Je, biblia imehalalisha mwanamke kuhubiri kanisani au kuwa mchungaji?


KijanaHuru

KijanaHuru

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2017
Messages
768
Likes
727
Points
180
KijanaHuru

KijanaHuru

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2017
768 727 180
Sehemu ya kwanza

Mistari muhimu ya kukumbuka:-

1 WAKORINTHO 14:34-36:-

34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.

35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.

36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?


1 TIMOTHEO 2:11-12:-

11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.


HII NI MADA YENYE UBISHI MKUBWA miongoni mwa vichwa vya watu wengi . Na maandiko hayo kwa kueleweka isivyo sahihi hutumiwa na baadhi ya watu wengi kujaribu kujenga hoja zao za kupinga kwamba mwanamke hana haki yoyote ya kuwa Mchungaji wala kusimama madhabahuni kuwahubiria watu kanisani.

Jambo hili limeleta mzozano mkubwa na mpasuko ndani ya makanisa mengi ya Mungu, kuhusu uhalali wa mwanamke kuhubiri madhabahuni na kuwa Mchungaji. Kuna mawazo ya positive na Negative, kuna wengine wanaona ni sahihi na kuna wengine kwao siyo sahihi kabisa .

Sasa basi ukweli na usahihi wa maandiko hayo ni upi basi? Je, ni sahihi kwamba mwanamke hatakiwi kuhubiri madhabahuni kanisani au kuwa Mchungaji ? Tatizo ni kwamba Maandiko hayo hayaeleweki vizuri kwa kwa wakristo wengi na hata baadhi ya wachungaji na Maaskofu, wanalifafanua hilo Andiko kwa maana potofu kabisa .

NB:-

Kuitwa Mtume, Nabii Askofu au Mchungaji n.k. Siyo kigezo kikubwa cha kwamba wewe unaielewa sana Biblia kwa usahihi wake. La asha ! Ndiomaana wako hata wachungaji wengine tena wengi tu ambao huyatafsiri maandiko isivyo na kuyapotosha kwa tamaa zao wenyewe.

MWALIMU MKUU WA BIBLIA NI ROHO MTAKATIFU; yeye ndiye aliyeyaleta maandiko hayo kwetu. Na hatuwezi sisi kuamua kuyatafsiri maandiko hayo vyovyote tu kama apendavyo mtu fulani kutafsiri. La Asha
[ 2 PETRO 1:19-20 ] .
Bali katika kanuni za kuyatafsiri maandiko, tunahitaji sana maongozi ya msaada wa Roho Mtakatifu mwenyewe katika kuyasoma na kuyaelewa maandiko vizuri na kuyatafsiri kwa usahihi wake. Neno la Biblia. Tunaweza kulifaham kwa kufunuliwa na Roho Mtakatifu pekee yake. Ndiomaana Yesu alisema uliwaficha wenye hekima na Akili (Wasomi), ukawafunulia watoto wachanga (Watu wasio na elimu) . Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza mbele zako [ MATHAYO 11:25-26]. "Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho Mtakatifu . Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu " .
[1 WAKORINTHO 2:10-15].

Si hilo tu. Nikodemo alikuwa ni mwalimu mkuu wa chuo cha Torati. Na watu walimwamini sana katika Taifa la Israeli. Lakini Nikodemo alipoambiwa na Yesu maneno mepesi tu ya Mungu , na usomi wake wote, alishindwa kuyaelewa maana yake nini !! Sasa Yesu ambaye hakupita chuo chochote cha Theolojia, ikambidi amfundishe Nikodemo, mwalimu mkuu wa chuo cha Theolojia ya Torati.
[ YOHANA 3:1- 10 ]

Sisemi wala kupinga kwamba kusoma chuo cha Biblia ni kosa au ni vibaya, au ni dhambi. Hapana. Ni nini maana ya kuanza kukwambia hayo. Maana yangu ni hii kwamba :- Ondoa dhana potofu ukafikili kila mtu anayeitwa Mchungaji, Askofu au Mwanatheolojia fulani msomi anaielewa sana Biblia ki-maana. Ukiwa na mawazo hayo tu, utapotezwa na kudanganyika sana Mpendwa . Na Mungu huwa hatendi kazi kwa misingi hiyo. Mchungaji /Ev/ Mwanatheolojia huyo Anaweza kuielewa Biblia kwa namna fulani tu ya akili hivi , lakini asiweze kabisa kuielewa Biblia kwa jinsi ya rohoni zaidi kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu . Na maana ya kweli ya maneno ya Biblia hutumbalikana kwa jinsi ya rohoni zaidi na sio kwa jinsi ya mwilini.
[ WAGALATIA 1:11-12 ; WAEFESO 1:17-19].

Hivyo ni vema zaidi tusiweke vipimo vyetu vya usomi kama kigezo cha kuitafsiri Biblia; bali tumuhitaji sana Roho wa Mungu ndio atuongoze katika kulitafsiri Neno lake Mungu.

Je, ni halali Mwanamke kuhubiri au kuwa Mchungaji?

Jibu :- Ni ndiyo kwa herufi kubwa.

Tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele vinne. Ambavyo ni :-

(1) HOJA POTOFU KUHUSU MWANAMKE KUTOKUWA MCHUNGAJI / MUHUBIRI.

(2) UHALALI WA MWANAMKE KUHUBIRI / KUFUNDISHA KANISANI .

(3) UHALALI WA MWANAMKE KUWA MCHUNGAJI

(4) UFAFANUZI WA ANDIKO LA 1 WAKORINTHO 14:34-35 NA 1 TIMOHEO 2:12 .

KIPENGELE NO:1

HOJA POTOFU KUHUSU MWANAMKE KUTOKUWA MCHUNGAJI/ MUHUBILI .

Ukiwasikia watu wengi wanaopinga mwanamke kuhubiri au kuwa Mchungaji. Mbali na kutumia Andiko la 1 Wakorintho 14:34-35 na 1 Timoheo 2:12-15 katika ufafanuzi wao .

Pia watajenga hoja yao nyingine ni kwamba MWANAMKE NI KIUMBE DHAIFU na hivyo wataeleza mengi tu katika kufafanua hoja yao hii.

Lakini mbele za Mungu, hoja ya mwanamke kutokuhubiri au kuwa Mchungaji kwa sababu eti ni kiumbe dhaifu. Hoja kama hii haikubaliki na wala haina maana yoyote. Kwa sababu Biblia inasema kwamba Hao hao watu walio dhaifu machoni petu ndio Mungu anayewachagua kuwa watumishi wake . Neno la Mungu linasema katika

1WAKORINTHO 1: 26-29:-" Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; TENA MUNGU ALIVICHAGUA VITU VINYONGE VYA DUNIA NA VILIVYODHARAULIWA (WANAWAKE), naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu."

Kwa maana hiyo ni muhimu kuzidi kuelewa na kufaham vizuri kwamba siku zote Mungu huwa hamchagui mtu yoyote kuwa mtumishi wake katika ngazi yoyote ya utumishi wa kihuduma kwa sababu tu ya kigezo cha jinsia yake kwamba ni kike au kiume. Hapana. Mungu hachagui mtu yoyote kwa kigezo cha sifa, umri, cheo au jinsia yake. Mungu huwa hatumikiwi wala kutenda kazi kwa misingi hiyo. Biblia inatuambia katika

1 SAMWELI 16:7-10 :-

7. Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA HAANGALII KAMA BINADAMU AANGALIAVYO; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

8. Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, BWANA hakumchagua huyu .

9. Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala BWANA hakumchagua huyu .

10. Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, BWANA hakuwachagua hawa .

WAFILIPI 3:3-4:-"Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, WALA HATUUTUMAINI MWILI. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi."

Kwa sababu hiyo. Mungu katika mpango wake anaweza kumchagua mtu yoyote yule bila kujali sifa yake, umri wake au jinsia yake kwamba ni mwanamke au mwanaume , Mungu anaweza kumchagua awe mtumishi wake katika ngazi yoyote ya utumishi na tena akamtumia kwa viwango visivyo vya kawaida. Kwa hiyo sisi wanadamu hatupaswi kuamua kumpangia Mungu kwamba mwanamke hawezi kuwa Mchungaji au muhubiri. Kivipi !? TUSILETE MFUMO-DUME NDANI YA KANISA LA MUNGU . Hilo ni chaguo la Mungu sio la kwako wewe mwanadamu. Na kwa maana hiyo Mungu akiamua kumchagua mwanamke kuwa Mchungaji, Askofu, Mwinjilisti, mtume, Nabii n. k. Atakuwa hivyo Mchungaji, mtume, Nabii na kadhalika. Biblia inasema katika

WARUMI 9:11-16 :-"
(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye) , aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia. Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!
Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu."

WAEBRANIA 5:4:-" Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ILA YEYE AITWAYE NA MUNGU , kama vile Haruni ".

Na kwa maana hiyo. Ngazi yoyote ya utumishi katika huduma mtu huwekwa na Mungu . Mungu akiamua kumwita mwanamke awe mchungaji, atakuwa ni Mchungaji tu na Mungu atajidhihirisha kwake kwa kumthibitisha kwamba yeye ndiye aliyemuita. Wako wachungaji wanawake na wahubiri duniani ambao Mungu anawatumia kwa viwango vya juu sana katika huduma zao . Hatuwezi kukanusha na kupinga utumishi wao kwa sababu tu ya kijinsia. Yesu alisema kama hamniamini mimi, ziamini zile kazi , kwa kuwa kazi zenyewe zanishuhudia ya kwamba Baba Mungu amenituma .
[ YOHANA 5:36; YOHANA 10:25, 36-38; YOHANA 14:10-12].

HOJA YAO YA PILI.

Watasema hata maandiko yanamtaja kwamba mwanaume ndiye anayepaswa kuwa Mchungaji (Askofu). Uaskofu ni ngazi ya juu ya madaraka ya kichungaji .

Na watatumia Andiko lao hili lifuatalo katika
1 TIMOHEO 3:1-12:-

1-7. Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu , atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, MUME(MWANAUME) wa mke mmoja , mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)
Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.

8-12. Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu; wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
Mashemasi na wawe WAUME wa mke mmoja , wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu. "

Ni muhimu kuelewa vizuri Andiko hilo kwa kusema mwanaume hapo ndiwe Askofu . Haimanishi kwamba basi limemkataza Mwanamke asiwe mchungaji au Askofu. Hapana. Kwa sababu ukitazama mukadha mzima wa maelezo yote ya Andiko nzima, yameendelea kusema pia " MASHEMASI NA WAWE WAUME wa mke mmoja " . Sasa Je, kwa kusema hivyo tuseme Paulo Mtume hapo hakuwaruhusu pia wanawake wasiwe washemasi kwa sababu tu amewataja wanaume? Jibu ni hapana.

Tunaona pia walikuwepo MASHEMASI WANAWAKE ambao pia Paulo mtume aliwachagua katika kanisa. Ukisoma katika WARUMI 16:1 , Biblia inasema:- " Namkabidhi kwenu Fibi, Ndugu yetu, aliye muhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea" . Mstari huo katika Biblia ya kingereza ya New International Version , unasomeka hivi, Romans 16:1:-" I commend to you our Sister Phoebe, a Servant (deaconess) of the church in Cenchrea" .

Kwa hiyo tunaona hapo juu ya Shemasi Mwanamke ingawa katika Waraka wa Timotheo wanatajwa tu kuwa mashemasi wanaume tu. Kwa maana hiyo tunapata kuelewa kwamba Andiko la 1 TIMOTHEO 3:1-12 , Ingawa liliwataja maaskofu na mashemasi kuwa wanaume hapo , lakini hakumaishi kwa wanaume tu pekee yao , bali hata wanawake pia wanaweza kuwa mashemasi, na vilevile wachungaji (maaskofu) pia kwa msingi huo.

Ni muhimu kuyaelewa maandiko ya Biblia vizuri sio kila mahali andiko linapotaja jambo kwa upande mmoja linamainisha tu kwa upande mmoja pekee yake . Hapana. Linaweza kutajwa kwa upande mmoja, lakini halikumainishi kuishia tu kwa upande mmoja, bali kwa pande zote mbili . Kwa mfano , Yesu alisema, kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake [ MATHAYO 5:27-28].

Sasa Swali la ufaham :- Andiko hilo hapo linamgusa tu mwanaume kumtamani mwanamke ndio dhambi. Lakini Je, tuseme mwanamke naye akimtamani mwanaume kiuasherati, itakuwa siyo dhambi? Kwa sababu tu eti Andiko hilo limemtaja tu mwanaume hapo? Jibu ni la!

Na kwa msingi huo huo hata kama Biblia imewataja wanaume kuwa ndio wawe maaskofu na mashemasi. Neno hilo halikuishia kumainisha tu kwa wanaume pekee yao bali hata kwa wanawake pia wanaweza kuwa wachungaji au maaskofu, mashemasi, mitume, manabii n.k.

Ni muhimu kufaham Biblia inasema katika MATENDO 10:34-35:-

" Petro akafumbua kinywa chake, akasema, HAKIKA NATAMBUA YA KUWA MUNGU HANA UPENDELEO; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. "

Kusema kwamba mwanaume tu ndio anayepasa kuhubiri na kuwa Mchungaji lakini mwanamke hafai kwa lolote. Huo ni upendeleo. Mungu wetu hana upendeleo wa aina yoyote ile , kila mtu awe ni mwanaume au mwanamke bado Mungu anaweza kuwatumia wote sawasawa katika nafasi yoyote ile ya utumishi iwe ni uchungaji na kadhalika.

Ni muhimu kufaham katika suala la utumishi wowote mbele za Mungu. Mwanaume hawezi kujivuna na kujiinua kwamba yeye anastahili sana zaidi ya mwanamke. Katika imani ya wokovu iliyobeba utumishi ndani yake, sisi wote ni sawasawa mbele za Mungu. Hakuna mmoja aliye bora wa kujiinua juu zaidi ya mwingine. Biblia inasema katika

1 WAKORINTHO 12:17-27:-

" BALI MUNGU AMEVITIA VIUNGO KILA KIMOJA KATIKA MWILI KAMA ALIVYOTAKA . Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi. Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana . Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe . Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho . Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza.............."

YOHANA 6: 28-29:-
"Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate KUZITENDA KAZI ZA MUNGU ? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye."

WAGALATIA 3:26-29:-

"Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. HAPANA MTU MUME WALA MTU MKE. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu." .

Maandiko hayo kwa ujumla wake yanatufundisha Mungu ndiye anaweza kuamua kumuweka mtu yoyote katika nafasi yoyote ya utumishi wa kazi ya huduma ya Mungu , huyu hivi na yule vile. Na kwa Mungu hakuna kigezo cha ubaguzi wowote wa jinsia katika nafasi yoyote ya kumtumikia .Na kwa maana hiyo WANAUME NA WANAWAKE WOTE KWA PAMOJA WANAWEZA KUWA WAHUBIRI, WACHUNGAJI, MITUME N. k.

Mwanaume huyu Akila na Mwanamke huyu Priska, mke na mume. Kwa pamoja wote wanatajwa kila mmoja wao katika kuhusika kuifanya kazi ya Mungu ya uchungaji waliokuwa nayo juu ya kanisa.
[ WARUMI 16:3-4. ]

Somo hili litaendelea sehemu ya pili........


Unakaribishwa pia kujiunga na group letu.

Mtumishi wa Mungu aliye hai.

MWL, REV:- ODRICK BRYSON

SIMU (0759 386 988; 0717 591 466) .

Whatsap group.

Email :- Odrick 16@gmail. Com.

" KWELI YOTE YA NENO LA MUNGU ISIYOGOSHIWA" .

[ 2 WAKORINTO 2:17 ]
 
Prosper Habona Eliti

Prosper Habona Eliti

Member
Joined
Apr 8, 2016
Messages
5
Likes
2
Points
5
Prosper Habona Eliti

Prosper Habona Eliti

Member
Joined Apr 8, 2016
5 2 5
Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu, somo zuri limenijenga sana.
 
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2017
Messages
2,856
Likes
2,777
Points
280
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2017
2,856 2,777 280
Imani ya Kikristo ni tofauti na imani nyingine.
Neno la Kristo ni hai na linafanya kazi muda wote.
Hivyo basi Maamuzi ya Roho Mtakatifu ndiyo yanayopewa kipaumbele hata kama hayakuwahi kutokea hapo awali, muda wote anaweza amua chochote na kikafanya Kazi Njema kama inavyompendeza yeye, na sio kinachotupendeza sisi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
T

tikakami wa lopelope

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Messages
1,379
Likes
638
Points
280
T

tikakami wa lopelope

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2017
1,379 638 280
Mwl, Mch OB asante. Sehemu ya pili ya somo hili naipata kwa njia gani?

Kwenye Imani nyingine wanaambiwa Roho Mtakatifu ndiye Mtume Muhamad SAW. Unawasaidiaje wasidanganywe?
 
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,013
Likes
2,531
Points
280
popbwinyo

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,013 2,531 280
livafan

livafan

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2016
Messages
1,133
Likes
1,107
Points
280
Age
28
livafan

livafan

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2016
1,133 1,107 280
Kwenye biblia sikuwahi kuona mwanamke akiwa kuhani, Nabii Wa mtume , sijui ni kwa nn ilikuw vile, Maana hata Yesu pamoja na kumheshimu Mama Maria, hakuwahi kuteua hata mtume Wa jinsia ya Kinamama.
Wenye ufafanuzi na uelewa Wa haya mambo Atupe elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
shungurui

shungurui

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2008
Messages
2,685
Likes
2,995
Points
280
shungurui

shungurui

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2008
2,685 2,995 280
Wapo, ukisoma agano jipya utakutana na nabii Anna.
Kwenye biblia sikuwahi kuona mwanamke akiwa kuhani, Nabii Wa mtume , sijui ni kwa nn ilikuw vile, Maana hata Yesu pamoja na kumheshimu Mama Maria, hakuwahi kuteua hata mtume Wa jinsia ya Kinamama.
Wenye ufafanuzi na uelewa Wa haya mambo Atupe elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
2,235
Likes
2,075
Points
280
Age
49
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
2,235 2,075 280
Kwenye biblia sikuwahi kuona mwanamke akiwa kuhani, Nabii Wa mtume , sijui ni kwa nn ilikuw vile, Maana hata Yesu pamoja na kumheshimu Mama Maria, hakuwahi kuteua hata mtume Wa jinsia ya Kinamama.
Wenye ufafanuzi na uelewa Wa haya mambo Atupe elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
manabii wa kike mbona wengi?......


msome pia debora, alikua nani
 
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
2,235
Likes
2,075
Points
280
Age
49
dong yi

dong yi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
2,235 2,075 280
Wapo, ukisoma agano jipya utakutana na nabii Anna.

Sent using Jamii Forums mobile app
hawasomi biblia, wala hawapendi kujifunza........


shida ya wakristo wa leo hawapendi kusoma theolojia.......


kuna baadhi ya mambo mitume waliandika kutokana na tamaduni za watu waliohubiriwa injili sehemu hizo.........


ukijiuliza kwann paulo alizuia wanawake kuhubiri, utalazimika kujifunza theolojia, na vitu vyake!..... hata leo wanaweza kuzuiwa kama hawatatii, its very simple!
 
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2018
Messages
4,763
Likes
1,944
Points
280
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2018
4,763 1,944 280
Mwl, Mch OB asante. Sehemu ya pili ya somo hili naipata kwa njia gani?

Kwenye Imani nyingine wanaambiwa Roho Mtakatifu ndiye Mtume Muhamad SAW. Unawasaidiaje wasidanganywe?
Unaweza kuthibitisha hili dai lako?
 
live on

live on

Member
Joined
Dec 30, 2018
Messages
42
Likes
47
Points
25
live on

live on

Member
Joined Dec 30, 2018
42 47 25
Wewe uliyeandika hu Uzi tambua kuwa

Hadi Yesu anapaa mbinguni
Hajaacha jengo linaloitwa kanisa
Hajaacha mtu anaeitwa padri
Hajaacha mtu anaeitwa mchungaji
Hajaacha mtu anaeitwaa sister
Hajaacha mtu anaeitwa papa
Hajaacha kitabu kinachoitwa wakoritho su wagaratia

Hayo yote wameanzosha wazungu na kushanga unamuhusisha Yesu katika mambo asiyo yajua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vi rendra

Vi rendra

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Messages
941
Likes
1,106
Points
180
Vi rendra

Vi rendra

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2017
941 1,106 180
WAKORINTHO 14:34-36:-

34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.

Heed my order!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2017
Messages
2,856
Likes
2,777
Points
280
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2017
2,856 2,777 280
Mungu kupitia kwa kinywa cha Nabii Yoeli, ametuambia

Yoeli 2
" 28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu "


Mungu pia anatukumbusha maagizo hayo katika Matendo ya Mitume 2
Kwa kusema

" 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri "

Unabii huu ni lazima Utimie hata kama hapo awali haukuagizwa, wakati wa kutimia Unabii huu ni sasa.
Kama wewe ni Mkristo hebu bofya kwenye tovuti ya
"You tube"
Halafu andika,

" Sermon With Avangalist Yinka "

Halafu sikiliza hapo maneno na matendo yanayo fanyika, halafu useme hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu au la.

Wenye Macho na Masikio wanaona na wanasikia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,262,481
Members 485,588
Posts 30,123,421