Je CCM ikiondolewa madarakani 2015 magazeti ya Uhuru na Mzalendo yataendelea kuwepo?

Landala

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
997
473
Watanzania wenzangu hivi haya magazeti ya magamba ya Uhuru na Mzalendo yataendelea kuwepo 2015 endapo CCM itaangukia pua kwenye uchaguzi mkuu ujao maana kwa sasa hivi hayanunuliwi na yanaendeshwa kwa kutegemea ruzuku kutoka CCM.
 
Yataendelea kuwepo na yatakuwa na UMUHIMU sana siku hizo kwani haya Pro-Chadema yatakuwa ni ya Mafisadi.

Uhuru yatapendwa sana kwani yatafumua siri zote za Serikali na chama cha CHADEMA.

Yatamwaga mabaya ya viongozi wote walioko madarakani kuanzia Rais hadi Waziri Mkuu.

Mie ntasoma zaidi hayo. Ila kwa sasa yanisubiri kwanza.
 
Uhuru ni la Serikali au CCM? Nadhani ruzuku inatoka Serikalini.
Mkuu, hayo magazeti ni ya magamba. Kwa mtazamo wangu naona yatakufa maana chama cha magamba hakitakuwa na pesa za kuendelea kuyapa ruzuku kwa kuwa kitakuwa kimetolewa kwenye chungu cha taifa ambako sasa wanajichotea wapendavyo.
 
Mkuu, hayo magazeti ni ya magamba. Kwa mtazamo wangu naona yatakufa maana chama cha magamba hakitakuwa na pesa za kuendelea kuyapa ruzuku kwa kuwa kitakuwa kimetolewa kwenye chungu cha taifa ambako sasa wanajichotea wapendavyo.

Kweli lazima yatoweke kwa mwendo huo mkuu
 
Uhuru ni la Serikali au CCM? Nadhani ruzuku inatoka Serikalini.

gazeti la uhuru linamilikiwa na chama cha mapinduzi mkuu na hujiendesha kwa ruzuku kutoka CCM mkuu.Magazeti ya serikali ni Habari leo na Daily News
 
Kwa sababu tanzania ni ya demokrasia kwa hiyo hayo magazeti yatafanya kazii kama kawaida.
 
Magazeti ya Uhuru na Mzalendo yataendelea kuwepo tu, mbona kwa sasa Mwananchi,Mwanahalisi na Tanzania daima yapo?
 
wapo wanazi wa CCM wataendelea kuyanunua kwa hiyo yataendelea kuwepo kwani nchi nyingi kuna vyama vya watu mahafidhina(convervative parties) ambao huwa hawaachi misimamo ya kizamani mpaka wanaingia kaburini
 
Kawaulize CCM, kwanza sidhani kama CCM inaweza ikatoka madarakani.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Back
Top Bottom