Je, CCM huwa inaamua mpinzani gani aende Bungeni? Kama ndio, ina maana Mbowe na genge lake walibwagwa kimkakati?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,087
6,568
Hiki chama kinachotawala hapa nchini kwetu kina mtandao mpana sana. Hii ni kwa mujibu ya historia yake na jinsi kilivyojijenga kisiasa.

Ndio maana ukiwazingua wanakuweka kando na kukushit.

Inasadikiwa kuwa Mbowe na genge lake CCM haiwataki kabisa, maana wamekuwa hawana uzalendo.

Swali linakuja kama ndioCCM ina uwezo wa kuchagua mpinzani gani awe na nguvu na yupi asiwe na nguvu. Je, Oktoba mwaka 2020 uchaguzi ulipofanyika CCM iliamua kuwabwaga Mbowe na genge lake?

N:B Halima Mdee na genge lake wanakuja juu mithiri ya kiboko anaibuka kwenye maji.
 
Swali hilo ndlo jibu lenyewe ccm ya awamu hii kama hawakutaki huwezi penya hata kwenye tundu la sindano,tume ya uchaguzi yao,usalama wa taifa wao,bunge lao,mahakama zao,polisi wao,pesa zao,vyombo vya habari vyao,spika wao,rais wao,wakurugenzi wao,sasa wewe unaona utashinda??? Kama waliweza kumtoa mtuhumiwa mahabusu kwenda kumwapisha ghafla bila ridhaa ya chama chake unafikiri wanashindwa nini?
Kwa kweli ile ya kumtoa mahabusu na kwenda naye kumwapisha haraka haraka vichochoroni ilikuwa kali ya mwaka. hawa hawashindwi chochote
 
kilivyojijenga kisiasa
Rekebisha hapa.Hakijajijenga ''Kisiasa'' bali kina mfumo wa kimafia,ambao kinautumia mfumo huu kujiweka madarakani.Kisiasa ina maana huwa kinapewa ridhaa na wananchi kitu ambacho si kweli.Rejea:Wizi wa waziwazi wa kura uchaguzi uliopita pamoja na nukuu ya mwenyekiti ya jana''Madiwani hamkuchaguliwa na wananchi''.
 
Hiki chama kinachotawala hapa nchini kwetu kina mtandao mpana sana. Hii ni kwa mujibu ya historia yake na jinsi kilivyojijenga kisiasa.

Ndio maana ukiwazingua wanakuweka kando na kukushit...

Usiingize ccm, maana ccm kama chama ni wafaidika tu wa madaraka ya urais yanayotumika vibaya. Wananchi ndio wanamaamumuzi ya kuingiza wabunge bungeni, ila rais kutokana na kiburi cha madaraka ndio anapoka haki ya wananchi, na kuingiza bungeni genge lake litakalolinda maslahi yake kinyume na matakwa ya wananchi.
 
Jibu no, why wenda wajua nini kilitokea,KWA uchaguzi huru na wa haki ccm ubunge wangepata viti visivyopungua,16 au chini, kiti Cha urais ingekua zilipendwa, hata malaika,au shetani anajua maana tz tuna mfungamano wa imani nyingi.

Ila ukweli wa mungu ccm mnajua,na Kama waboshi chukua biblia hapa ulipo utashangaa,dunia utashangaa, hakuna ccm tz hii KWA sasa ni mapambio so far mko madarakani.

Note
Kwa sasa ni mwanachama mpya wa CHADEMA but hapo juu hayausiani na uhanachama bali upendo wa taifa langu , sio chama hapa Kama wewe
 
CCM ni uchafu kama ulivyo uchafu mwingine tu wa jalalani. Ipo siku tu tutausafisha na kuuondoa Nchini mwetu.
Hizi kauli za ipo siku sizani kama itakuja kutimia tanzania hii, akuna viumbe wazuri kubwana mtandaoni na waoga kufanya mamuzi kama wa tz na yote inachangiwa na umimi tulionao
 
Usiingize ccm, maana ccm kama chama ni wafaidika tu wa madaraka ya urais yanayotumika vibaya. Wananchi ndio wanamaamumuzi ya kuingiza wabunge bungeni, ila rais kutokana na kiburi cha madaraka ndio anapoka haki ya wananchi, na kuingiza bungeni genge lake litakalolinda maslahi yake kinyume na matakwa ya wananchi.
Duh!
 
Swali hilo ndlo jibu lenyewe ccm ya awamu hii kama hawakutaki huwezi penya hata kwenye tundu la sindano,tume ya uchaguzi yao,usalama wa taifa wao,bunge lao,mahakama zao,polisi wao,pesa zao,vyombo vya habari vyao,spika wao,rais wao,wakurugenzi wao,sasa wewe unaona utashinda??? Kama waliweza kumtoa mtuhumiwa mahabusu kwenda kumwapisha ghafla bila ridhaa ya chama chake unafikiri wanashindwa nini?
Fuu la nazi hilo. Anajifunzia kuandika jf. Kachukua nafasi ya P. Anauliza swali! Katoka nchi gani huyu? Mei 2020 jimboni Kongwa kuonyesha uamiri jeshi wake akiwakatinga ndani ya kiwalo cha jwtz. Kaoorodhesha matatizo lukuki hapo jimboni. Hakusema yatatatuliwa vipi. Kawambia wapiga kura wa Kongwa kuwa atamtuma mbunge wao. Usiniulize anamtuma kufanya nini. Hayajui wakati yeye ndiye mbunge?
Walikataa kwa kusema kuwa asimtume. Haraka haraka akawaelewa. Akasema hatamtuma kwa kuwa yeye ni spika! Elewa Nyankurungu usoelewa. Wapiga kura hawamtaki. Mathematician akakokotoa quadratic equation haraka. Jibu ni kupita bila kupingwa. Vituo hewa na masanduku yalojaa kura Oktoba 2020 visingefua dafu. Zingepigwa hata kura za maruhani! Soma hiyo! Mwendo wa uchafuzi tu.
 
Who is P? Mpaka nijifunze kwake? Mimi ni mtu huru.
 
Kuelewa kwako ndilo tatizo. Nimesema kuandika unajifunzia jf. Umechukua nafasi ya P. Umejifunza kwake wewe hilo walijua zaidi. Halinihusu. P. is P. Watwana hawajifunzi. Wakijifunza utwana utakoma. Watu huru hujifunza kwa ari na maarifa. Leo nimekutana na asiyejifunza. Mtwana hakika!
 
Back
Top Bottom