Je CCM Imekodi wazungu wa Finland Kumchafua Dr.Slaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je CCM Imekodi wazungu wa Finland Kumchafua Dr.Slaa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by IsangulaKG, Oct 15, 2010.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Jana wakati nimekaa sina hili wala lile ikaingia sms katika kibofya changu toka katika namba '+3588108226' ikisema,'SLAA NI MROPOKAJI NA MGOMVI ANATUKANA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.ANATAKA DAMU IMWAGIKE ILI MRADI AINGIE IKULU.TUMKATALIE KUIGEUZA NCHI YETU SOMALIA'. Baada ya kusoma sms hii nilighafilika sana.Kwa harakaharaka nilijua aliyeituma ni Mpumbavu,Muoga,hana uwezo wa kufikiri au ametoroka hospitali ya vichaa japo nachua chama anachotokea.Nilipojaribu kuipiga namba hii wala kuijibu sms nikashindwa.Namba hii baadae niligundua ni Code ya Finland katika mji uitwao Oulu Swali hapa ni kuwa Je CCM Imekodi Wazungu wa Kumchafua Dr. Slaa?
  Ninazo sababu nyingi za kumuita mtuma sms mjinga,myoga au Mpunbavu na Punguani,Kwanza kabisa;
  KUMWITA SLAA MROPOKAJI NA MGOMVI
  Ni mropokaji huyuhuyu ndiye aliyeweza kufichua kashfa kibao za Ufisadi ambazo wabunge kibao 'Mabubu' Waliogopa Kuropoka. Matokea ya kuropoka kwake tukayaona,Akina Lowasa wakawajibika. Angalau tukaona kesi kadhaa Japo za 'Vimeo vya ufisadi'.Tunamtaka huyu huyu 'MROPOKAJI' awe Raisi wetu...awaseme watendaji wasiotimiza wajibu wao.Tunamtaka Huyuhuyu 'Mgomvi' ambaye akiwaambia watu wasiotimiza wajibu wao Ukweli anaonekana Mgomvi...Mimi huyuhuyu Mropokaji na Mgomvi ndiye RAIS WANGU!

  SLAA KUTUKANA VYOMBO VYA USALAMA
  Nani asiyeona vyombo vya Usalama vinavyoibeba CCM? Nani asiyeona Upendeleo wa Wazi ? Nani asiyeona Ulinzi anaopewa Salma Kikwete? Kwa Nini Mke Wa Lipumba na wake wa Wagombea wengine wa Urais hawapewi ulinzi ili wawapigie kampeni waume zao? Kwa hili Mtuma Message ni Punguani. Kwa hiyo alitaka Slaa avisifu vyombo vya Ulinzi kwa kuipendelea CCM? Nnachomwomba Slaa...Endelea Hivyo hivyo Rais wangu.Asiyewajibika na kutenda haki mpe 'DOZI' yake hapohapo

  ATI SLAA ANATAKA DAMU IMWAGIKE ILI AINGIE IKULU
  Kweli mtuma sms ni Mtumwa wa Kiakili ama hajasoma au nikichaa. Nani alikuambia Demokrasia ina vunja Amani. Hebu angalia Marekani enzi za Kampeni za Kina Obama.. Damu ilimwagika? Najua atasingizia Kenya au Zanzibar Miaka ya Nyuma pasipo kujua kuwa 'DAMU HUMWAGIKA HAKI IKIPINDISHWA NA KURA KUIBIWA!! Nani asiyejua kuwa Raila Odinga aliibiwa kura? Nani asiyejua kuwa Maalim Seif aliibiwa kura na Kudhulumiwa Urais.....Namtahadharisha mtuma sms kuwa iwapo Chama chake kitaiba Kura na Kumdhulumu Slaa haki ya kuwa Rais inawezekana kweli Damu Ikamwagika.. Sipendi Tufike Huko kwa kumwagika Damu.. Kimsingi nnachosema ni Kuwa HAKI Ikitendeka siku zote Hakuna damu inayomwagika. Labda sijamwelewa mtuma sms..Ana maana Slaa akiiingia Ikulu Damu Inamwagika? Ina maana Chama cha mtuma sms (CCM) Kimejiandaa kumwaga Damu Slaa akiingia Ikulu??? Kwani Nchi Hii ni ya CCM?
  Ndiyo maana nikamwita mtuma sms kuwa ni Punguani na Mtumwa wa Mawazo .Watu kama hawa ni Pazia la kukua kwa Demokrasia...Hawatakiwi nchi hii.

  ETI SLAA ATAGEUZA NCHI KUWA SOMALIA
  Kuna watu humu Duniani wanahitaji Kufanyiwa Neurological Surgery. Huyu Jamaa hajui hata Historia ya Somalia. Hajui Hata Historia ya Tanzania. Hajui kwa nini Tanzania haiwezi kuwa na machafuka kama Somalia. Naomba arudi Darasani akasome historia vizuri.

  HITIMISHO
  Ni vema tusianze kuwatisha watanzania kupitia Sms na badala yake tuwaeleze Sera za vyama vyetu na jinsi ya kuzitekeleza na siyo kutuma sms zenye kuwaponda wagombea, Kwa mfano mtuma sms alidhani ameikampenia CCM kumbe ndiyo ameipunguzia CCM Kura yangu.
  Watanzania Tuache Uoga na tuachane na Vitisho.
  Ni KAMA VILE WATU WANAVYOSEMA ELIMU BURE KWA WOTE HAIWEZEKANI?? Nakumbuka Profesa wangu alinifundisha kuwa 'FEAR OF FAILURE IS A FAILURE ITSELF'
  Watu wanaogopa na hawasomi SERA Vizuri..Tuanze Kubadilika mawazo na Kuamini kuwa kila kitu Kinawezekana. Mbona Tunaamini kuwa 'TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA? Wakati tunajua Ukimwi ni Chronic Infection na Kwamba ili tuwe na Tanzania Isiyo na Ukimwi ni Lazima Wagonjwa wote wa Ukimwi wauwawe?.. Lakini Bado Tunaamini tu Kuwa Tanzania Bila Ukimwi Inawezekana..Tena tunasimama na Kuimba Majukwaaani....Tanzania Bila UKIMWI Inawezekana!!!! Sasa kama Tanzania bila Ukimwi Inawezekana na tuna Mamililioni ya Wagonjwa wa Ukimwi na wengine maelfu wanaambukizwa kila siku na bado tunasema Bila Ukimwi inawezekana.. Je Kama Rasilimali zetu na Mafedha kibao yanayotumika Bungeni na Matumizi feki ya Serikali yakidhibitiwa hatuwezi Kuwa na ELIMU BURE KWA WOTE?
  Kila Mtanzania achambue Sera na aepuke Propaganda za Mapunguani
  wachache wanaotaka kuogopesha wengine

   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Ni wajinga pekee ndiyo watashabikia huu ujumbe, mwisho wa CCM ushafika.
   
 3. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  POST HII IMETOLEWA KWA RUHUSA YA Mwana JF 'Kaisa079"
   
 4. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu ni uongo mtupu, namba sio ya Finland. Imetengenezwa hapa hapa nchini. Mi nimewahi kuwa Finland na namba za kule ni kama za huku kwetu kwa maana kwamba baada ya code number, kunakuwa na tarakimu zingine tisa (kama huku kwetu). Kwa mfano naomba nikupe namba ya rafiki yangu wa Finland (nimemuomba kufanya hivyo ili kuondoa utata), ambayo hata ukiipiga sasa hivi inaita; +358 407 450 963. Anatumia Mtandao wa Telefinland, na mitandao yote kule ina tarakimu idadi sawa na hizo.

  Kwa hiyo hii wanayotumia CCM ni geresha, imetengenezwa hapahapa na ukiipiga unaambiwa haipo.... We unatumia mtandao gani?
   
 5. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Mimi natumia Mitandao yote Zain,Tigo,TTCL Mobile,Vodacom na Zantel kikazi kibiashara na shughuli Binafsi
  Inawezekana CCM imepartner na TCRA Kunipiga Changa La macho na Hata nikipiga wala Kutuma Sms Haziendi Kabisa
   
 6. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hata product huwa inafikia kilele then hufa... huu ndo mwisho wa CCM...
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,655
  Likes Received: 21,868
  Trophy Points: 280
  CCM iko ICU na madaktari wamedhibitisha kuwa haiwezi kupona kabisaaaa, kuna aina za magonjwa ambazo mtu akitaka kukata roho huwa anahangaika sana. Ndivyo ilivyo kwa CCM, inakata roho kwa mahangaiko sana
   
 8. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #8
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Wasi Wasi wangu ni Kuwa Huu Mwamko tulio nao sisi tulio Mjini ndo huohuo hata Vijijini? Ambako Nyuma ina matobo kibao ya Udongo,Kitanda kunguni tele cha Kamba na inachangiwa na binadamu na wanyama lakini nje kuna Poster ya 'Chagua CCM,CHAGUA KIKWETE?
   
 9. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #9
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Wasi Wasi wangu ni Kuwa Huu Mwamko tulio nao sisi tulio Mjini ndo huohuo hata Vijijini? Ambako NYUMBA ina matobo kibao ya Udongo,Kitanda kunguni tele cha Kamba na inachangiwa na binadamu na wanyama lakini nje kuna Poster ya 'Chagua CCM,CHAGUA KIKWETE?
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Bado siamini kama sms hiyo inatoka Finland. Utakuwa umetengenezwa na genge la wahuni wa Kihindi tu hapa hapa Tanzania.

  Huo ujumbe ulitengenezwa hapahapa. Lakini uko 'encrypted'. Hiyo kitu inawezekana kwenye ishu za Information Security. Hiyo +358 inawezekana ni 0713, 0788, 0754, .........inaweza kuwa chochote kulingana na code zilizotumika.

  Ubalozi wa Finlanda wanasemaje?
   
 11. p

  pierre JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  it is true
   
 12. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ila jamani huku kuchezewa tunakofanyiwa si sawa na kuambiwa hatuna akili Watz?
   
 13. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hii kitu naamini imetengenezwa hapahapa..labda wako kwenye "trial" ya kugeuza matokeo...
   
 14. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #14
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Huku Vijijini CCM Wanawadanganya Watu kuwa wakichagua UPINZANI nchi itakuwa Kama Kenya..Hawatangazi Sera ila Wanawaogopesha Wananchi.Na Unachunguza vizuri Video za watu wanaomuimbia Kikwete katika Kasmpeni zake Vijijini? Wengi wamevaa Yebo Yebo na wana Mipasuko Miguuni...but wao kwao Hiyo Si Shida...Ni Chagua CCM Tu Mioyoni mwao! We are Still Very Far from Realizing that We Need Change in this Country...especially the Leadership Change! ....and Mind set Change! Kama bado watu wanaona MATATIZO ni HAKI yao bado hatuwezi Kupata UKOMBOZI wa Kimaendeleo!
   
 15. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Certainly namba ni ya kutengenezwa, katika teknolojia hilo ni jambo dogo sana.

  Hawa jamaa wanafanya kila liwezekanalo but thank GOD THAT ALL EVIL PLANS + WILES & DEVICES will fail.

  Vijijini wapo waliochoshwa kama TARIME, MBY etc. Kuna documentary moja nilituma link hapa ila naona imekataa, ukiiona utaelewa vyema jinsi watz walivyochoka.

  Mungu kawakumbuka mwaka huu!
   
 16. k

  kyabola Member

  #16
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dogo..hapo wa kulaumiwa ninani? ni CCM?,Uchaguzi huu ni wa nne wa vyama vingi..twendeni vijijini kuelimisha watu.
   
 17. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Heko tulutumbi.

  Nakushauri uipeleke makala hii ichapishwe Mwanahalisi, Raia Mwema, Mwananchi, Majira, etc. Fanya malekebisho kidogo uondoe majina ya vyama na ujumbe wako utawapata wengi, Hongera sana kwa andiko zuri!
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kazi ipo
   
 19. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Message kama hizi ni rahisi kujua zimetokea wapi. Hata TCRA wanatafuna midomo tu ila ni rahisi sana kujua ilikotokea, hazijifichi. Kitu cha kwanza angalia umepokea ujumbe huo kwenye namba ya mtandao gani. Kama simu yako ina namba ya Voda kwa mfano, manake hiyo message imekuwa forwarded na SMSC ya Vodacom. SMSC ni kifupi cha Short Messages Center. SMSC ya vodacom haiwezi ku-forward message ambayo Vodacom hawajui ina-originate wapi, mpo hapo??

  Message yoyote lazima ioneshe ilikotokea na inakokwenda. Ikikosa kimojawapo, SMSC ya mtandao husika haiwezi kuituma. Kwa hiyo kama umeipata kwenye namba ya Tigo, Tigo wanajua ilikotoka; kama umeipata kutoka kwenye namba ya Vodacom, Vodacom wanajua ilikotoka. Sasa angalieni, wanaotumia baadhi ya mitandao, hiyo message hawapati, manake hiyo mitandao haijatumiwa.

  Lazima kuna makubaliano kati ya anayetuma message na mtandao husika. Kwa kuwa message hiyo haioneshi imetokea wapi, basi mtandao husika (ambao umepokelea hiyo message) una makubaliano maalum na huko ilikotokea message hiyo. Nani anailipia message hiyo? Ni lazima iwe inalipiwa na mtandao hauwezi kukubali kusambaza message ambayo haijalipiwa.

  Tanzania mawasiliano ya message ni sender keeps all. Manake anayetuma ujumbe huchukua fedha yote. Kwa hiyo, ili mtandao wowote wa Tanzania utume ujumbe lazima ujue kuwa ujumbe huo umetokea kwa mtandao wa Tanzania! Vinginevyo wanau-filter ujumbe huo. Kama umetokea nje, basi mtandao uliousambaza una makubaliano fulani na chanzo chake huko nje.

  Kwa hiyo, kama ujumbe umeupata kwenye namba ya Tigo, Tigo wanajua. Kama unaupata kwenye namba ya Zain, basi zain wanajua. Hakuna muujiza hapo. Ni rahisi mno. Na hakuna siri hata kidogo!
   
 20. Mtuflani

  Mtuflani JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 323
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dawa ni kumpiga chini na wabunge wake hapa mjini ili vijijini wajifunze
   
Loading...