Je, CCM imebemendwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, CCM imebemendwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jogi, Apr 24, 2012.

 1. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Hitimisho la kikao cha bunge leo limebainisha kuwa ccm inalinda na italinda kile inachodhani kuwa ni "sifa za kikwete" hata ikiwa ni kwa gharama ya kujinyonga.

  Msingi wa hoja yangu upo kwenye ibara ya 8(1) (a), (b), (c) na (d). pia ibara ya 9(a)-(i).

  Pamoja na ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali kuweka wazi kuwa mawaziri wametusababishia hasara kubwa iliyotokana na uvunjwaji wa katiba kwenye ibara nilizozitaja hapo juu, bado waziri mkuu Pinda ameendelea kuruka sarakasi huku amevaa taulo, anatuimbia ngonjera tukiwa icu, anatusomea risala tukipiga miayo ya njaa. Anashuhudia mawaziri ambao yeye ni kiranja wao wakihujumu uchumi kwa dhamana tuliyowapa, na kung'ang'ania madaraka hayo, Pinda kajipinda kuwafundisha maprofesor kusoma, kuandika na kuhesabu!!!!!!

  Mchezo mzima ni kutochukua hatua ili aje achukue hatua hizo kikwete iwe kwamba wengine wooooote wabaya including ccm isipokuwa mzuri pekee ashangiliwaye na wazee wa dar kwa kuchelewa kuutatua mgogoro baina ya serikali na madaktari!!!!! na sasa mawaziri wamebainika kututia hasara, wanadai kuwa sahihi kutuibia, na Pinda kajipiiiinda kusoma risala ya kuahirisha bunge, kanakwamba hakuna lililotokea ili hatimaye kikwete akiisha kwisha chelewa kwa kujizungusha aje kushangiliwa na wazee wa dar kwa kumiminiwa misifa kibao! Haya niambieni huo uzuri wa jk v/s ccm, wapi mtiririko wa kimamlaka, ccm kweli inaweza kuisimamia serikali? au ishabemendwa na sifa ya mtu mmoja?(jk)
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Loading......
   
Loading...