Je, bunge limebadilisha majukumu yake ya msingi au kuna mpango maalum kuwa siku ni wabunge wa upinzani?

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,091
Kwa siku Za karibuni bunge letu limekuwa linapoteza mvuto kwa wananchi kutokana na kukiuka misingi ya uwepo wake ambao ni kutunga sheria lakini pia kuisimamia na kuishauri serikali.

Sasa hivi bunge limekuwa kama tawi la serikali kwa kupitisha kila serikali inachotaka hata kiwe hakuna manufaa kwa wananchi. Itakumbukwa kuwa kwa siku Za hivi karibuni imekuwa ni dhambi kubwa kuikosoa serikali hasa bungeni tangu itoke kauli ya “Wakiwa mule bungeni wana kinga kwahiyo we watoe tu Huku nje halafu mi nitashughulika nao”

Tangu kauli hii imetoka tumeshuhudia wabunge wengi wa upinzani wakikumbwa na adhabu mbalimbali zikiwemo kufungiwa kutohudhuria vikao kadhaa vya bunge kwa kupatikana na hatia kwa vile tu walitoa maoni yaliyopingana na yale serikali inataka.

Mpaka Sasa kiasi cha wabunge 8 wa upinzani wameshaitwa kwenda kwenye kamati ya maadili ambayo mara zote imeishia kupendekeza adhabu za kufungiwa kuhudhuria vikao mpaka vitatu vya bunge.

Spika wa bunge aliwahi kumwambia mmoja wa wabunge wa upinzani kwamba anaweza kumfungia kuhudhuria bunge na asimfanye lolote. Kauli kama hizi si tu zinatia mashaka juu ya dhamira ya viongozi wa bunge Bali pia zinafanya ile dhana ya bunge kuwa dhaifu kuwa na mashiko machoni mwa wananchi na wale wasioangalia mambo kwa mtazamo wa kichama.

Jana mbunge mwingine wa upinzani Mhe Catherine Ruge ameitwa kwenye kamati ya Maadili, haki na Madaraka ya Bunge kwenda kuthibitisha kauli yake kuwa mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge utagharimu zaidi ya 21trilion tofauti na gharama ambazo zinasemwa na serikali. Na hii alifanya reference Kwenye report ya Joerg Hartmann PhD ambaye ni mtaalam wa masuala ya nishati na mazingira aliyeufanyia utafiti mradi huo. Hii ilitokana na naibu waziri wa nishati kusema kuwa wao (Serikali) wanajua mradi utagharimu 6Trilion bila kuelezea kwa kina gharama hizo zimepatikanaje.

Swali la kujiuliza ni je kuna umuhimu wa kuwa na bunge ambalo Sasa limegeuka kuwa tawi la serikali?
bfb38588-a9a8-4d5e-8829-7b5efb3e3d80.jpg
IMG_3326.JPG
 
View attachment 1107275View attachment 1107277
Ogopa sana....kukosa akili....

Ujinga unakufanya unavyotaka.....

Adui Ujinga na Maradhi wakishikana pamoja ni hatari sana. kama ni Spika itakuwa inapiga makelele tu na kuwa kero ktk jamii....

Bunge ni Dhaifu...
 
Back
Top Bottom