Je, CCM ina mkono katika Kamati ya Maadili ya Mawakili?

PhD PM

Senior Member
Apr 29, 2019
112
250
Tanzania ni nchi huru yenye mihimili 3. Bunge, Mahakama, na Utawala. Hivi karibuni tumeona mihili hii isivyo na nguvu na mhimili mmoja kuendesha mihimili mingine. Mf. Bunge kuendeshwa na Serikali. Mf. Chunguzi za Kamati za Bunge kuwasilishwa nje ya Bunge, yaani Ikulu (e.g. makinikia). Rais kutumia pesa nje ya Budget kuu nk (Chato Airport). Hizi mifano ni michache snaaa. Rais alifikia hatua ya kutamka "kuna mhimili 1 umejishindilia zaidi Ardhini" kwani ndio una lipa mihimili mingine! Kuna vitendo vya Rais kuagiza Hakimu flani aondolewe na Hakimu flani apande cheo (yule wa kesi ya Sugu).

Binafsi Bunge nilisha liondoa ktk Mihimili huru. Kijana mdogo asiye na mbele wala nyuma (Nape Nnauye) kuondoa Bunge Live kwa maslahi ya CCM. Inaonesha Bunge lilivyo dhaifu. Kitendo cha kufukuza watumishi 17,000 wa mishahara ya 300,000 na kurudisha wabunge hewa 19 wa mishahara mil 12+ kwa mwezi. Magari, mikopo, nk. Na Pension ya Mill 500 baada ya miaka 5 ina onesha jinsi Bunge lilivyodhaifu!

Ilibakia mhimili 1 wa Mahakama. Japo malalamishi ya kuonewa wapinzani ni mengi sana. Kesi za T. Lissu, kesi ya Akwilina (Mbowe, Mnyika, Mashinji, nk), kesi ya Lipumba vs Maalim Seif (J. Mtatiro). Kunyimwa dhamana kwa Wapinzani kwa makosa yenye dhamana, nk. Uta ona hili Gazeti la Tanzanite lina andika Vifo vya mbowe na Mrema au UVCCM kudai ni haki ya T. Lissu kupigwa Risasi, au ulipona ila awamu hii tutakumaliza kwa Sindano ya sumu, au kijana wa CCM kutishia mtu uhai mtandaoni kisa kutofautiana mitazamo kwa sasa ni jambo la kawaida sana na hafanywi chochote. Wadau visa na mikasa ni mingi ya Police, Mahakama na Msajili wa vyama vya siasa.

Takribani wiki 3 zimepita Tagu Ndg. Hamphrey Polepole (Katibu Mwenezi CCM Taifa) asifie Rais kwa Uteuzi wa Jaji wa Kamati ya Maadaili ya mawakili. Akaenda mbali zaidi na kumsifia Jaji huyo. Akisema mawakili wasiowazalendo wafutiwe UWAKILI. Leo tunaona shawiba wa H. Polepole (Dr. Bashiru) akiteuliwa kiwa Katibu Kiongozi! Ina maana CCM na serikali ni kurwa na doto! Je maneno ya H. Polepole hayawezi influence utendaji wa Kamati hii? Shida ktk Tz yetu kwa sasa ni tafasri ya neno MZALENDO ni nani? Mtetezi wa wanyonge kwa sasa anaitwa msaliti, kibaraka wa mabeberu, Shoga, nk. Nidhihaka na tafrani tupu nchini.

Leo tarehe 15/03/2021 Kamati ya Maadili ya Mawakili ime waandikia wito Mawakili Jebra Kambole na Edson Kilatu kujadiliwa ikiwemo kusimamishwa au kufukitiwa leseni zao za Uwakili. Japo imesogezwa mbele kidogo kusoma upepo.

Ndg zangu Watanzania (CCM na wa upinzani) tukemee huu UDIKTETA! Wanyonge tutakosa watetezi! Nchi hii kwa sasa inaskitisha! Watawala mnako tupeleka siyo. Itafikia hatua tutanza visasi nyumba kwa nyumba, raia mmoja mmoja na polisi, tutazikana kwa visasi, nk.

CCM ina uzoefu wa kuongoza nchi toka 1961 (TANU). CCM imeshinda Serikali za mitaa 99.99%, Madiwani 99.98%, Wabunge 99.99%, Rais 100%. Why muingize mitutu, ubabe, vitisho, nguvu kibao kwa ushindi huo? Yaani nchi nzima inyamaze kama maji ya dimbwi? Msiogope kukoselewa. Hoja mbadala hujenga demokrasia ya nchi. Ukikosolewa unajua Mapungufu yako. Una jirekebisha.

Tuipende nchi yetu ila tusitetee kila uovu!
 

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,205
2,000
Mm nashauri tu ukitaka mabadiliko nchi hii hakikisha kipato chako watu hawakijui vizur hapa nacho kiona washamsoma jebra kambole ugal wake unapitia uwakili so wanakata mirija ili uteseke

DUME LA NYANI HALIOGOPI UMANDE
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom