Je, biblia imehalalisha mwanamke kuhubiri kanisani au kuwa mchungaji?


jangala

jangala

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Messages
1,349
Likes
1,837
Points
280
jangala

jangala

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2014
1,349 1,837 280
Mtoa post kaa utafakari ni amri ngapi leo hii umezivunja ktk amri kumi za Mungu?
Ukipata jibu kisha ujiulize kuwa KAMA UMESHINDWA KUTOVUNJA AMRI ZA MUNGU, UNAPATA WAPI UWEZO WA KUKOSOA WENGINE ILIHALI WW MWENYEWE SIO MSAFI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
2,235
Likes
2,075
Points
280
Age
49
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
2,235 2,075 280
Kwa hyo Tanzania yakitokea matatizo km ya wale hakipaswi kitabu hicho kufundishia sababu tu haikuwahusu watanzania siyo,
Nadhani sasa imefika mahali kanisa la Tanzania kitamaduni na tabia hatuendani kabisa na tamaduni historia na tabia za wooote walioaswa jambo Fulani ktk Biblia,
Hii iliyoangazia asili na tabia za wasio watanzania tuiache maana tunapaswa kunukuu kufuatana na tabia na tamaduni za watu mahalia

Sent using Jamii Forums mobile app
sasa mpk leo waarabu na watu wa mashariki ya kati wao wanaona ni mhimu mwanamke kufunika kichwa ALWAYS.........


tanzania hilo linawezekana?..........

siongei kishabiki, naongea vitu navijua HASA!!!...... there are things sisi hatuwezi kufuatisha namna wale waliishi..........


kuna habari za watumwa mle,sie tuna watumwa?.......


hence, uhitaji wa elimu ya theolojia, ili tutambue lipi linatakiwa kuwa applied tanzania or sub saharan to be precise, na lipi halitakiwi..........


THATS THE REASON KWANN PAULO ALIPELEKWA KWA MATAIFA NA SIO PETRO, MAANA PETRO HAKUTAKA KUZIWEKA KANDO TAMADUNI ZA KIYAHUDI, ALITAKA MATAIFA WAZIFUATE!!!!........


Paulo angetumia vitabu vya kiyahudi, ni wazi angewawekea kokwa wale wa mataifa ambao Injili imewajilia...... so ndugu, get to know the doctrine!
 
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2017
Messages
2,856
Likes
2,777
Points
280
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2017
2,856 2,777 280
Mstari unaanza kwa kusema hata baada ya hayo,
Anza kwanza kujua hayo yepi,
Halafu Agano jipya lilikuwa maandalizi ya agano jipya,unaanzaje kuchukua maagizo ya njiani ukakataa maagizo ya mwisho ama ya ukamilifu,
Km ndivyo basi tusibague,tuchukue yote ya agano la kale tuyafuate,
Halafu ndugu acha ujinga wa kudhani kila muujiza ni kazi ya Roho mtakatifu,sijui nani kawaroga ninyi hadi mnapima uwepo wa Roho mtakatifu kwa miujiza

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2017
Messages
2,856
Likes
2,777
Points
280
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2017
2,856 2,777 280
Kinachoongelewa siyo kuthaminiwa,
Asiyemthamini mwanamke huyo ni mjinha zaidi ya ujinga,
Kinachoongelewa ni maagizo ya kuongoza kanisani,km ambavyo mtume Paulo katuonya,
Ama tuseme hivi mtume Paulo aliongopa ila ninyi ndo wakweli,
Halafu naomba unisaidie jambo moja,nipe mahala panapomuingelea Nabii Esther agano jipya nipasome

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa kuniuliza swali uliloninukuu nikisema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2017
Messages
2,856
Likes
2,777
Points
280
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2017
2,856 2,777 280
Kinachoongelewa siyo kuthaminiwa,
Asiyemthamini mwanamke huyo ni mjinha zaidi ya ujinga,
Kinachoongelewa ni maagizo ya kuongoza kanisani,km ambavyo mtume Paulo katuonya,
Ama tuseme hivi mtume Paulo aliongopa ila ninyi ndo wakweli,
Halafu naomba unisaidie jambo moja,nipe mahala panapomuingelea Nabii Esther agano jipya nipasome

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesema nikupe andiko katika Agano Jipya linalosema kuwa Esther ni Nabii...!
1.Wewe hilo wazo umelitoa wapi ?
2. Aliyekuambia Esther ni Nabii kwa mujibu wa Agano Jipya ni nani ?
3. Mimi nahusika vipi na hilo swali lako ?Sent using Jamii Forums mobile app
 
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2017
Messages
2,856
Likes
2,777
Points
280
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2017
2,856 2,777 280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,013
Likes
2,531
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,013 2,531 280
ni kweli ndugu,.....


kuna mtu alifafanua ile kauli ya "ni rahisi ngamia kupita ktk tundu la sindano kuliko tajiri kurithi ufalme" katika namna ambayo ilinishangaza.........


sasa kauli km hio, kwa mty asiejua historia ya ule ufalme miaka ile atatoa tafsiri ya ajabu kabisa.........


the same na ile kauli ya Yohana mbatizaji "tazama mwana kondoo wa Mungu..." kumbe alitamka vile ili kufit audience yake! ila watu wa leo ni wao na Roho Mtakatifu..... ndio maana watu wanakaa miaka 10 church lkn bado wachanga kiroho!
Tafsiri za kutunga hizo,ambazo kiiila uchwao zinakuja kadri watumishi matumbo wanavyoibuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sundoka

sundoka

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2011
Messages
1,091
Likes
914
Points
280
sundoka

sundoka

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2011
1,091 914 280
Sehemu ya kwanza

Mistari muhimu ya kukumbuka:-

1 WAKORINTHO 14:34-36:-

34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.

35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.

36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?


1 TIMOTHEO 2:11-12:-

11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.


HII NI MADA YENYE UBISHI MKUBWA miongoni mwa vichwa vya watu wengi . Na maandiko hayo kwa kueleweka isivyo sahihi hutumiwa na baadhi ya watu wengi kujaribu kujenga hoja zao za kupinga kwamba mwanamke hana haki yoyote ya kuwa Mchungaji wala kusimama madhabahuni kuwahubiria watu kanisani.

Jambo hili limeleta mzozano mkubwa na mpasuko ndani ya makanisa mengi ya Mungu, kuhusu uhalali wa mwanamke kuhubiri madhabahuni na kuwa Mchungaji. Kuna mawazo ya positive na Negative, kuna wengine wanaona ni sahihi na kuna wengine kwao siyo sahihi kabisa .

Sasa basi ukweli na usahihi wa maandiko hayo ni upi basi? Je, ni sahihi kwamba mwanamke hatakiwi kuhubiri madhabahuni kanisani au kuwa Mchungaji ? Tatizo ni kwamba Maandiko hayo hayaeleweki vizuri kwa kwa wakristo wengi na hata baadhi ya wachungaji na Maaskofu, wanalifafanua hilo Andiko kwa maana potofu kabisa .

NB:-

Kuitwa Mtume, Nabii Askofu au Mchungaji n.k. Siyo kigezo kikubwa cha kwamba wewe unaielewa sana Biblia kwa usahihi wake. La asha ! Ndiomaana wako hata wachungaji wengine tena wengi tu ambao huyatafsiri maandiko isivyo na kuyapotosha kwa tamaa zao wenyewe.

MWALIMU MKUU WA BIBLIA NI ROHO MTAKATIFU; yeye ndiye aliyeyaleta maandiko hayo kwetu. Na hatuwezi sisi kuamua kuyatafsiri maandiko hayo vyovyote tu kama apendavyo mtu fulani kutafsiri. La Asha
[ 2 PETRO 1:19-20 ] .
Bali katika kanuni za kuyatafsiri maandiko, tunahitaji sana maongozi ya msaada wa Roho Mtakatifu mwenyewe katika kuyasoma na kuyaelewa maandiko vizuri na kuyatafsiri kwa usahihi wake. Neno la Biblia. Tunaweza kulifaham kwa kufunuliwa na Roho Mtakatifu pekee yake. Ndiomaana Yesu alisema uliwaficha wenye hekima na Akili (Wasomi), ukawafunulia watoto wachanga (Watu wasio na elimu) . Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza mbele zako [ MATHAYO 11:25-26]. "Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho Mtakatifu . Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu " .
[1 WAKORINTHO 2:10-15].

Si hilo tu. Nikodemo alikuwa ni mwalimu mkuu wa chuo cha Torati. Na watu walimwamini sana katika Taifa la Israeli. Lakini Nikodemo alipoambiwa na Yesu maneno mepesi tu ya Mungu , na usomi wake wote, alishindwa kuyaelewa maana yake nini !! Sasa Yesu ambaye hakupita chuo chochote cha Theolojia, ikambidi amfundishe Nikodemo, mwalimu mkuu wa chuo cha Theolojia ya Torati.
[ YOHANA 3:1- 10 ]

Sisemi wala kupinga kwamba kusoma chuo cha Biblia ni kosa au ni vibaya, au ni dhambi. Hapana. Ni nini maana ya kuanza kukwambia hayo. Maana yangu ni hii kwamba :- Ondoa dhana potofu ukafikili kila mtu anayeitwa Mchungaji, Askofu au Mwanatheolojia fulani msomi anaielewa sana Biblia ki-maana. Ukiwa na mawazo hayo tu, utapotezwa na kudanganyika sana Mpendwa . Na Mungu huwa hatendi kazi kwa misingi hiyo. Mchungaji /Ev/ Mwanatheolojia huyo Anaweza kuielewa Biblia kwa namna fulani tu ya akili hivi , lakini asiweze kabisa kuielewa Biblia kwa jinsi ya rohoni zaidi kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu . Na maana ya kweli ya maneno ya Biblia hutumbalikana kwa jinsi ya rohoni zaidi na sio kwa jinsi ya mwilini.
[ WAGALATIA 1:11-12 ; WAEFESO 1:17-19].

Hivyo ni vema zaidi tusiweke vipimo vyetu vya usomi kama kigezo cha kuitafsiri Biblia; bali tumuhitaji sana Roho wa Mungu ndio atuongoze katika kulitafsiri Neno lake Mungu.

Je, ni halali Mwanamke kuhubiri au kuwa Mchungaji?

Jibu :- Ni ndiyo kwa herufi kubwa.

Tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele vinne. Ambavyo ni :-

(1) HOJA POTOFU KUHUSU MWANAMKE KUTOKUWA MCHUNGAJI / MUHUBIRI.

(2) UHALALI WA MWANAMKE KUHUBIRI / KUFUNDISHA KANISANI .

(3) UHALALI WA MWANAMKE KUWA MCHUNGAJI

(4) UFAFANUZI WA ANDIKO LA 1 WAKORINTHO 14:34-35 NA 1 TIMOHEO 2:12 .

KIPENGELE NO:1

HOJA POTOFU KUHUSU MWANAMKE KUTOKUWA MCHUNGAJI/ MUHUBILI .

Ukiwasikia watu wengi wanaopinga mwanamke kuhubiri au kuwa Mchungaji. Mbali na kutumia Andiko la 1 Wakorintho 14:34-35 na 1 Timoheo 2:12-15 katika ufafanuzi wao .

Pia watajenga hoja yao nyingine ni kwamba MWANAMKE NI KIUMBE DHAIFU na hivyo wataeleza mengi tu katika kufafanua hoja yao hii.

Lakini mbele za Mungu, hoja ya mwanamke kutokuhubiri au kuwa Mchungaji kwa sababu eti ni kiumbe dhaifu. Hoja kama hii haikubaliki na wala haina maana yoyote. Kwa sababu Biblia inasema kwamba Hao hao watu walio dhaifu machoni petu ndio Mungu anayewachagua kuwa watumishi wake . Neno la Mungu linasema katika

1WAKORINTHO 1: 26-29:-" Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; TENA MUNGU ALIVICHAGUA VITU VINYONGE VYA DUNIA NA VILIVYODHARAULIWA (WANAWAKE), naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu."

Kwa maana hiyo ni muhimu kuzidi kuelewa na kufaham vizuri kwamba siku zote Mungu huwa hamchagui mtu yoyote kuwa mtumishi wake katika ngazi yoyote ya utumishi wa kihuduma kwa sababu tu ya kigezo cha jinsia yake kwamba ni kike au kiume. Hapana. Mungu hachagui mtu yoyote kwa kigezo cha sifa, umri, cheo au jinsia yake. Mungu huwa hatumikiwi wala kutenda kazi kwa misingi hiyo. Biblia inatuambia katika

1 SAMWELI 16:7-10 :-

7. Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA HAANGALII KAMA BINADAMU AANGALIAVYO; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

8. Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, BWANA hakumchagua huyu .

9. Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala BWANA hakumchagua huyu .

10. Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, BWANA hakuwachagua hawa .

WAFILIPI 3:3-4:-"Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, WALA HATUUTUMAINI MWILI. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi."

Kwa sababu hiyo. Mungu katika mpango wake anaweza kumchagua mtu yoyote yule bila kujali sifa yake, umri wake au jinsia yake kwamba ni mwanamke au mwanaume , Mungu anaweza kumchagua awe mtumishi wake katika ngazi yoyote ya utumishi na tena akamtumia kwa viwango visivyo vya kawaida. Kwa hiyo sisi wanadamu hatupaswi kuamua kumpangia Mungu kwamba mwanamke hawezi kuwa Mchungaji au muhubiri. Kivipi !? TUSILETE MFUMO-DUME NDANI YA KANISA LA MUNGU . Hilo ni chaguo la Mungu sio la kwako wewe mwanadamu. Na kwa maana hiyo Mungu akiamua kumchagua mwanamke kuwa Mchungaji, Askofu, Mwinjilisti, mtume, Nabii n. k. Atakuwa hivyo Mchungaji, mtume, Nabii na kadhalika. Biblia inasema katika

WARUMI 9:11-16 :-"
(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye) , aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia. Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!
Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu."

WAEBRANIA 5:4:-" Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ILA YEYE AITWAYE NA MUNGU , kama vile Haruni ".

Na kwa maana hiyo. Ngazi yoyote ya utumishi katika huduma mtu huwekwa na Mungu . Mungu akiamua kumwita mwanamke awe mchungaji, atakuwa ni Mchungaji tu na Mungu atajidhihirisha kwake kwa kumthibitisha kwamba yeye ndiye aliyemuita. Wako wachungaji wanawake na wahubiri duniani ambao Mungu anawatumia kwa viwango vya juu sana katika huduma zao . Hatuwezi kukanusha na kupinga utumishi wao kwa sababu tu ya kijinsia. Yesu alisema kama hamniamini mimi, ziamini zile kazi , kwa kuwa kazi zenyewe zanishuhudia ya kwamba Baba Mungu amenituma .
[ YOHANA 5:36; YOHANA 10:25, 36-38; YOHANA 14:10-12].

HOJA YAO YA PILI.

Watasema hata maandiko yanamtaja kwamba mwanaume ndiye anayepaswa kuwa Mchungaji (Askofu). Uaskofu ni ngazi ya juu ya madaraka ya kichungaji .

Na watatumia Andiko lao hili lifuatalo katika
1 TIMOHEO 3:1-12:-

1-7. Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu , atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, MUME(MWANAUME) wa mke mmoja , mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)
Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.

8-12. Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu; wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
Mashemasi na wawe WAUME wa mke mmoja , wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu. "

Ni muhimu kuelewa vizuri Andiko hilo kwa kusema mwanaume hapo ndiwe Askofu . Haimanishi kwamba basi limemkataza Mwanamke asiwe mchungaji au Askofu. Hapana. Kwa sababu ukitazama mukadha mzima wa maelezo yote ya Andiko nzima, yameendelea kusema pia " MASHEMASI NA WAWE WAUME wa mke mmoja " . Sasa Je, kwa kusema hivyo tuseme Paulo Mtume hapo hakuwaruhusu pia wanawake wasiwe washemasi kwa sababu tu amewataja wanaume? Jibu ni hapana.

Tunaona pia walikuwepo MASHEMASI WANAWAKE ambao pia Paulo mtume aliwachagua katika kanisa. Ukisoma katika WARUMI 16:1 , Biblia inasema:- " Namkabidhi kwenu Fibi, Ndugu yetu, aliye muhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea" . Mstari huo katika Biblia ya kingereza ya New International Version , unasomeka hivi, Romans 16:1:-" I commend to you our Sister Phoebe, a Servant (deaconess) of the church in Cenchrea" .

Kwa hiyo tunaona hapo juu ya Shemasi Mwanamke ingawa katika Waraka wa Timotheo wanatajwa tu kuwa mashemasi wanaume tu. Kwa maana hiyo tunapata kuelewa kwamba Andiko la 1 TIMOTHEO 3:1-12 , Ingawa liliwataja maaskofu na mashemasi kuwa wanaume hapo , lakini hakumaishi kwa wanaume tu pekee yao , bali hata wanawake pia wanaweza kuwa mashemasi, na vilevile wachungaji (maaskofu) pia kwa msingi huo.

Ni muhimu kuyaelewa maandiko ya Biblia vizuri sio kila mahali andiko linapotaja jambo kwa upande mmoja linamainisha tu kwa upande mmoja pekee yake . Hapana. Linaweza kutajwa kwa upande mmoja, lakini halikumainishi kuishia tu kwa upande mmoja, bali kwa pande zote mbili . Kwa mfano , Yesu alisema, kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake [ MATHAYO 5:27-28].

Sasa Swali la ufaham :- Andiko hilo hapo linamgusa tu mwanaume kumtamani mwanamke ndio dhambi. Lakini Je, tuseme mwanamke naye akimtamani mwanaume kiuasherati, itakuwa siyo dhambi? Kwa sababu tu eti Andiko hilo limemtaja tu mwanaume hapo? Jibu ni la!

Na kwa msingi huo huo hata kama Biblia imewataja wanaume kuwa ndio wawe maaskofu na mashemasi. Neno hilo halikuishia kumainisha tu kwa wanaume pekee yao bali hata kwa wanawake pia wanaweza kuwa wachungaji au maaskofu, mashemasi, mitume, manabii n.k.

Ni muhimu kufaham Biblia inasema katika MATENDO 10:34-35:-

" Petro akafumbua kinywa chake, akasema, HAKIKA NATAMBUA YA KUWA MUNGU HANA UPENDELEO; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. "

Kusema kwamba mwanaume tu ndio anayepasa kuhubiri na kuwa Mchungaji lakini mwanamke hafai kwa lolote. Huo ni upendeleo. Mungu wetu hana upendeleo wa aina yoyote ile , kila mtu awe ni mwanaume au mwanamke bado Mungu anaweza kuwatumia wote sawasawa katika nafasi yoyote ile ya utumishi iwe ni uchungaji na kadhalika.

Ni muhimu kufaham katika suala la utumishi wowote mbele za Mungu. Mwanaume hawezi kujivuna na kujiinua kwamba yeye anastahili sana zaidi ya mwanamke. Katika imani ya wokovu iliyobeba utumishi ndani yake, sisi wote ni sawasawa mbele za Mungu. Hakuna mmoja aliye bora wa kujiinua juu zaidi ya mwingine. Biblia inasema katika

1 WAKORINTHO 12:17-27:-

" BALI MUNGU AMEVITIA VIUNGO KILA KIMOJA KATIKA MWILI KAMA ALIVYOTAKA . Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi. Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana . Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe . Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho . Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza.............."

YOHANA 6: 28-29:-
"Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate KUZITENDA KAZI ZA MUNGU ? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye."

WAGALATIA 3:26-29:-

"Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. HAPANA MTU MUME WALA MTU MKE. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu." .

Maandiko hayo kwa ujumla wake yanatufundisha Mungu ndiye anaweza kuamua kumuweka mtu yoyote katika nafasi yoyote ya utumishi wa kazi ya huduma ya Mungu , huyu hivi na yule vile. Na kwa Mungu hakuna kigezo cha ubaguzi wowote wa jinsia katika nafasi yoyote ya kumtumikia .Na kwa maana hiyo WANAUME NA WANAWAKE WOTE KWA PAMOJA WANAWEZA KUWA WAHUBIRI, WACHUNGAJI, MITUME N. k.

Mwanaume huyu Akila na Mwanamke huyu Priska, mke na mume. Kwa pamoja wote wanatajwa kila mmoja wao katika kuhusika kuifanya kazi ya Mungu ya uchungaji waliokuwa nayo juu ya kanisa.
[ WARUMI 16:3-4. ]

Somo hili litaendelea sehemu ya pili........


Unakaribishwa pia kujiunga na group letu.

Mtumishi wa Mungu aliye hai.

MWL, REV:- ODRICK BRYSON

SIMU (0759 386 988; 0717 591 466) .

Whatsap group.

Email :- Odrick 16@gmail. Com.

" KWELI YOTE YA NENO LA MUNGU ISIYOGOSHIWA" .

[ 2 WAKORINTO 2:17 ]
Nilidhani kwenye maandiko yote haya nitaona linalohalalisha mwanamke kuwa mchungaji, kumbe ni tafsiri yenu tu. Niwakumbushe tu ukristo umefika hapa kwa ajili ya tafsiri hizi. Kila mmoja anajidai anaongozwa na roho mtakatifu matokeo yake tunakuwa na madhehebu kibao na yenye misimamo tofauti.

Mimi nilishakataaga kutafsiriwa biblia. Nataka nioneshwe mstari unaosema kitu moja kwa moja, over! Kwa nini wewe unitafsilie?! Kwani walioandika sinwaliongozwa na roho mtakatifu ndo wakaandika? Sasa kwa nini wewe utafute tena roho mtakatifu wa kuyabadili maandiko yao kwa kisingizio cha tafsiri??

Mimi nakataa na nitaendelea kukataa, biblia haijaruhusu mwanamke kusimama madhabahuni. Na nitakayemuelewa ni yule atakayekuja na andiko linalomruhusu moja kwa moja mwanamke kusimama madhabahuni na sio kutafsiri.

Kuna vitu vinachekesha! Hivi kwa nini maandiko hayahiyaji tafsiri kuonesha kuwa mwanamke haruhusiwi? Yaani wewe ukihitaji aruhusiwe ndo unatafuta tafsiri ili uone uwezekano wa maandiko kumruhusu mwanamke? Ina maana walioandika walikuwa hawajui kama neno kuruhusiwa lipo? Kwa nini wasiliandike? Eti wasubirie wewe uje kutafsiri kutoruhusiwa kuwe kuruhusiwa??

Mna dhambi sana mnaocheza na maandiko ya Mungu kutimiza mnachopenda kuona kinatokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
2,235
Likes
2,075
Points
280
Age
49
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
2,235 2,075 280
Tundu la sindano ndiyo,
Hyo tafsiri ingine mnajizoom tu,

Sent using Jamii Forums mobile app
thats why nasisitiza sana kusoma theolojia............Yohana yule alieenda kuchukua mwili wa BWANA baada ya ile kazi pale msalabani alikua ni mtu tajiri,,, na kwaio wapo matajiri ambao waliingia ufalme ule na wanaendelea kuingia..........


kama sindano hapo lilimaanisha tundu la sindano, tundu ambalo hata njiti ya kiberiti iwezi pita, then automatically Kristo alimaanisha matajiri hawataurithi kamwe ufalme ule........... tafsiri ambayo itakua sio sahihi


kwa sababu hio, naachia huu mjadala hapa, maana inaonekana hata simple basics za kutafsiri bible pengine zinatutatisha!..........


kama hio sentensi imekushinda kutafsiri sidhan kama ingekua/itakua vyepesi kuelewana kuhusu paulo! na maagizo yake!
 
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
2,235
Likes
2,075
Points
280
Age
49
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
2,235 2,075 280
Tafsiri za kutunga hizo,ambazo kiiila uchwao zinakuja kadri watumishi matumbo wanavyoibuka

Sent using Jamii Forums mobile app
nina mashaka wewe ni moja ya watu ambao hawaamini katika theolojia.......

pili, nina mashaka kama hata una ufahamu wa kutosha kuhusu Roho Mtakatifu (nimesoma majibizano yako na ndugu mmoja huko juu).......


tatu, nina mashaka pia kama kweli wewe ni mwanafunzi wa kweli wa Kristo (lugha ulizotumia huko juu katika mjadala huu zimenifanya nihitimishe hivi).........


kwa sababu hio, sitaweza kuongea ukanielewa, maana mambo ya Rohoni hujulikana na watu wa Rohoni....
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,013
Likes
2,531
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,013 2,531 280
nina mashaka wewe ni moja ya watu ambao hawaamini katika theolojia.......

pili, nina mashaka kama hata una ufahamu wa kutosha kuhusu Roho Mtakatifu (nimesoma majibizano yako na ndugu mmoja huko juu).......


tatu, nina mashaka pia kama kweli wewe ni mwanafunzi wa kweli wa Kristo (lugha ulizotumia huko juu katika mjadala huu zimenifanya nihitimishe hivi).........


kwa sababu hio, sitaweza kuongea ukanielewa, maana mambo ya Rohoni hujulikana na watu wa Rohoni....
Hongera mtu wa Rohoni,ambae unaamini kujitungia tafsiri ili tu ufanikishe faraja kwa ulilojitungia,
Hongera wewe unaedhani kumfahamu Roho mtakatifu ni kufuata miujiza ya wajidondoshao,
Ipo theology halisi na ipo theology mnayolishwa na wapindishao maana ili wafanikishe azma zao za kushibisha matumbo yao,hongera kwa kudhani kuwafuasa watumikia matumbo ndo kumjua Roho mtakatifu,
NB:kiBiblia na kimapokeo vyote vinapingana na hili fundisho mnaleta kwa kulivisha tafsiri mnazolishwa na wachumia tumbo,
Kumjua Roho mtakatifu ni tofauti na kumtaja,ni tofauti na kujiangusha angusha,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,013
Likes
2,531
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,013 2,531 280
thats why nasisitiza sana kusoma theolojia............Yohana yule alieenda kuchukua mwili wa BWANA baada ya ile kazi pale msalabani alikua ni mtu tajiri,,, na kwaio wapo matajiri ambao waliingia ufalme ule na wanaendelea kuingia..........


kama sindano hapo lilimaanisha tundu la sindano, tundu ambalo hata njiti ya kiberiti iwezi pita, then automatically Kristo alimaanisha matajiri hawataurithi kamwe ufalme ule........... tafsiri ambayo itakua sio sahihi


kwa sababu hio, naachia huu mjadala hapa, maana inaonekana hata simple basics za kutafsiri bible pengine zinatutatisha!..........


kama hio sentensi imekushinda kutafsiri sidhan kama ingekua/itakua vyepesi kuelewana kuhusu paulo! na maagizo yake!
Theology ipi hasa,
Yani theology ni kuamini tafsiri za kulishwa na wavuna sadaka,kwanza theolojia ni jambo ambalo mmeanza kujifunza majuzi tu maana awali mliishi kwa kujizoom tu kihisia huku mkimsingizia Roho mtakatifu,
Hiyo tafsiri uliyoitoa wala haijabeba upana wa swali uliliuliza,
Mfano wa ngamia na tundu la sindano na tajiri,una maana zaidi ya uliyoisema ww,ww umeiangalia kutoka kwenye angle moja ya uliyolishwa basi ukahitimisha kuwa maana ni hyo tu,ndo maana nilikujibu ulipouliza kifupi sana maana nilijua kwa akili ya kujizoom kujua unadhani unanitega,
Hilo fundisho ni pana zaidi ya ulichojibu,halafu umejibu jambo ambalo hata haukuuliza,wala hakuna aliyekuwa anaongelea hilo,lkn sababu ulishakarili ka tafsiri hako basi unakalazimisha popote tu ili uonekane mjuzi,
Hata kimapokeo mitume na waKristo wa mwanzo hawakuishi hili fundisho mnalolileta,Paulo anajua zaidi yenu ndo maana akaonya,hakuna cha mazingira sijui hayakumruhusu mwanamke,km ni mazingira basi Biblia nzima haituhusu maana yote imeandikwa ktk mazingira na tamaduni tofauti kabisa na yetu,
Lkn km upo huko wanakoongoza wanawake kazana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,013
Likes
2,531
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,013 2,531 280
Matumbo yanasumbua sana,ndo maana Leo nguvu ya Roho mtakatifu inatafsiriwa kutokana na nguvu ya kudondosha watu chini na kupagawa,yani nguvu ya kitabia ya shetani ya vurugu na makelele na kupagaza watu imelinganishwa kiutendaji na tabia ya nguvu ya Roho mtakatifu
Nilidhani kwenye maandiko yote haya nitaona linalohalalisha mwanamke kuwa mchungaji, kumbe ni tafsiri yenu tu. Niwakumbushe tu ukristo umefika hapa kwa ajili ya tafsiri hizi. Kila mmoja anajidai anaongozwa na roho mtakatifu matokeo yake tunakuwa na madhehebu kibao na yenye misimamo tofauti.

Mimi nilishakataaga kutafsiriwa biblia. Nataka nioneshwe mstari unaosema kitu moja kwa moja, over! Kwa nini wewe unitafsilie?! Kwani walioandika sinwaliongozwa na roho mtakatifu ndo wakaandika? Sasa kwa nini wewe utafute tena roho mtakatifu wa kuyabadili maandiko yao kwa kisingizio cha tafsiri??

Mimi nakataa na nitaendelea kukataa, biblia haijaruhusu mwanamke kusimama madhabahuni. Na nitakayemuelewa ni yule atakayekuja na andiko linalomruhusu moja kwa moja mwanamke kusimama madhabahuni na sio kutafsiri.

Kuna vitu vinachekesha! Hivi kwa nini maandiko hayahiyaji tafsiri kuonesha kuwa mwanamke haruhusiwi? Yaani wewe ukihitaji aruhusiwe ndo unatafuta tafsiri ili uone uwezekano wa maandiko kumruhusu mwanamke? Ina maana walioandika walikuwa hawajui kama neno kuruhusiwa lipo? Kwa nini wasiliandike? Eti wasubirie wewe uje kutafsiri kutoruhusiwa kuwe kuruhusiwa??

Mna dhambi sana mnaocheza na maandiko ya Mungu kutimiza mnachopenda kuona kinatokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Matumbo yanasumbua sana,ndo maana Leo nguvu ya Roho mtakatifu inatafsiriwa kutokana na nguvu ya kudondosha watu chini na kupagawa,yani nguvu ya kitabia ya shetani ya vurugu na makelele na kupagaza watu imelinganishwa kiutendaji na tabia ya nguvu ya Roho mtakatifu,
Yani wao Upole siyo nguvu ya Roho mtakatifu ila kupayuka na makelele ndiyo,Nknk,
Halafu wana kamatwa na tumaneno twa kuambiwa,NINYI NDO MNA ROHO MTAKATIFU basi wanajizooooom na kudharau kila asiye upande wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
L

Lami

Senior Member
Joined
Jan 1, 2014
Messages
102
Likes
25
Points
45
L

Lami

Senior Member
Joined Jan 1, 2014
102 25 45
Biblia, ukisoma kama maandishi ni kitabu kama vitabu vingine. Tena kwa hoja ya kimaandishi, mimi mwenyewe ni moja ya watu wanaojiuliza kuwa kulikuwa na vitabu vingapi duniani vilivyochambuliwa na kunyumbulishwa mpaka leo tuna biblia ya vitabu 72 kwa 66? Hali kadhalika wahusika wa huo uchambuzi ni kina nani? wakati mwingine huwa natamani kuwa bora vingeachwa vitabu vyooote ili tusome na tujue vitabu vyooooote. Hii ni kwa sababu kuna tafsiri kadha kadha katika biblia hizi tulizo nazo (vitabu 72 kwa 66) ndo maana kila kukicha kuna kanisa jipya kwa tafsiri mpya kabisa tena zenye upotofu wa hali ya juu kwa kisingizio cha Roho Mtakatifu.

Kwa ninachofahamu kwa elimu yangu ya bible knowledge ya O-level na divinity A-level, hatuwezi kutofautisha mafundisho yatolewayo ndani ya biblia na mila na tamaduni ya kiyahudi au mahali NENO linapofundishwa. Mf. kuna 'utata' hapo juu kuhusu maana ya ngamia kupenya tundu la sindano, kiuhalisia sio sindano hizi za kushonea nguo. Kulikuwa na eneo lenye njia nyembamba mnoo kiasi ngamia hawezi kupita mpaka ashushwe mizigo yote, akunjwekunjwe, asukumwe n.k. ndo apite, akifanikiwa kupita ndo arudishiwe mizigo ndo safari iendelee. Hilo eneo ngamia hupita kwa shida isiyoelezeka, ndo waliita kwa Kiswahili chetu 'tundu la sindano'. Tazama, ni andiko linaloreflect eneo la mahali Fulani ila lipo katika bible.

Naungana na wachangiaji waliopita kuwa theolojia ni muhimu sana kwa wahudumu wa makanisa yetu ya leo. Ili mtu aweze kutafsiri vizuri andiko Fulani, ni lazima uijue historia ya mwandishi na kinachozungumzwa katika mstari husika. Mf. ukisoma Marko, Luka na Matayo wote wanatofautiana juu ya rangi ya nguo aliyoteswa nayo Yesu. Hii haimanishi kuwa Yesu hakuwa na nguo wakati anateswa bali alivuliwa kabla hajapandishwa msalabani. Mtu mwingine anaweza akaja na hoja kuwa mwandishi Fulani ameongopa au ameandika kitu cha uongo, sivyo. Theme hapa sio rangi ya nguo bali ni kuvuliwa nguo (kudhalilishwa) kwa Yesu kabla hajapandishwa msalabani.

Biblia, ukisoma kama NENO, hautafuata ya mwilini. Tutakuwa na tafsiri kutoka kwa ROHO MTAKATIFU. Kama mtoa mada alivyonukuu maandiko, NENO haliangalii kimo, rangi, jinsia, kabila, etc vya walengwa. NENO huangaza roho imuelekee Mwenyezi Mungu muumba Mbingu na Dunia.

Nikirudi katika mada, ukisoma biblia kama maandishi yanavyosomeka, hoja ya wanawake kukatazwa kuhudumu madhabahuni haina majibu halisi, lakini ukisoma biblia kama NENO, majibu yapo mengi sana maana NENO huangaza ROHO na biblia inasema MUNGU NI ROHO NA WAMWABUDIO YAPASA KUMWABUDU KWA ROHO NA KWELI. Tofauti zetu za mwilini hazina maana yoyote kwa MUNGU.

Nawatakia uchangiaje mwema wa hii mada.
 
Mtoto wa Baba

Mtoto wa Baba

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Messages
1,697
Likes
1,899
Points
280
Age
24
Mtoto wa Baba

Mtoto wa Baba

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2018
1,697 1,899 280
Kwenye biblia sikuwahi kuona mwanamke akiwa kuhani, Nabii Wa mtume , sijui ni kwa nn ilikuw vile, Maana hata Yesu pamoja na kumheshimu Mama Maria, hakuwahi kuteua hata mtume Wa jinsia ya Kinamama.
Wenye ufafanuzi na uelewa Wa haya mambo Atupe elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
"Palikuwa na nabii mke jina lake Ana binti fanueli wa kabila ya Asheri......."

Nitakuja na mstari specific unaosema hivi kwenye biblia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,013
Likes
2,531
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,013 2,531 280
Biblia, ukisoma kama maandishi ni kitabu kama vitabu vingine. Tena kwa hoja ya kimaandishi, mimi mwenyewe ni moja ya watu wanaojiuliza kuwa kulikuwa na vitabu vingapi duniani vilivyochambuliwa na kunyumbulishwa mpaka leo tuna biblia ya vitabu 72 kwa 66? Hali kadhalika wahusika wa huo uchambuzi ni kina nani? wakati mwingine huwa natamani kuwa bora vingeachwa vitabu vyooote ili tusome na tujue vitabu vyooooote. Hii ni kwa sababu kuna tafsiri kadha kadha katika biblia hizi tulizo nazo (vitabu 72 kwa 66) ndo maana kila kukicha kuna kanisa jipya kwa tafsiri mpya kabisa tena zenye upotofu wa hali ya juu kwa kisingizio cha Roho Mtakatifu.

Kwa ninachofahamu kwa elimu yangu ya bible knowledge ya O-level na divinity A-level, hatuwezi kutofautisha mafundisho yatolewayo ndani ya biblia na mila na tamaduni ya kiyahudi au mahali NENO linapofundishwa. Mf. kuna 'utata' hapo juu kuhusu maana ya ngamia kupenya tundu la sindano, kiuhalisia sio sindano hizi za kushonea nguo. Kulikuwa na eneo lenye njia nyembamba mnoo kiasi ngamia hawezi kupita mpaka ashushwe mizigo yote, akunjwekunjwe, asukumwe n.k. ndo apite, akifanikiwa kupita ndo arudishiwe mizigo ndo safari iendelee. Hilo eneo ngamia hupita kwa shida isiyoelezeka, ndo waliita kwa Kiswahili chetu 'tundu la sindano'. Tazama, ni andiko linaloreflect eneo la mahali Fulani ila lipo katika bible.

Naungana na wachangiaji waliopita kuwa theolojia ni muhimu sana kwa wahudumu wa makanisa yetu ya leo. Ili mtu aweze kutafsiri vizuri andiko Fulani, ni lazima uijue historia ya mwandishi na kinachozungumzwa katika mstari husika. Mf. ukisoma Marko, Luka na Matayo wote wanatofautiana juu ya rangi ya nguo aliyoteswa nayo Yesu. Hii haimanishi kuwa Yesu hakuwa na nguo wakati anateswa bali alivuliwa kabla hajapandishwa msalabani. Mtu mwingine anaweza akaja na hoja kuwa mwandishi Fulani ameongopa au ameandika kitu cha uongo, sivyo. Theme hapa sio rangi ya nguo bali ni kuvuliwa nguo (kudhalilishwa) kwa Yesu kabla hajapandishwa msalabani.

Biblia, ukisoma kama NENO, hautafuata ya mwilini. Tutakuwa na tafsiri kutoka kwa ROHO MTAKATIFU. Kama mtoa mada alivyonukuu maandiko, NENO haliangalii kimo, rangi, jinsia, kabila, etc vya walengwa. NENO huangaza roho imuelekee Mwenyezi Mungu muumba Mbingu na Dunia.

Nikirudi katika mada, ukisoma biblia kama maandishi yanavyosomeka, hoja ya wanawake kukatazwa kuhudumu madhabahuni haina majibu halisi, lakini ukisoma biblia kama NENO, majibu yapo mengi sana maana NENO huangaza ROHO na biblia inasema MUNGU NI ROHO NA WAMWABUDIO YAPASA KUMWABUDU KWA ROHO NA KWELI. Tofauti zetu za mwilini hazina maana yoyote kwa MUNGU.

Nawatakia uchangiaje mwema wa hii mada.
Acha uzushi,
Ngamia ni ngamia na tundu la sindano ni tundu la sindano,
Hakuna mahali panaitwa tundu la sindano ktk mazingira aloishi Yesu,waulize walowahi enda hija watakujuza,
Tafuta Biblia hata za zamani za lugha yyte ambayo tafsiri ya kiswahili ilinyonywa humo uone km maana ni hyo usemayo,
Wengine nao wanamaana nyingine eti ngamia anaeongelewa hapa si ngamia mnyama,
Yani kila msaka tonge anakuja na tafsiri yake,

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,262,498
Members 485,586
Posts 30,123,975