Je, biblia imehalalisha mwanamke kuhubiri kanisani au kuwa mchungaji?

popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,012
Likes
2,529
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,012 2,529 280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,012
Likes
2,529
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,012 2,529 280
sasa mpk leo waarabu na watu wa mashariki ya kati wao wanaona ni mhimu mwanamke kufunika kichwa ALWAYS.........

tanzania hilo linawezekana?..........

siongei kishabiki, naongea vitu navijua HASA!!!...... there are things sisi hatuwezi kufuatisha namna wale waliishi..........

kuna habari za watumwa mle,sie tuna watumwa?.......

hence, uhitaji wa elimu ya theolojia, ili tutambue lipi linatakiwa kuwa applied tanzania or sub saharan to be precise, na lipi halitakiwi..........

THATS THE REASON KWANN PAULO ALIPELEKWA KWA MATAIFA NA SIO PETRO, MAANA PETRO HAKUTAKA KUZIWEKA KANDO TAMADUNI ZA KIYAHUDI, ALITAKA MATAIFA WAZIFUATE!!!!........

Paulo angetumia vitabu vya kiyahudi, ni wazi angewawekea kokwa wale wa mataifa ambao Injili imewajilia...... so ndugu, get to know the doctrine!
Huyu jamaa wa ajabu huyu,
Eti arabuni kuna watumwa Tanzania hakuna,
Halafu anajiita mtaalamu wa lugha na teolojia,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
2,235
Likes
2,075
Points
280
Age
49
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
2,235 2,075 280
Biblia, ukisoma kama maandishi ni kitabu kama vitabu vingine. Tena kwa hoja ya kimaandishi, mimi mwenyewe ni moja ya watu wanaojiuliza kuwa kulikuwa na vitabu vingapi duniani vilivyochambuliwa na kunyumbulishwa mpaka leo tuna biblia ya vitabu 72 kwa 66? Hali kadhalika wahusika wa huo uchambuzi ni kina nani? wakati mwingine huwa natamani kuwa bora vingeachwa vitabu vyooote ili tusome na tujue vitabu vyooooote. Hii ni kwa sababu kuna tafsiri kadha kadha katika biblia hizi tulizo nazo (vitabu 72 kwa 66) ndo maana kila kukicha kuna kanisa jipya kwa tafsiri mpya kabisa tena zenye upotofu wa hali ya juu kwa kisingizio cha Roho Mtakatifu.

Kwa ninachofahamu kwa elimu yangu ya bible knowledge ya O-level na divinity A-level, hatuwezi kutofautisha mafundisho yatolewayo ndani ya biblia na mila na tamaduni ya kiyahudi au mahali NENO linapofundishwa. Mf. kuna 'utata' hapo juu kuhusu maana ya ngamia kupenya tundu la sindano, kiuhalisia sio sindano hizi za kushonea nguo. Kulikuwa na eneo lenye njia nyembamba mnoo kiasi ngamia hawezi kupita mpaka ashushwe mizigo yote, akunjwekunjwe, asukumwe n.k. ndo apite, akifanikiwa kupita ndo arudishiwe mizigo ndo safari iendelee. Hilo eneo ngamia hupita kwa shida isiyoelezeka, ndo waliita kwa Kiswahili chetu 'tundu la sindano'. Tazama, ni andiko linaloreflect eneo la mahali Fulani ila lipo katika bible.

Naungana na wachangiaji waliopita kuwa theolojia ni muhimu sana kwa wahudumu wa makanisa yetu ya leo. Ili mtu aweze kutafsiri vizuri andiko Fulani, ni lazima uijue historia ya mwandishi na kinachozungumzwa katika mstari husika. Mf. ukisoma Marko, Luka na Matayo wote wanatofautiana juu ya rangi ya nguo aliyoteswa nayo Yesu. Hii haimanishi kuwa Yesu hakuwa na nguo wakati anateswa bali alivuliwa kabla hajapandishwa msalabani. Mtu mwingine anaweza akaja na hoja kuwa mwandishi Fulani ameongopa au ameandika kitu cha uongo, sivyo. Theme hapa sio rangi ya nguo bali ni kuvuliwa nguo (kudhalilishwa) kwa Yesu kabla hajapandishwa msalabani.

Biblia, ukisoma kama NENO, hautafuata ya mwilini. Tutakuwa na tafsiri kutoka kwa ROHO MTAKATIFU. Kama mtoa mada alivyonukuu maandiko, NENO haliangalii kimo, rangi, jinsia, kabila, etc vya walengwa. NENO huangaza roho imuelekee Mwenyezi Mungu muumba Mbingu na Dunia.

Nikirudi katika mada, ukisoma biblia kama maandishi yanavyosomeka, hoja ya wanawake kukatazwa kuhudumu madhabahuni haina majibu halisi, lakini ukisoma biblia kama NENO, majibu yapo mengi sana maana NENO huangaza ROHO na biblia inasema MUNGU NI ROHO NA WAMWABUDIO YAPASA KUMWABUDU KWA ROHO NA KWELI. Tofauti zetu za mwilini hazina maana yoyote kwa MUNGU.

Nawatakia uchangiaje mwema wa hii mada.
mkuu hongera kwa mchango........

afadhali wewe umelisemea hilo la ngamia na tundu la sindano, maana mie niliona naambiwa mara mtumishi wa tumbo n.k nikaamua nikae kimya!........

watu wanasoma biblia kama novel zingine ndio wanaleta tafsiri zao, au wengine wanakomalia neno kwa neno bila kujua that way mtu anaenda upotevuni...........

to them siku hizi hakuna Roho Mtakatifu, its very sad aisee
 
3 Angels message

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2017
Messages
1,359
Likes
2,092
Points
280
3 Angels message

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2017
1,359 2,092 280
Japo umedai injili yako siyo iliyoghoshiwa ila ulichoandika hakifanani na injili isiyoghoshiwa

Ofisi ya ukuhani kuanzia agano la kale mpk jipya kipindi cha Kristo kabla ya kufa msalabani haijawahi kuwa na mwanamke na hapa inabidi ujue tofauti kati ya kuhani na nabii mwanamke anaweza kuwa nabii ila kuwa kuhani hawezi sasa kutaka kuaminisha kuwa mwanamke anaweza kuhudumu kama Mchungaji ni upotoshaji wa wazi usioungwa mkono na maandiko maana mwanamke hawezi kuwa Mchungaji
 
little master

little master

Senior Member
Joined
Jul 16, 2018
Messages
162
Likes
191
Points
60
little master

little master

Senior Member
Joined Jul 16, 2018
162 191 60
Kuna vitu vipo wazi kabisa na haviitaji shahada kuvielewa. Mbona unapingana na maagizo ya Paul, Yeye kakataza na ipo wazi ila sawa kila mtu na mtazamo wake.

Maana tukiongea hamkawii kusema hatuna roho mtakatifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,012
Likes
2,529
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,012 2,529 280
Mtoto wa Baba

Mtoto wa Baba

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Messages
1,697
Likes
1,899
Points
280
Age
24
Mtoto wa Baba

Mtoto wa Baba

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2018
1,697 1,899 280
Alipewa daraka hilo baada ya Kristo au kabla ya Kristo,maana alipokuja Kristo alikuta taratibu za kale na hazikukokoma haraka ila baada ya mafundisho yake,naamini utanambia Huyu unaemsema alichaguliwa ama kusimikwa na Yesu km alivyowasimika akina Petro siyo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana huyu alikuwepo hata kabla ya yesu mkuu
Ukisoma biblia utagundua ni mmoja kati ya watu ambao walifurahia ujio wa yesu duniani yeye pamoja na Yule mzee Simeoni kama sijasahau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,012
Likes
2,529
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,012 2,529 280
Ndugu naomba kuuliza,
Kristo alizaliwa zama zipi,
Zama za Agano la kale ama zama za Agano jipya,
Hiki kifungu hakiongelei zama za Agano jipya japo kimeongelewa na Luka,
Pekua Biblia uone huyu mama alipata lini daraka hilo,
Na inaongelea wakati Kristo bado kichanga kabisa,na zilizokuwa zinafanya kazi ni destuli za wayahudi,destuli za Agano la kale,hata kusali ilikuwa jmosi,hapo chini wameongelea kutairi km destuli ya wayahudi,
Tunaposema Agano jipya na mpangilio wa daraka ama daraja ama nafasi tunamaanisha zilizowekwa/kuteuliwa na ama Kristo mwenyewe ama mitume baada ya Kristo,
Kifupi hilo fungu ni la taratibu za kale,taratibu za Agano lililokuwa kuu kuu,taratibu za Agano lililokuwa karibu na kutoweka,taratibu za Agano lilikuwa na mapungufu maana lisingekuwa na mapungufu lisingekuja la pili,taratibu za zama za kuenenda kwa mwili na sheria za mwili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,012
Likes
2,529
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,012 2,529 280
mkuu hongera kwa mchango........

afadhali wewe umelisemea hilo la ngamia na tundu la sindano, maana mie niliona naambiwa mara mtumishi wa tumbo n.k nikaamua nikae kimya!........

watu wanasoma biblia kama novel zingine ndio wanaleta tafsiri zao, au wengine wanakomalia neno kwa neno bila kujua that way mtu anaenda upotevuni...........

to them siku hizi hakuna Roho Mtakatifu, its very sad aisee
Ninyi ndo mnasoma kwa tafsiri za kuambiwa kwenye semina,kifupi hamjui maana haswa ya neno,mnajua tafsiri zinazopingana za kulishwa na wasaka tonge,
Acheni Kumsingizia Roho Mtakatifu,
Mnaliaibisha kanisa,mngekuwa mnaongozwa na Roho mtakatifu na siyo kuongozwa na tamaa za kujaza matumbo mnaojiita wa kiroho msingekuwa mmegawanyika gawanyika na msingekuwa mnapingana,mngekuwa wamoja maana imeandikwa mahali Fulani hivi kuhusu kuwa wamoja na kunia mamoja km alivyo Kristo na Baba,sasa hii kila mtu kuwa kivyake ndo maongozo ya Roho mtakatifu,Roho mtakatifu siyo wa utengano wala wa vita wala wa husuda wala wa wivu wala wa chuki yote haya yamejikita makanisani kwenu,
Mnampima Roho mtakatifu kupitia makelele na fujo na watu kuangushwa kwa nguvu chini,
Injili mnayohubiri ni ya kuwajaza watu matumaini hewa na utajiri,hakuna hata siku mnakazia masomo juu ya manabii wa uongo waliotabiriwa zama hizi maana mnajua inawagusa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,012
Likes
2,529
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,012 2,529 280
Kuna vitu vipo wazi kabisa na haviitaji shahada kuvielewa. Mbona unapingana na maagizo ya Paul, Yeye kakataza na ipo wazi ila sawa kila mtu na mtazamo wake.

Maana tukiongea hamkawii kusema hatuna roho mtakatifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na maagizo ya Paulo siyo yake ni ya Kristo,
Yani jamaa huwa wakiambiwa kwa makelele kuwa Ppooookea Pokeaaaa!,basi wanajijaza hisia Kali wanadhani ndo nguvu ya Roho mtakatifu,anzia hapo huwa wanajiaminisha kuwa kila wafanyacho ni sahihi na anafanya Roho,hata wakati wa Deci walimsingizia Roho,yule mchungaji mmama aliyenaswa anasukuma mtu na kumkonyeza apige kelele nae ni Roho,kibwetele,hata babu wa loliondo walisema kazi ya Roho mtakatifu,
Kifupi wanamtukanisha Roho mtakatifu sababu ya ujinga na kusaka sadaka,Roho mtakatifu kaanza kutafsiriwa kwa ishara za vurugu,wakati Biblia inaonesha kabisa upole,hekima na uwezo wa Roho mtakatifu,hata Yesu hakuwa anapayuka wala kupigisha watu makelele wala kusukuma watu vichwani alipokuwa anawavuvia Roho mtakatifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
J

jopss

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
240
Likes
320
Points
80
J

jopss

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
240 320 80
Kwenye biblia sikuwahi kuona mwanamke akiwa kuhani, Nabii Wa mtume , sijui ni kwa nn ilikuw vile, Maana hata Yesu pamoja na kumheshimu Mama Maria, hakuwahi kuteua hata mtume Wa jinsia ya Kinamama.
Wenye ufafanuzi na uelewa Wa haya mambo Atupe elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye Biblia kuna Nabii mwanamke mkuu. Anaitwa HULDA

2 Mambo ya Nyakati 34:22
Basi Hilkia, na hao waliotumwa na mfalme, wakamwendea HULDA NABII MKE, mkewe Shalumu, mwana wa Tohathi, mwana wa Hasra, mtunza mavazi; (naye alikuwa akikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili); wakasema naye kama hayo.

Na mwingine ni DEBORAH

Waamuzi 4:4
Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,012
Likes
2,529
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,012 2,529 280
SMART PASSENGER

SMART PASSENGER

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Messages
556
Likes
371
Points
80
SMART PASSENGER

SMART PASSENGER

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2018
556 371 80
Kwenye biblia sikuwahi kuona mwanamke akiwa kuhani, Nabii Wa mtume , sijui ni kwa nn ilikuw vile, Maana hata Yesu pamoja na kumheshimu Mama Maria, hakuwahi kuteua hata mtume Wa jinsia ya Kinamama.
Wenye ufafanuzi na uelewa Wa haya mambo Atupe elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
SOMA kitabu kwenye biblia kinaitwa waamuzi

Waamuzi 4:4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
L

Lami

Senior Member
Joined
Jan 1, 2014
Messages
102
Likes
25
Points
45
L

Lami

Senior Member
Joined Jan 1, 2014
102 25 45
Acha uzushi,
Ngamia ni ngamia na tundu la sindano ni tundu la sindano,
Hakuna mahali panaitwa tundu la sindano ktk mazingira aloishi Yesu,waulize walowahi enda hija watakujuza,
Tafuta Biblia hata za zamani za lugha yyte ambayo tafsiri ya kiswahili ilinyonywa humo uone km maana ni hyo usemayo,
Wengine nao wanamaana nyingine eti ngamia anaeongelewa hapa si ngamia mnyama,
Yani kila msaka tonge anakuja na tafsiri yake,

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila kukukashifu wewe mhusika wala post yako, fahamu kwamba Israel ya leo hii ni nchi mpya kabisa iliojengwa baada ya vita nyingi kupiganwa katika eneo hilo na kuleta uharibifu kadha wa kadha. Maeneo mengi ya manabii na mitume hayapo leo, maana yake ni kuwa sehemu (areas) chache sana zina majina yaleyale tokea wakati wa manabii na mitume. Mifano ipo mingi nitatoa michache. Leo hii kuna mji unaitwa Tel Aviv huko Israel, kipindi cha manabii na mitume hakukuwa na huo mji. Vivo hivyo kuna miji na sehemu zilikuwepo zamani leo hazipo. Mf. Hakuna yoyote alieenda Israel akaonyeshwa pasina shaka kaburi la Yesu lilipokuwepo, HAKUNA.
Elewa tu kwamba Yesu mwenyewe alitabiri kupigwa na kuanguka (kupelekwa utumwani) kwa Israel, hivyo miji mingi ya Israel ya zamani imekosa mwendelezo wake and vice versa is true.
Hivyo, kwa habari ya eneo la Tundu la Sindano, hiyo sehemu kwa sasa haipo, lakini ukisoma biography za sehemu na watunzi mbalimbali wa vitabu vya kale vinadhibitsha uwepo wa hiyo sehemu.
 
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2017
Messages
2,856
Likes
2,776
Points
280
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2017
2,856 2,776 280
Angalieni sio kwa jazba bali kwa utulivu kabisa kwenye tovuti ya Youtube

Andika
" Healing and Derivarence by Evangelist Yinka "

Halafu angali Clip yote na sio nusu na sio kwa MUHEMUKO

Yinka ni Mwanamke, Halafu Semeni anachofanya ni Kipawa Cha Roho Mtakatifu au la.

Note
Nimesema angalieni kwa utulivu halafu toeni maoni yenu bila ya Jazba wala matusi.
Nataka watu wenye busara ndio waseme.
Kama sio unasema tu sio, kama ndio unasema ndio na sababu zake uziseme
Hivyo ndivyo wenye hekima wanavyojadiliana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hanitoni

Hanitoni

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2015
Messages
1,048
Likes
821
Points
280
Hanitoni

Hanitoni

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2015
1,048 821 280
Ngamia ni zile kamba nene zilizokuwa zinatumika katika uvuvi ni nene sana.pia zilitumika hata katk majahazi na kuweka nanga sasa kamba km ile inawezaje kupenya kwenye tundu la sindano????
Biblia, ukisoma kama maandishi ni kitabu kama vitabu vingine. Tena kwa hoja ya kimaandishi, mimi mwenyewe ni moja ya watu wanaojiuliza kuwa kulikuwa na vitabu vingapi duniani vilivyochambuliwa na kunyumbulishwa mpaka leo tuna biblia ya vitabu 72 kwa 66? Hali kadhalika wahusika wa huo uchambuzi ni kina nani? wakati mwingine huwa natamani kuwa bora vingeachwa vitabu vyooote ili tusome na tujue vitabu vyooooote. Hii ni kwa sababu kuna tafsiri kadha kadha katika biblia hizi tulizo nazo (vitabu 72 kwa 66) ndo maana kila kukicha kuna kanisa jipya kwa tafsiri mpya kabisa tena zenye upotofu wa hali ya juu kwa kisingizio cha Roho Mtakatifu.

Kwa ninachofahamu kwa elimu yangu ya bible knowledge ya O-level na divinity A-level, hatuwezi kutofautisha mafundisho yatolewayo ndani ya biblia na mila na tamaduni ya kiyahudi au mahali NENO linapofundishwa. Mf. kuna 'utata' hapo juu kuhusu maana ya ngamia kupenya tundu la sindano, kiuhalisia sio sindano hizi za kushonea nguo. Kulikuwa na eneo lenye njia nyembamba mnoo kiasi ngamia hawezi kupita mpaka ashushwe mizigo yote, akunjwekunjwe, asukumwe n.k. ndo apite, akifanikiwa kupita ndo arudishiwe mizigo ndo safari iendelee. Hilo eneo ngamia hupita kwa shida isiyoelezeka, ndo waliita kwa Kiswahili chetu 'tundu la sindano'. Tazama, ni andiko linaloreflect eneo la mahali Fulani ila lipo katika bible.

Naungana na wachangiaji waliopita kuwa theolojia ni muhimu sana kwa wahudumu wa makanisa yetu ya leo. Ili mtu aweze kutafsiri vizuri andiko Fulani, ni lazima uijue historia ya mwandishi na kinachozungumzwa katika mstari husika. Mf. ukisoma Marko, Luka na Matayo wote wanatofautiana juu ya rangi ya nguo aliyoteswa nayo Yesu. Hii haimanishi kuwa Yesu hakuwa na nguo wakati anateswa bali alivuliwa kabla hajapandishwa msalabani. Mtu mwingine anaweza akaja na hoja kuwa mwandishi Fulani ameongopa au ameandika kitu cha uongo, sivyo. Theme hapa sio rangi ya nguo bali ni kuvuliwa nguo (kudhalilishwa) kwa Yesu kabla hajapandishwa msalabani.

Biblia, ukisoma kama NENO, hautafuata ya mwilini. Tutakuwa na tafsiri kutoka kwa ROHO MTAKATIFU. Kama mtoa mada alivyonukuu maandiko, NENO haliangalii kimo, rangi, jinsia, kabila, etc vya walengwa. NENO huangaza roho imuelekee Mwenyezi Mungu muumba Mbingu na Dunia.

Nikirudi katika mada, ukisoma biblia kama maandishi yanavyosomeka, hoja ya wanawake kukatazwa kuhudumu madhabahuni haina majibu halisi, lakini ukisoma biblia kama NENO, majibu yapo mengi sana maana NENO huangaza ROHO na biblia inasema MUNGU NI ROHO NA WAMWABUDIO YAPASA KUMWABUDU KWA ROHO NA KWELI. Tofauti zetu za mwilini hazina maana yoyote kwa MUNGU.

Nawatakia uchangiaje mwema wa hii mada.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hanitoni

Hanitoni

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2015
Messages
1,048
Likes
821
Points
280
Hanitoni

Hanitoni

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2015
1,048 821 280
Ngamia ni zile kamba zilizokuwa zinatumika ktk uvuvi na kwenye majahazi
Acha uzushi,
Ngamia ni ngamia na tundu la sindano ni tundu la sindano,
Hakuna mahali panaitwa tundu la sindano ktk mazingira aloishi Yesu,waulize walowahi enda hija watakujuza,
Tafuta Biblia hata za zamani za lugha yyte ambayo tafsiri ya kiswahili ilinyonywa humo uone km maana ni hyo usemayo,
Wengine nao wanamaana nyingine eti ngamia anaeongelewa hapa si ngamia mnyama,
Yani kila msaka tonge anakuja na tafsiri yake,

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,262,459
Members 485,588
Posts 30,122,935