Je CCM Imekodi wazungu wa Finland Kumchafua Dr.Slaa?

Wana JF kwa ulewa wangu kidogo wa mawasiliano ya simu za mkononi ni kwamba mtu ye yote ambae anataka kutangaza/kusambaza ujumbe wo wote (wa kheri/kibiashara kwa wote wenye simu za kampuni fulani) anaweza akakubaliana na kampuni husika na wakiridhika na kulipwa wakautuma wao (kampuni ya simu) na nadhan TCRA pia wanaweza kumpatia mtu au kampuni ikatuma ujumbe -. Nilipata ujumbe kutoka TAKUKURU wiki kama 3-4 zilizopita na nadhani walifuata utaratibu kama huo hapo juu. LOGICALL then ni kwamba mkuu wa kaya na watu wake wametumia mbinu hizo na kuweza kusambaza ujumbe mbovu/mchafu. wasitake kutufanya wajinga eti wanachunguza! wanajua chanzo na lengo ILA lengo lao halitofanikiwa kwani watanzania walio wengi sasa hatudanganyiki.
 
Hakuna cha wazungu wa Finland wala nini. Hawa ni watanzania kama sisi ambao bado wana mawazo mgando ya kuamini kuwa ni wenyewe peke yao wenye haki ya kuwaongoza watanzania wengine.

Muda si mrefu mtawajua ni akina nani waliotuma sms hizo.
 
Ndugu yangu ni uongo mtupu, namba sio ya Finland. Imetengenezwa hapa hapa nchini. Mi nimewahi kuwa Finland na namba za kule ni kama za huku kwetu kwa maana kwamba baada ya code number, kunakuwa na tarakimu zingine tisa (kama huku kwetu). Kwa mfano naomba nikupe namba ya rafiki yangu wa Finland (nimemuomba kufanya hivyo ili kuondoa utata), ambayo hata ukiipiga sasa hivi inaita; +358 407 450 963. Anatumia Mtandao wa Telefinland, na mitandao yote kule ina tarakimu idadi sawa na hizo.

Kwa hiyo hii wanayotumia CCM ni geresha, imetengenezwa hapahapa na ukiipiga unaambiwa haipo.... We unatumia mtandao gani?
Hiyo namba si ya mkononi bali ya mezani. Kuna simu za mezani ambazo unaweza kupokea na kutuma sms!! Ni kweli simu za mkononi Finland zinaanzia 40... na 50... Kwa vigezo hivi haifuti ukweli kuwa simu inatoka Finland. Vema serikali ya Finland ikaingilia hili kwani inachafua hadhi yao na kuwaweka katika hali ya kukosa usalama kimtandao iwapo mtu amefyongoa country code yao.
 
Jana wakati nimekaa sina hili wala lile ikaingia sms katika kibofya changu toka katika namba '+3588108226' ikisema,'SLAA NI MROPOKAJI NA MGOMVI ANATUKANA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.ANATAKA DAMU IMWAGIKE ILI MRADI AINGIE IKULU.TUMKATALIE KUIGEUZA NCHI YETU SOMALIA'. Baada ya kusoma sms hii nilighafilika sana.Kwa harakaharaka nilijua aliyeituma ni Mpumbavu,Muoga,hana uwezo wa kufikiri au ametoroka hospitali ya vichaa japo nachua chama anachotokea.Nilipojaribu kuipiga namba hii wala kuijibu sms nikashindwa.Namba hii baadae niligundua ni Code ya Finland katika mji uitwao Oulu Swali hapa ni kuwa Je CCM Imekodi Wazungu wa Kumchafua Dr. Slaa?
Ninazo sababu nyingi za kumuita mtuma sms mjinga,myoga au Mpunbavu na Punguani,Kwanza kabisa;
KUMWITA SLAA MROPOKAJI NA MGOMVI
Ni mropokaji huyuhuyu ndiye aliyeweza kufichua kashfa kibao za Ufisadi ambazo wabunge kibao 'Mabubu' Waliogopa Kuropoka. Matokea ya kuropoka kwake tukayaona,Akina Lowasa wakawajibika. Angalau tukaona kesi kadhaa Japo za 'Vimeo vya ufisadi'.Tunamtaka huyu huyu 'MROPOKAJI' awe Raisi wetu...awaseme watendaji wasiotimiza wajibu wao.Tunamtaka Huyuhuyu 'Mgomvi' ambaye akiwaambia watu wasiotimiza wajibu wao Ukweli anaonekana Mgomvi...Mimi huyuhuyu Mropokaji na Mgomvi ndiye RAIS WANGU!

SLAA KUTUKANA VYOMBO VYA USALAMA
Nani asiyeona vyombo vya Usalama vinavyoibeba CCM? Nani asiyeona Upendeleo wa Wazi ? Nani asiyeona Ulinzi anaopewa Salma Kikwete? Kwa Nini Mke Wa Lipumba na wake wa Wagombea wengine wa Urais hawapewi ulinzi ili wawapigie kampeni waume zao? Kwa hili Mtuma Message ni Punguani. Kwa hiyo alitaka Slaa avisifu vyombo vya Ulinzi kwa kuipendelea CCM? Nnachomwomba Slaa...Endelea Hivyo hivyo Rais wangu.Asiyewajibika na kutenda haki mpe 'DOZI' yake hapohapo

ATI SLAA ANATAKA DAMU IMWAGIKE ILI AINGIE IKULU
Kweli mtuma sms ni Mtumwa wa Kiakili ama hajasoma au nikichaa. Nani alikuambia Demokrasia ina vunja Amani. Hebu angalia Marekani enzi za Kampeni za Kina Obama.. Damu ilimwagika? Najua atasingizia Kenya au Zanzibar Miaka ya Nyuma pasipo kujua kuwa 'DAMU HUMWAGIKA HAKI IKIPINDISHWA NA KURA KUIBIWA!! Nani asiyejua kuwa Raila Odinga aliibiwa kura? Nani asiyejua kuwa Maalim Seif aliibiwa kura na Kudhulumiwa Urais.....Namtahadharisha mtuma sms kuwa iwapo Chama chake kitaiba Kura na Kumdhulumu Slaa haki ya kuwa Rais inawezekana kweli Damu Ikamwagika.. Sipendi Tufike Huko kwa kumwagika Damu.. Kimsingi nnachosema ni Kuwa HAKI Ikitendeka siku zote Hakuna damu inayomwagika. Labda sijamwelewa mtuma sms..Ana maana Slaa akiiingia Ikulu Damu Inamwagika? Ina maana Chama cha mtuma sms (CCM) Kimejiandaa kumwaga Damu Slaa akiingia Ikulu??? Kwani Nchi Hii ni ya CCM?
Ndiyo maana nikamwita mtuma sms kuwa ni Punguani na Mtumwa wa Mawazo .Watu kama hawa ni Pazia la kukua kwa Demokrasia...Hawatakiwi nchi hii.

ETI SLAA ATAGEUZA NCHI KUWA SOMALIA
Kuna watu humu Duniani wanahitaji Kufanyiwa Neurological Surgery. Huyu Jamaa hajui hata Historia ya Somalia. Hajui Hata Historia ya Tanzania. Hajui kwa nini Tanzania haiwezi kuwa na machafuka kama Somalia. Naomba arudi Darasani akasome historia vizuri.

HITIMISHO
Ni vema tusianze kuwatisha watanzania kupitia Sms na badala yake tuwaeleze Sera za vyama vyetu na jinsi ya kuzitekeleza na siyo kutuma sms zenye kuwaponda wagombea, Kwa mfano mtuma sms alidhani ameikampenia CCM kumbe ndiyo ameipunguzia CCM Kura yangu.
Watanzania Tuache Uoga na tuachane na Vitisho.
Ni KAMA VILE WATU WANAVYOSEMA ELIMU BURE KWA WOTE HAIWEZEKANI?? Nakumbuka Profesa wangu alinifundisha kuwa 'FEAR OF FAILURE IS A FAILURE ITSELF'
Watu wanaogopa na hawasomi SERA Vizuri..Tuanze Kubadilika mawazo na Kuamini kuwa kila kitu Kinawezekana. Mbona Tunaamini kuwa 'TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA? Wakati tunajua Ukimwi ni Chronic Infection na Kwamba ili tuwe na Tanzania Isiyo na Ukimwi ni Lazima Wagonjwa wote wa Ukimwi wauwawe?.. Lakini Bado Tunaamini tu Kuwa Tanzania Bila Ukimwi Inawezekana..Tena tunasimama na Kuimba Majukwaaani....Tanzania Bila UKIMWI Inawezekana!!!! Sasa kama Tanzania bila Ukimwi Inawezekana na tuna Mamililioni ya Wagonjwa wa Ukimwi na wengine maelfu wanaambukizwa kila siku na bado tunasema Bila Ukimwi inawezekana.. Je Kama Rasilimali zetu na Mafedha kibao yanayotumika Bungeni na Matumizi feki ya Serikali yakidhibitiwa hatuwezi Kuwa na ELIMU BURE KWA WOTE?
Kila Mtanzania achambue Sera na aepuke Propaganda za Mapunguani
wachache wanaotaka kuogopesha wengine



Kwani huko finland hakuna watanzania?, mzungu gani atazungumza ujinga huo?
 
Mzungy hawezi mchafua Dr.W.Slaa rejea mapokezi ya kihsoria aliyofanyiwa ndani ya aridhi ya america.
Wakamtangaza km mtu anaemkaribia hayati nelson mandela kwa uongozi wa kisiasa,japo kuna viongoz wengne kila week wapo kule wanaishia kusubiriwa na mabalozi tu
huyo atakuwa w.ngeleja katuma,maana nilisikia yupo nch za scanavia
 
Last edited by a moderator:
Dk wilbroad slaa ni chaguo la watanzania.hakuna shaka kuwa anawaumiza kichwa wapenda dhuruma na chama cbao chakavu.2015 lazima kielewekeb
 
Niko hapa finland na hiyo number ni ya kampuni inayoitwa sonera au dna ngoja niwaambie wabongo furani hapa ili tuanze kumtafuta ni nani.kulikuwa na madiwani kutoka majimbo huko tanzania na inawezekana kuna jamaa mmoja ccm jina ngoja kidogo utafiti
 
Hiyo number imefungwa lakini nitakwenda kuchukua form na nitajaza kisha nitawapa number na wataiproces kisha atajulikana kana alinunu R.kiosk au laa kitu simple
 
Sio lazima sms iwe imetokea finland mkuuu,siku izi teknolojia yaweza fanikisha utengenezaji na utumaji sms ikaonekana imetoka sehem yoyote na namba yoyote duniani,zaidi kasome spoofsms.com
 
Kwikwi we ni mgeni wa teknolojia.... hiyo SMS kuna uwezekano wametengeneza wenyewe il I kumpaisha tuu Slaa maana hata Yericko alisha sema umaarufu wake umeporomoka .

Hiyo sms ina Ukweli
Muulize Slaa kama lile kontena la liko wapi?
Muulize Yale mabomba ya gas yaliyo pitishwa baharini kupeleka gas ulaya yamefikia wapi?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom