye mtego maana lazima atekeleze maamuzi ya mkutano wa maandalizi., Magufuli ndio kabisaaa kama mtu anaelinda nafasi ya Uwaziri.

Nataka kusikia miaka 50 ijayo Tanzania itafananaje, ili tuwabakize mtekeleze... hizi siku mbili zijazo mnatufanya tuendelee kuganga njaa kisa mnagombania kura wala hamjali nchi hii itafananaje huko mbeleni.

Hivi mkutano wa siasa ni lazima ugharamie watu kuja? Hii siyo rushwa? Je kama unaamini CCM ina mvuto ni kwanini msifanye kama vyama vingine watu wanakuja wenyewe uwanjani? na hoja kuwa mna pesa? Dah, ni kauli mbovu na mbaya kuliko zote mbele ya kadamnasi ya wengi wasiokuwa na uhakika wa maisha. Haya na mengine yatawamaliza, mmevimbiwa hamuwajui wenye njaa.

Dah ma-engeneers wa Siasa wako wapi? Vipi sikuizi hampeleki watu kusomea political engeneering Bulgaria na Cuba? Maana wale waliofuzu najua wengi ni wale waliosoma wakati wa vita baridi.
 
Back
Top Bottom