Je, bomba la mafuta kutoka Uganda litapita kwenye maeneo ya hifadhi za barabara yetu?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,090
Mwaka 2017 rais Museveni kupitia mitandao ya kijamii alitoa taarifa kuwa lile bomba la mafuta litakaotoka nchini mwake kupitia Tanzania litaweza kupita kwenye baadhi ya maeneo nchini ambayo ni hifadhi ya barabara zetu

Majuzi hapa baada ya kukutana kwa raisi Museveni na Magufuli wamekubaliana mpango wa ujenzi wa bomba la mafuta kupitia nchini mwetu uendelee.

Hata hivyo sisi wananchi tungependa kujua

1. Je, kwa nini mkataba wa makubaliano baina yetu na Uganda katika suala hilo unakuwa siri?

2. Kama bomba linapita katika hifadhi ya barabara, je sheria ya hifadhi za barabara imezingatiwa vyema?

3. Tatu, Je, tukipitisha bomba hilo kwenye hifadhi za barabara je hatujifungi sisi wenyewe kushindwa kupanua barabara zetu?

4. Tumebomolea wananchi wetu maelfu kwa maelfu nyumba zao kisa wamejenga katika hifadhi za barabara, Je iweje leo tufunge macho kuhusu kupitisha bomba hilo kwenye hifadhi za barabara hizo wakati hizo hifadhi hazikutengwa makhsusi kwa ajili ya bomba hilo, Au ndo falsafa ya kuhusudu vitu ila linapokuja suala la watu hatujali?.

5. Tunataka kujua, ikitokea umwagikaji wa mafuta kwa bomba kutoboka au kupasuka njiani na uharibifu wa mazingira yetu ukatokea, ni nani atakuwa responsible kugharamia usafishaji wa mazingira na kulipa gharama za majanga ya moto kama ukitokea na kuunguza maelfu ya hekari za misitu na mimea yetu, nyumba na mali za wananchi!

6. Na katika maeneo ya wananchi ambayo hilo bomba litapita, wamewahusishaje wananchi ili kujua haki zao kabla ya kuwekeana mkataba?

Tunataka serikali iweke wazi mikataba ya rasilimali zetu inayoingia kwa niaba yetu

Hii hapa ni tweet ya Museveni akiishukuru serikali ya Tanzania kumpa hifadhi za barabara yake apitishe bomba!

Img-1600848924943.jpg
 
Road reserve sio kwa ajili ya barabara tu, road reserve kazi yake pia ni kama hiyo kupitisha mabomba.

Achana na hilo bomba la kwenda uganda, pia LINE ya haya mabomba ya maji majumbani hupita kwenye road reserve, mkongo wa mawasiliano hupita hapo, nguzo za tanesco hupita pia hapo na ndio maana kwa trunk road unaona kuna upana wa mita 45.

Hivyo kwa bomba hilo la mafuta kupita hapo wala sio shida na kwere.
 
Back
Top Bottom