Elections 2010 Je Baregu, Marando walimsaidiaje Dr Slaa kuhusu wizi wa kura na uchakachuaji matokeo?

H6MohdH6

Member
Oct 8, 2010
43
0
Prof Baregu alikuwa Mwenyekiti wa Kampeni ya Urais ya Bw. Mrema mwaka 1995 ambapo kulikuweko na uchakachuaji mkubwa wa kura uliomwezesha bwana Mkapa na CCM kuupora ushindi na kuwa Rais wakati Bw Marando amekuwa mtu wa ndani ya Usalama wa Taifa kwa muda mrefu. Kwa misingi hiyo, wote wawili wana uzoefu na swali la wizi wa kura: Baregu kwa kuibiwa tena mwaka 1995 na Marando kwa kujua undani wa utendaji wa UWT. Je, walitumiaje uzoefu wao na ujuzi wao kumtahadharisha Dr Slaa na kukiweka Chadema katika mkao wa kupambana na uchakachuaji huo? Au walikuwa wanasema "subiri tuone?"
 
Oct 5, 2010
20
0
Tatizo ni kwamba mbinu za wizi wa kura za mwaka 2010 ni tofauti na za 1995. Hawa CCM wanabadilika kama vinyonga. Ndio maana nasema CCM mzuri ni yule aliyekufa.
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,524
2,000
Prof Baregu alikuwa Mwenyekiti wa Kampeni ya Urais ya Bw. Mrema mwaka 1995 ambapo kulikuweko na uchakachuaji mkubwa wa kura uliomwezesha bwana Mkapa na CCM kuupora ushindi na kuwa Rais wakati Bw Marando amekuwa mtu wa ndani ya Usalama wa Taifa kwa muda mrefu. Kwa misingi hiyo, wote wawili wana uzoefu na swali la wizi wa kura: Baregu kwa kuibiwa tena mwaka 1995 na Marando kwa kujua undani wa utendaji wa UWT. Je, walitumiaje uzoefu wao na ujuzi wao kumtahadharisha Dr Slaa na kukiweka Chadema katika mkao wa kupambana na uchakachuaji huo? Au walikuwa wanasema "subiri tuone?"

Mwaka huu uthibiti ni wa hali ya juu sana kiasi kwamba wameumbuka. Wewe kipofi au mzito kufikiri au uwezo wako mdogo sana wa kupambanua na kuoanisha mambo ndio maana uelewi kinachofanyika na Chadema.
 
ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,158
2,000
Uchakachuaji wakuu unaanzia kule kule zinakotengenezwa hizo karatasi, kwa kifupi wizi wa safari hii ulikuwa Logical in other words (hauonekani kwa macho NOT PHYSICAL), kwa akili ya kawaida utagundua tu umeibiwa lakini proove how inakuwa ngumu.

Mfano mzuri ni Majimbo yote ambayo CHADEMA imeshinda, angalia kura za Rais utagundua ni mchezo mchafu.
 
dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,726
1,500
prof baregu alikuwa mwenyekiti wa kampeni ya urais ya bw. Mrema mwaka 1995 ambapo kulikuweko na uchakachuaji mkubwa wa kura uliomwezesha bwana mkapa na ccm kuupora ushindi na kuwa rais wakati bw marando amekuwa mtu wa ndani ya usalama wa taifa kwa muda mrefu. Kwa misingi hiyo, wote wawili wana uzoefu na swali la wizi wa kura: Baregu kwa kuibiwa tena mwaka 1995 na marando kwa kujua undani wa utendaji wa uwt. Je, walitumiaje uzoefu wao na ujuzi wao kumtahadharisha dr slaa na kukiweka chadema katika mkao wa kupambana na uchakachuaji huo? Au walikuwa wanasema "subiri tuone?"

watanzania ndo tudai tume huru na sio vyama vya ushindani peke yao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom