Boniphace Bembele Ng'wita
JF-Expert Member
- Dec 25, 2013
- 3,446
- 1,812
Ni kufumba macho wakati roho mtakatifu anapowatokea wale kina mama wacha mungu.
Mkuu sasa mambo ya kutoa boriti sijui kibanzi yanahusiana nini na mada?? Yaani assume mimi naabudu mawe na nina boriti sijatoa jichoni mwangu pamoja na mabaya yote duniani je nikiuliza hili swali kuhusu biblia gani inafaa alafu wewe ukanipa huu mstari utakuwa umenisaidia kweli??Kukuuliza haina maana nimetoka nje ya mada. Sasa kwakuwa wewe ni mfuasi/muabudu mungu mwezi/makopo/Jiwe etc.
Jibu ni hili. Na mistari hii inakuhusu sana mtu kama wewe.
Matthew 7:3-5 King James Version (KJV)
3 And why beholdest thou the mote that is in thy brother's eye, but considerest not the beam that is in thine own eye?
4 Or how wilt thou say to thy brother, Let me pull out the mote out of thine eye; and, behold, a beam is in thine own eye?
5 Thou hypocrite, first cast out the beam out of thine own eye; and then shalt thou see clearly to cast out the mote out of thy brother's eye.
Hakuna kejeli hapo.Mkuu sasa mambo ya kutoa boriti sijui kibanzi yanahusiana nini na mada?? Yaani assume mimi naabudu mawe na nina boriti sijatoa jichoni mwangu pamoja na mabaya yote duniani je nikiuliza hili swali kuhusu biblia gani inafaa alafu wewe ukanipa huu mstari utakuwa umenisaidia kweli??
Baki kwenye mada umesema bible zote wapo sawa sasa huu mstari wa mathayo ukisoma Samaritan Bible haitambui kabisa kitabu cha mathayo hivo huu mstari sitouona je hadi hapo huoni Biblia haziwezi kuwa sawa?? Yaani ww unayesoma Mathayo mkristo wa Israel anakuona umepotoka sababu bible yake haitambui hizo 4 gospels sasa wote mpo sawa mkuu???
Embu tujikite kwenye mada kejeli zije baadae
Kama hoja imekushinda unaenda kujisomea alafu unarudi na majibu sio kulazimisha fikra zako ziwe sahihi ilihali hazina mashiko.Hakuna kejeli hapo.
Nimekuuliza swali la msingi sana. ili nikikujibu nikujibu kwa kile unachoamini ili unielewe.
Jibu lako limekuja la hovyo. Hiyo ndiyo size ya jibu lako PERIOD!.
Unaposema tusijadili WATU, kwani hivyo vitabu wanatumia MBUZI KUABUDU? Mbona unakuwa kama siyo Muislam?Kama hoja imekushinda unaenda kujisomea alafu unarudi na majibu sio kulazimisha fikra zako ziwe sahihi ilihali hazina mashiko.
Wewe jibu swali unaposema Biblia zipo sawa ilihali zinakinzana je kivipi zote ziwe halali
Mfano kuna Biblia hazitambui kabisa uwepo wa Yesu kama messiah sababu imefuta kabisa Gospels i.e. Samaritan Bible maana inatambua Torah pekee kama vitabu vitakatifu na vingine vyote ni BATILI!!
sasa ni vizuri ungeitetea hoja yako kwa upana kuliko kuhangaika na nachoamini mimi maana hakiwezi badili swali langu so tujadili muktadha sio WATU!
Kwanza hii mentality ya kila anayehoji Biblia kwamba lazima ni muislam imetoka wapi?? Mie huwa niko balanced sana na mijadala ya kidini nisome hapa navyoitetea Biblia soma kuanzia hiyo page mpaka mjadala ulipoisha.Unaposema tusijadili WATU, kwani hivyo vitabu wanatumia MBUZI KUABUDU? Mbona unakuwa kama siyo Muislam?
Swali langu kuhusu imani yako ndio linanipa uwanja mpana wa kukupa jibu kulingana na kile unachoamini. Kinyume na hapo huwezi kubali jibu langu sawa na ilivyo sasa! Maana tayari wewe unajibu lako.
La kwangu bado lipo pale pale. ZIPO SAWA KULINGANA NA UELEWA NA UFAHAMU WA MTUMIAJI!
Hata Shetani hujigeuza malaika wa Nuru apate kuwahadaa wanadamu!Kwanza hii mentality ya kila anayehoji Biblia kwamba lazima ni muislam imetoka wapi?? Mie huwa niko balanced sana na mijadala ya kidini nisome hapa navyoitetea Biblia soma kuanzia hiyo page mpaka mjadala ulipoisha.
Zifahamu siri 7 zilizofichika kuhusu sikukuu ya Pasaka - JamiiForums
2. Back to mada.... Unasema viko sawa kulingana na uelewa wa mwanadamu hapo nakubaliana na wewe 100%. Ila wote tunafahamu mawazo ya Mungu ndio tunatakiwa kuyafuata sio ya mwanadamu sasa basi mbele ya macho ya Mungu ni anafurahi kuona Biblia zikikinzana?? Je anawatreat wote sawa machoni pake??
Karibu
UTANGULIZI
Historia ya Biblia ya kikristo ni ndefu jinsi vitabu vilivyopatikana lakini ntaandika kwa kifupi sana na mengine tutaandaika tunavyozidi kuchangia kwenye uzi huu. Na pia nitoe rai mapema kuwa uzi huu sio wa kidini bali wa kielimu/historia hivyo sitegemei watu kurushiana matusi ya kuhusu dini sijui Mungu yupo au hayupo!! N.k
abu 73, waprotestant vitabu 66, Orthodox Tawahedo (Ethiopia) ina vitabu 81 hili limenifanya nifungue uzi ili tumalize mkanganyiko huu na naomba tusome taratibu na kwakuelewa mada inazungumzia nini kabla ya kuchangia kwa kuongozwa na ushabiki au mihemko.
Moderator[/USER] kina Active na Mhariri msihamishe uzi huu jukwaa la dini ili niweze kupata mawazo ya wana JF wote hta wasio na access na jukwaa la dini, nitashukuru kwa hilo.
Nimeona nilete maandiko ya wataalamu mbalimbali ili kwa wale walioamua kuchimba ukweli halisi wapate references za kutosha. Naomba tumsome huyu ambaye pia katoa historia ya Biblia vizuri sana.Shukrani mods kwa kuuachia mapema karibuni great thinkers mtupie maoni yenu
Mkuu MTAZAMO ahsante kwa kushare hilo bandiko la kisomi lakini kuna kitu muhimu sana amekiacha.
Hajaeleza je Canon ilikuwa fixed (maximum books) tokea enzi Biblia inaanza kuandikwa na wayahudi walipokuwa uhamishoni au kulikua na canon tofauti ukiachana na septuagint..... Maana kuna wakati wayahudi waliokuwa uhamishoni walitofautiana namba ya vitabu na wayahudi waliobaki/rudi Israel hasa baada ya kopi za kigiriki na kiebrania kuandikwa zikiwa na namba za vitabu tofauti na hapa ndio mzizi wa hoja. Ilitakiwa aeleze je ipi ilianza kabla ya ingine ili tujue nani ndio ana biblia halisi kati ya Greek septuagint au Hebrew masoretic.
2. Anasema pia Biblia ya catholic yenye vitabu 7 zaidi haikuwa challenged ila anasahau kuwa Padri Jerome alipotafsiri Biblia kutoka kiebrania kwenye kilatin (lugha ya kanisa) takribani miaka 1000 kabla martin luther hajazaliwa alivitenga vitabu vya Deuterocanonical kutoka main canon yaani hakuvipa hadhi sawa na vile vingine hivyo si kweli kuwa hivi vitabu 7 havikuwa challenged maana kama vinsingepingwa ina maana vingewekwa kwenye agano la kale kama vingine.
3. Ameongelea kuwa church fathers walivikubali. Hiyo hoja ipo too general anaposema church fathers bila kumtaja hata mmoja fathers kama origen,jerome,Athanasius na Cyril hawakuvitambua hivyo vitabu 7 vya wakatoliki sasa anaacha maswali kidogo.
4. Pia kaongelea tu catholic vs protestants canon hajaeleza kuwa hata kabla martin luther hajazaliwa kuna makanisa kama East orthodox yalikuwa na canon tofauti na catholic. Mfano Ethiopian Tawahedo Orthodox church walikuwa na canon ya vitabu 80+ tokea AD 400 ila ameruka hadi kwa martin luther kana kwamba kabla ya hapo makanisa yote yalikuwa na canon moja!!
HITIMISHO
Bandiko hilo bado limeacha utata juu ya suala hili maana halijajibu baadhi ya hoja tulizoibua humu
Shukrani
Nakubali mkuu kuwa KITABU CHA ENOCK kipo ingawa baadhi ya biblia zimekitoa.Umeandika vizuri japo kuna makosa kidogo ya kimtazamo umeyafanya mwanzoni mwa mada yako umeomba mjadala huu usijadiliwe kidini wakati unazungumzia kitabu cha dini nadhan sio sahihi kuijadili biblia na vitabu vyake kwakutumia historia,vitabu vya biblia hujadiliwa kwa kutumia maandiko ya Mungu Mwenyewe dhidi ya maandiko yake mwenyewe
Mfano.......
1.Mungu Mwenyewe kasema yeye sio mwandishi wa mkanganyiko (AUTHOR OF CONFUSSION)
1 wakolintho 14:33,soma biblia ya KJV ndio utapata maana nzuri zaidi '33 For God is not the author of confusion, but of peace, as in all churches of the saints " Kwahiyo kama Mungu kasema sio mwandishi wa kuchanganya bali wa amani kwa kanisa loote la watakatifu wake kamwe mkanganyiko wowote utakao husisha maandiko yake umetengenezwa na yule adui mwovu shetani kwa lengo la kuvuruga uelewa wa watu
2.Mungu sio mwanadamu mpaka aseme uongo
Hesabu 23:19
sasa kwakutumia hizo nguzo mbili hapo tunaweza tukavichambua vitabu hivyo vilivyozidi zaidi ya hapo 66 kwenye hiyo biblia ya kiprotestant kama ulivyoiweka, sasa kwa haraka haraka ipo hivi,maandiko mengi kwenye biblia yanatengeneza kitu kinaitwa "HARMONY" yaani yanatengeneza muunganiko flani mmoja yanaungana mkono na hayapingani yenyewe kwa yenyewesababu yoote yametoka kwa Mungu mmoja,mfano kuna zile amri 10 za Mungu kwenye kitabu cha kutoka 20,utakuta kuanzia pale hadi mwisho wa biblia vitabu vingine vinaendelea kuzirejea,kuzikumbushia,kuzisistiza nk kwahiyo kama kikitokea kitabu cha ziada cha hapo 66 kinatakiwa kiungane mkono pafectly na vitabu vingine 66!
1. Naanza na kitabu cha HENOKO(ENOCH)
Ukisoma kitabu cha Yuda 1:14 kinasema hivi "
"Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.
Sasa swali linakuja hivi huu unabii wa Henoko (yule aliyepaishwa na Mungu kwenda mbinguni) umeandikwa wapi katika biblia hiyo ya vitabu 66 mpaka nabii Yuda akaunukuu????,inamaana hadi huyu nabii Yuda anaunukuu kuna mahala umeandikwa kama vile tu walivyokuwa wananukuu torati ya Musa sababu iliandikwa kwenye vile vitabu vya Musa!
Ukweli ni kwamba kuna kitabu cha HENOKO na ndio kuna huu unabii amabo mtume YUDA alikuwa ananukuu,haya maneno ya YUDA hayapatikani popote kwenye biblia Henoko alipoyasema zaidi ya kwenye kitabu chake alichoandika .
itaendelea..
Mm ni mkristo kwenye dhehebu la Roman Catholic ila kuna wakati hata biblia naanza kuhisi imechakachuliwa balaa. Kibaya ni kwamba viongozi wanatetea nyufa zilizomo ndani ya baadhi ya mistari ya biblia.UTANGULIZI
Historia ya Biblia ya kikristo ni ndefu jinsi vitabu vilivyopatikana lakini ntaandika kwa kifupi sana na mengine tutaandaika tunavyozidi kuchangia kwenye uzi huu. Na pia nitoe rai mapema kuwa uzi huu sio wa kidini bali wa kielimu/historia hivyo sitegemei watu kurushiana matusi ya kuhusu dini sijui Mungu yupo au hayupo!! N.k
View attachment 993939
Prologue
Biblia ya kikristo ni mjumuiko wa vitabu mbalimbali vya manabii/Mitume wa Mungu ambao vimejumuishwa pamoja ili kutoa muongozo wa kiimani kwa wakristo kote ulimwenguni. Biblia inatambulika kama iliandikwa na vitabu kujumuishwa kwa uweza wa MUNGU hivyo ni kitabu kitakatifu, lakini kilichonishtua ni kugundua kwamba kati ya wakristo wanatumia Biblia tofauti kabisa yaani Wakatoliki Biblia yao ina vitabu 73, waprotestant vitabu 66, Orthodox Tawahedo (Ethiopia) ina vitabu 81 hili limenifanya nifungue uzi ili tumalize mkanganyiko huu na naomba tusome taratibu na kwakuelewa mada inazungumzia nini kabla ya kuchangia kwa kuongozwa na ushabiki au mihemko.
Historia
Wayahudi (Israel) walikuwa wanaandika maandiko wanayovuviwa na Mungu wao Yahweh tokea miaka 600 kabla ya Yesu na walikuwa na fixed canon ya vitabu 24 (39 ukivigawa) mpaka kipindi cha nabii wa mwisho Malachi 400 BC hivyo inasemekana ndio vitabu pekee vilivyokuwepo. kufikia karne ya 4 kabla ya kristo (KK) wayahudi waliokuwa uhamishoni hasa misri walitafsiri vitabu vya agano la kale vilivyoandikwa kiebrania kwenda kigiriki na kuzaa Biblia iliofahamika kama ''Septuagint''.... Biblia hii ilipata ushawishi sana kuliko ya kiebrania na ieleweke kwamba ni Biblia hii ndio imetumika mpaka na Yesu alipokuwa akinakili maandiko ya agano la kale kiufupi 70% ya quotes kutoka agano la kale kwenye vitabu vya Agano jipya vimetolewa kwenye Greek Septuagint. Kufikia hapa kukawepo na Biblia mbili kuu hivyo twende pamoja.
View attachment 993940
Mgogoro
Ikumbukwe Septuagint ilijumuisha vitabu vya kimafundisho ambavyo Hebrew bible haikuvitambua vitabu hivi vinajumuisha Macabees, Sirach,Wisdom of solomon n.k. Sasa ikafika mahali Septuagint (kigiriki) ikawa inatumika zaidi kuliko maandiko ya kiebrania (wayahudi) hivyo kwa mujibu wa mwanahistoria Heinrich Graetz ikabidi kikundi cha wayahudi kikutane kwa kilichoitwa council of Jamnia kilichofanyika 70 Baada ya kristo ambapo ndio kiliweka msimamo wa vitabu gani vya biblia ya kiebrania ndio vitambulike kwa wayahudi wote yote hii ili kuzuia upepo wa Biblia ya Greek sepruagint na hivyo hapa wakawa na msimamo wa vitabu vichache hasa vya agano la kale 39 tofauti na 46 vya septuagint. Hivyo tokea hapa madhehebu tofauti ya kikristo yakachukua Biblia mojawapo ya pande hizi mfano RC wao waliendelea na Greek Septuagint ambayo ndio ilitumiwa na mitume ila waprotestant wao waliamua kuendelea na Hebrew Bible wakiamini ndio halali na haijachakachuliwa pia madhehebu mengine kma Tawahedo Orthodox na mengineo yalikuwa na misimamo yao juu ya vitabu fulani hivyo utakuta baadhi ya makanisa yana vitabu kati ya hivyo 39 hadi 46 vya agano la kale.
Martin Luther
Karne ya 16 kiongozi wa wanamabadiliko/protestants walioamua kujitenga na ukatoliki Dr. Martin Luther naye aliamua kufanya tafsiri ya Biblia kwenda lugha ya kijerumani. Kiliandikwa 1520-34 na katika kuifanyia majumuisho naye alitaka kupunguza vitabu 7 vya agano jipya vikiwemo Ufunuo,Yuda,Waebrania na Yakobo n.k kwa kile alichokiita kwamba "havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu" na hata leo hii kwenye Luther bible cha waprotestant hivyo vitabu 4 vimewekwa vya mwisho kabisa katika biblia yao na nakala za mwanzoni viliwekwa kundi moja na vitabh vilivyoitwa ''apocrypha''.
Pia luther alikipinga vikali kitabu cha esther nakutaka kifutwe kutoka kwa Biblia. Alisema hakina uvuvio wa Roho mtakatifu maana hakuna mahala kinamtaja MUNGU!! Martin luther alipinga pia uwepo wa kitabu cha James/Yakobo kwenye Biblia sabau kwanza kiliandikwa karne ya 2 ambapo muandishi wanayedai ni Yakobo kaka yake yesu alishakuwa amekufa toka mwaka 67 BK hivyo aliona kma ni kilifojiwa tu.
View attachment 993938
HITIMISHO
Sasa baada ya kuwa nimepitia baadhi ya hoja za wana JF humu hasa zinazogusa maslahi ya kikristo huwa wana conclude kuwa Biblia haina makosa maana ilivuviwa na Roho mtakatifu sasa nilikuwa nataka wajuzi mnisaidia maswali yafuatayo
1.je kauli hii inapotolewa huwa ina maana ya Biblia ipi ambayo ilivuviwa na Roho?
2. Je Biblia gani ni halali
3. Manabii wanasema usiongeze au kupunguza neno kwenye Vitabu vyao sasa Je kama mmoja ndio yupo sahihi ina maana wengi wamepotoshwa??
4. Na kama wamepotoshwa je nini hatma ya ukristo kama wahuni wachache wanaweza ongeza maneno au kupunguza kwenye Biblia
5. Swali la mwisho naamini MUNGU anaona haya makosa Je ina maana karuhusu neno lake lipotoshwe?? Na kama sio kwanini mpaka sasa kaacha wahuni wachezee NENO lake.
Naomba kuwasilisha
Cc: ningeomba Moderator kina Active na Mhariri msihamishe uzi huu jukwaa la dini ili niweze kupata mawazo ya wana JF wote hta wasio na access na jukwaa la dini, nitashukuru kwa hilo.
nyufa hizo kama zipi ulizoziona ww? ziweke hapa tuzijadiliMm ni mkristo kwenye dhehebu la Roman Catholic ila kuna wakati hata biblia naanza kuhisi imechakachuliwa balaa. Kibaya ni kwamba viongozi wanatetea nyufa zilizomo ndani ya baadhi ya mistari ya biblia.
Divinity ya biblia inasidi kupotea kila baada ya muda unavyozidi kwenda....