Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,443
- 113,452
Wanabodi
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala fikirishi za "Kwa Maslahi ya Taifa".
Mada ya leo ni swali
Jee kuna uwezekano Bunge letu L
linaendeshwa kikada?. Ili tuwe na Bunge madhubuti la Haki, lenye uwezo wa kuisimamia serikali kikamilifu, jee kuna haja kwa Spika asitokane na vyama vya siasa na mawaziri wasiwe wabunge?
Baada ya kuvuliwa ubunge kwa Mbunge wa Arumeru Mhe. Joshua Nasari, kwa kosa ndogo tuu la kutotoa taarifa ya kutohudhuria mikutano zaidi ya mitatu bila ruhusa ya Spika, kuna wengi wanaona uamuzi wa Spika kama una some elements za ukada ukada!, mfano sijabahatika kumuona au kumsikia Prof. Mhongo akichangia hoja yoyote tangu alipotumbuliwa uwaziri, or let's assume taarifa ya kutoonekana kwake jee zipo mezani kwa Spika?!.
Japo mfumo wa Bunge letu ni mfumo wa Westminster wa Bunge la Uingereza na mabunge ya Commonwealth, lakini katika mfumo wa vyama vingi, ili haki itendeke na kuonekana kuwa haki inatendeka, jee mnaonaje kama tutabadili sheria ili Spika wa Bunge letu asiwe mwanachama wa chama chochote cha siasa, kama walivyo Majaji, ili kuepuka maamuzi ya kikada?.
Kuna uwezekano kabisa wa uamuzi huu wa Spika ni uamuzi wa haki kabisa uliofuata sheria, taratibu na kanuni za Bunge, lakini chama athirika bado kikaona kama kimeonewa, na kuwa haya ni maamuzi ya kikada kukibeba chama chake!. Mbona tunawasikia wabunge wa CCM wakitoa kauli za hovyo na za kiajabu ajabu mule Bungeni lakini sijawahi kusikia wakishurutushwa kufuta kauli au kutolewa nje, inamaana wabunge wakosefu ni wa upinzani tuu?!
Sambamba na hilo, ili tuwe na Bunge imara na madhubuti lenye uwezo wa kuisimamia serikali kikamilifu na ikibidi kuiwajibisha, mnaonaje kama mawaziri wasitokane na wabunge, ili kuutimiza ile dhana ya the principle of separation of powers, checks and balances?.
Bunge linapaswa kuisimamia serikali, na serikali inapoboronga, Bunge letu linatakiwa liwe na uwezo wa kuiwajibisha serikali!, hili bunge jipendekeza na Bunge jikombakomba linaweza kweli kuisimamia serikali?.
Inapotokea Wabunge wenye jukumu la kuisimamia serikali, halafu miongoni mwa Wabunge hao wanateuliwa kuwa mawaziri ambao sio tuu wanakuwa ni sehemu ya serikali, bali wanapokea ulaji, sasa katika mazingira kama haya, Wabunge hawa wanaweza vipi kuiwajibisha serikali wakati wao ni sehemu ya serikali?. Mtu unawezaje kulikata tawi la mtu ulilokalia, au mkono unaokulisha?.
Tena kazi ya Bunge sio tuu kuisimamia serikali au kuiwajibisha serikali, bali ndio mamlaka pekee yenye uwezo wa kumuwajibisha rais wa JMT kwa kumuondoa madarakani!, Bunge letu hili Bunge nyoronyoro, rais wa JMT akivunja katiba wanaweza kumuwajibisha?.
Lakini kwa mfumo wetu, rais ni sehemu ya Bunge kwa kuliunda, kulihutubia na kulivunja, pamoja na kuteua mtendaji Mkuu wa Bunge, ikitokea rais amefanya kosa kubwa mfano la uvunjaji wa Katiba, Bunge likaamua ku initiate impeachment process, lakini kwa mamlaka aliyokuwa nayo rais wa JMT kwa mujibu wa katiba yetu, kabla Bunge halijamuwajibisha rais, rais naweza kulivunjilia mbali Bunge, na kuitisha uchaguzi mwingine!.
Tukija kwenye uteuzi wa wakuu wa mihimili na vyombo vya dola, kama Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, CDF, Mkurungezi Mkuu wa TISS, Takukuru, CAG, etc, rais aendelee kuwateua lakini waidhinishwe na Bunge ili kama rais amewateua rafiki zake tuu wasio na sifa au vigezo, Bunge limkatalie, au ikitokea rais amekwenda kinyume cha katiba, vyombo hivi viwe na meno ya kung'ata.
Kwa mfumo huu tulionao sasa wa Spika wa Bunge kutoka chama tawala, hata ikitokea ni kweli rais amevunja Katiba na anapaswa kuwajibishwa, hivi kweli Spika gani anaweza hata ku entertains such motion, yaani ipitishe hoja ya kujadili kumuondoa Mwenyekiti wa chama chake madarakani?, chama kilichokupa huo Uspika?.
Spika asipotokana na chama cha siasa, atakuwa na chance ya kuliendesha Bunge kwa haki bila kutokea hisia za ukada ukada, kama walivyo Majaji, hawana vyama, na kwenye nafasi za juu za utendaji Jaji Mkuu, na wakurugenzi wakuu wote wa taasisi za umma, nafasi zitangazwe, wenye sifa waombe, na sio watu hawana sifa lakini wanateuliwa kwa mserereko.
Nawatakia Furahi Dei Njema.
Wasalaam.
Paskali
Rejea
Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika! - JamiiForums
Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!. - JamiiForums
Swali: Jee Spika Anayo Mamlaka Kuzuia Muongozo wa Spika au ni Udikteta Tuu?! - JamiiForums