Je Bunge la Katiba Litapatikana vip?

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,417
3,154
Kwa mujibu wa machapisho, Bunge lilounda Katiba ya sasa mnamo 1977 lilikuwa Bunge la kuteuliwa, hivyo lilitekeleza majukumu ya wale walioliteua.
Naomba kujua, Bunge lijalo la kutengeneza Katiba kwa kuunganisha mawazo ya Watanzania litapatikanaje? Je litakuwa la kuteuliwa au kupigiwa kura na Wananchi?
 
nadhani kwa mujibu wa sheria iliyopo ni hili bunge lililopo plus wabunge wengine 116 wa kuteuliwa na Rais. nimejibu swali lako mkuu?
 
Aiseee kama bunge la katiba litakuwa na wabunge wa bunge hili hili tulilolizoea itakuwa ni hatari sana hiyo katiba naona bado itaendelea kuwa katiba ya ccm na sio katiba ya wananchi.
 
Kuna kiasi Cha wabunge kwenye bunge hili na ni wachache sio wengi Kama hao wengine watakaotoka kwenye kada mbalimbali
 
Ahsanteni wote! Naomba mchango wenu juu ya haya maswali: Je hao wabunge wataotoka nje ya Bunge la sasa watapatikana vipi? Je hao Wabunge wa kutoka Bunge la sasa wataacha majukumu waliopewa na Watanzania na kufanya kazi ya kuunda Katiba? Je kama ni hivyo, hao Wabunge wa sasa hawatoweza, kupitia majimboni, kuwashawishi wananchi kupitisha Katiba mbovu waliyoipitisha?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom