Je, Baraza la Mawaziri linawatendea haki watanzania bila kuwa na baraka zao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Baraza la Mawaziri linawatendea haki watanzania bila kuwa na baraka zao?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fasta fasta, May 17, 2011.

 1. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Baraza la Mawaziri latupiwa lawama kukubali wakimbizi
  NA DEGE MASOLI
  17th May 2011

  Baraza la Mawaziri limetupiwa lawama kwa kile kilichodaiwa kumshauri vibaya Rais Jakaya Kikwete, kuhusiana na kukubali ombi la jumuiya ya kimataifa la kutaka kutoa uraia na ardhi kwa wakimbizi wa Burundi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, mmoja wa wanaharakati wa haki za binaadamu mkoani hapa, Aseli Shewally, alisema kitendo cha Rais kukubali ombi la jumuiya ya kimataifa kutoa uraia na ardhi kwa raia wa Burundi bila kuliwasilisha kwa wadau na wananchi, kinaonyesha kwamba mawaziri wake hawakumpa ushauri mzuri.
  Jumla ya kaya 1,700 raia wa Burundi zimeombewa makazi nchini na jumuiya ya kimataifa, ambapo kaya 800 zitapelekwa wilaya ya Handeni, kaya 700 wilaya ya Kilindi na kaya 200 wilaya ya Mkinga, zote za mkoa wa Tanga na zilizobaki zitapelekwa mikoa ya Kusini.

  Shewally ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo kwa Vijana Mkoa wa Tanga (TAYODEA), alikosoa kuwa wananchi wa maeneo husika hawakuhusishwa na ujio wa wageni hao, jambo ambalo linaweza kuleta hali ya uvunjifu wa amani na kutoelewana.
  Alitoa mfano wa ombi kama hilo lililowahi kutolewa mwaka 1978 na aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Abrialimana, kumtaka Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere kutoa ardhi kwa raia milioni moja wa nchi hiyo kuishi hapa nchini, ombi ambalo lilikataliwa.

  "Mawaziri wa wakati huo walikuwa makini, walifanya tafiti juu ya wageni hao na walimshauri Rais kukataa baada ya kubaini kuwa raia waliyoombewa hifadhi ni wahalifu wakubwa kule nchini kwao na waliyobaki ni wazee ambao si nguvu kazi, sasa kwa hawa utafiti gani umefanyika?", alihoji Shewally.
  Kutokana na hali hiyo mwanaharakati huyo alitoa ushauri kwa Rais kusitisha uamuzi huo na badala yake suala hilo lipelekwe Bungeni, ambako litapatiwa ufumbuzi wa kukubaliwa ama kukataliwa.

  Gazeti la Nipashe
   
 2. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Gusa vingine...but siyo ARDHI! Patachimbika sana ,Kenya na Uganda hawana ardhi nzuri hivo wanimezea mate ya kwetu
   
 3. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Sasa Tanzania imekuwa dampo la kutupia kila kitu. Wameshindwa kutatua matatizo ya watanzania leo wanaongeza kero nyingine tena. Tunaomba viongozi wetu wawe makini sio kila kitu wanaamua wenyewe wajue wananchi ndio wanaopata usumbufu wakati wao wapo magesti, masaki osbarbay. Yaani huu usumbufu wa wawekezaji wanavyowasumbua wanavijiji hawajaona madhara yake au ndio wanataka vita.
   
 4. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Si sahihi kulitupia lawama na tuhuma baraza la Mawaziri ati limemshauri vibaya Rais. Mh. Rais analijua vizuri tatizo la wakimbizi na madhara yao kwa ustawi wa nchi yetu kuliko Mawaziri wengi tu waliomo kwenye baraza hivi sasa, tusipotoshwe katika hili. Tumezidi kukubali kila kitu bila kufikiria vema madhara ya baadaye.
   
 5. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,238
  Likes Received: 931
  Trophy Points: 280
  Cha muhimu tukubaliane Watanzania wote wenye nia njema na Taifa ili,wanasiasa,viongozi wa dini na jumuiya mbalimbali,watu na taasisi binafsi kumtangaza rais Jakaya mrisho kikwete ni Janga la Kitaifa ili kila mmoja afikiri na kubuni jinsi ya kuondokana na janga hilo
   
 6. Niko

  Niko Member

  #6
  May 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi kila anachoamua/fanya Rais kashauriwa na mtu?
   
Loading...