Je Bunge la Tanzania linafanya kazi ya uzalendo kwa Watanzania au ni kazi zao binafsi?

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kwa mjibu wa katiba ya Tanzania ,Bunge la Tanzania ndio chombo kikuu cha kuisimamia serikali na taasisi zake zote

Kilichofanywa na Bunge la Tanzania leo ni kitu cha ajabu sana ambacho kwa mawazo ya kawaida au kwa kufikiria kawaida,nani anakomolewa hapa

Hivi Bunge la Tanzania linafanya kazi zao binafsi au wanafanya kazi za wananchi waliowachagua

Bunge la Tanzania kumsusia CAG kutofanya kazi naye nani anaumia? Nani anakomolewa? Nani atapata hasara?

Kwa majibu ya haraka sana ni kwamba wananchi ndo tunaumizwa

Wala CAG hana shida,washirikiane au wasishirikiane,mshahara na marupu rupu yake yapo pale pale,mwisho wa mwezi account yake inajazwa manoti

Bunge la Tanzania linamkomoa nani?

CAG anakagua hesabu na matumizi ya serikali,na Bunge katika kulisimamia serikali lazima waangalie CAG amegundua madudu gani ili Bunge litie pressure watu wachukuliwe hatua,najiuliza kazi ya Bunge la Tanzania itakuwa ipi hapo Bungeni?

Kwa kweli watanzania tumepotea sana kuwa na Bunge kama hili

Utadhani Bunge ni kampuni badala kuwa chombo cha wananchi kinachomlika serikali' fedha inayokusanywa je inafanya kazi kama ilivyoelekezwa au wanafanya mambo yao

Hili ni Bunge la ajabu,kususia CAG ni kumkomoa mwananchi wala hamjamkomoa CAG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichokisema CAG hakina tofauti na wimbo wa mkuu wa nchi kuhusu Upigaji wa dili unaofanywa na watanzania na bunge linafumba macho na halina habari. Wacha CAG amsaidie mkuu wa nchi.
 
Tanzania hakuna bunge la uwakilishi wa wananchi, bali kuna bunge la uwakilishi wa serikali.

Bunge huwa ni sauti ya umma lakini kwa hapa Tanzania ni idara ya serikali.

Kuna sheria mbalimbali za hovyo zinapitishwa na bunge hadi unajiuliza hizi sheria ni kwa manufaa ya nani!

Bunge ambalo kazi yake kubwa ni kukandamiza raia kupitia sheria linalozitunga unawezaje kuliita bunge la wananchi?!.
 
Kwa mjibu wa katiba ya Tanzania ,Bunge la Tanzania ndio chombo kikuu cha kuisimamia serikali na taasisi zake zote

Kilichofanywa na Bunge la Tanzania leo ni kitu cha ajabu sana ambacho kwa mawazo ya kawaida au kwa kufikiria kawaida,nani anakomolewa hapa

Hivi Bunge la Tanzania linafanya kazi zao binafsi au wanafanya kazi za wananchi waliowachagua

Bunge la Tanzania kumsusia CAG kutofanya kazi naye nani anaumia? Nani anakomolewa? Nani atapata hasara?

Kwa majibu ya haraka sana ni kwamba wananchi ndo tunaumizwa

Wala CAG hana shida,washirikiane au wasishirikiane,mshahara na marupu rupu yake yapo pale pale,mwisho wa mwezi account yake inajazwa manoti

Bunge la Tanzania linamkomoa nani?

CAG anakagua hesabu na matumizi ya serikali,na Bunge katika kulisimamia serikali lazima waangalie CAG amegundua madudu gani ili Bunge litie pressure watu wachukuliwe hatua,najiuliza kazi ya Bunge la Tanzania itakuwa ipi hapo Bungeni?

Kwa kweli watanzania tumepotea sana kuwa na Bunge kama hili

Utadhani Bunge ni kampuni badala kuwa chombo cha wananchi kinachomlika serikali' fedha inayokusanywa je inafanya kazi kama ilivyoelekezwa au wanafanya mambo yao

Hili ni Bunge la ajabu,kususia CAG ni kumkomoa mwananchi wala hamjamkomoa CAG

Sent using Jamii Forums mobile app
Bunge la ndugai ni genge hatari kwa mustakabali wa taifa. Ni uamuzi "mgumu"tu unaoweza kunusuru nchi. OPRESHENI DELETE ccm INAHITAJIKA!.
 
Back
Top Bottom